Mishahara ya walimu kulipwa kutokana na vyuo walivyosoma?

mbona mm sielewi hili swali?? je kwann mada ibase kwa waalim kulipwa kutokana na vyuo halaf ndani tunaambiwa madaktar na manesi na bcom???

labda ubongo wangu umelel unashindwa kuamka ukaelewa.
 
Kama ni serikalini kuna salary scale (TGTS) katika kada ya ualimu,hivyo chuo ulichotoka si kigezo cha mshahara ilimradi chuo hicho kinatambulika rasmi,ILA kwa shule binafsi lolote linaweza kutokea kutokana na ushindani wa soko huria ambako vitu kama uzoefu,masomo uliyosomea (say sayansi au sanaa),chuo ulichotoka na kuwa nondo (competent) vinaweza kupelekea uwe na mpunga mrefu!:target:
 
Tatizo waliosoma vyuo vya kata hawajiamini wawapo kazini hata akiulizwa umesoma chuo gani anajibu kwa hofu, na wengine ni vilaza kweli wamebeba ma GPA makubwa hawana confidence ya kuyatumai, mlolongo wa namna alivyosoma ameunga ni balaa ana vyeti 3 vya olevel 2vya Alevel.hasa hao walimu sio wote ila wengi ni matatizo, wapo kazini kwangu tena toka vyuo mbalimbali vya kata hawajiamini. lakini fanya uchunguzi mdogo kujua wanafunzi wa ualimu wanao soma sauti,tumaini,teku,m.meru,arusha n.k background yao wengi walikuwa vilaza toka sekondari,nani hapendi kusoma udsm, sua vyuo vikubwa?naongelea kwa walimu. mkwawa na duce hawana shida ilahao wanaotoka private university hawajiamini ndo maana wanaonekana hawafai.lakini kuna mmojammoja wapo vizuri kichwani.

Ubongo wako umejaa matope sana,ambacho mleta mada hakiafiki wewe ndiyo umekomalia
 
Jamaa yangu Practical bila Theory basi hata darasa la 7 Humshindi kwa Practically
Ujenzi kuna jamaa kibao ni mafundi Uashi na wanachapia Maghorofa ripu sio Mchezo lakini jamaa wanaotoka UDSM hata kushika mwiko au mkono bawa hawaujui au hawajui je Mshahara watalingana?
Chukulia Ma Dr Hospitalini utachukulia uzoefu wa miaka mingi au waliotoka Muhimbili na Urusi
Yaani kuna tofauti sana ya kitabu na uzoefu mfano wa mwisho mafundi wa TTCL na Analogy zao utawashindanisha na wahitimu wa sasa hivi wa IT kwanini TTCL isife ki-Silencer wakiwa na Mafundi waliosomea Posta na Simu wakiwapisha Vodacom Airtel, tiGo na Makampuni mengine inayowasomesha kila siku Technolojia inapobadilika tena huko nje sio DIT au Arusha Tech na theory za 1970 (Analogy)
Kwa hiyo Mwalimu anayefundisha VETA somo la Computer ni Tofauti mashahara na anayefundisha masomo hayohayo UDSM, UDOM nk
Mishahara serikaliniinategemea vitu vitatu
Idadi ya miaka kusomea fani husika
Asilimia ya kurisk
Mahitaji ya soko na uhaba wa wahitimu
Kwenye mashirika ya umma kuna tofauti ya skeli tu yaani skeli zipo juu kwa sifa linganifu.
Kuhusu uwezo wa utendaji huwezi linganisha technician na bachela holda ( when other fsctor remain constant) always technician atakuwa juu praktiko.
 
Jamaa yangu Practical bila Theory basi hata darasa la 7 Humshindi kwa Practically
Ujenzi kuna jamaa kibao ni mafundi Uashi na wanachapia Maghorofa ripu sio Mchezo lakini jamaa wanaotoka UDSM hata kushika mwiko au mkono bawa hawaujui au hawajui je Mshahara watalingana?
Chukulia Ma Dr Hospitalini utachukulia uzoefu wa miaka mingi au waliotoka Muhimbili na Urusi
Yaani kuna tofauti sana ya kitabu na uzoefu mfano wa mwisho mafundi wa TTCL na Analogy zao utawashindanisha na wahitimu wa sasa hivi wa IT kwanini TTCL isife ki-Silencer wakiwa na Mafundi waliosomea Posta na Simu wakiwapisha Vodacom Airtel, tiGo na Makampuni mengine inayowasomesha kila siku Technolojia inapobadilika tena huko nje sio DIT au Arusha Tech na theory za 1970 (Analogy)
Kwa hiyo Mwalimu anayefundisha VETA somo la Computer ni Tofauti mashahara na anayefundisha masomo hayohayo UDSM, UDOM nk
Hongera ila ulipofikia ttcl umenikumbusha kitu. Japo hutaweza amini.unafahamu kuwa walioanzisha mobitel na celtel walitokea huko? Je uunafahamu kuwa kuna watu wako tcra ya leo( branch ya ttcl by then) wanafundisha it parttimer vyuo vikubwa huko dunia ya kwanza? Pia wapo wataalam wa ttcl ambao waliacha kaz na kufanya kazi za kivumbuzi kwenye makampuni ya kutengeneza handset zenye jina duniani kwa elimu hizo hizo? Kuna watu walisoms teknolojia ambayo imekuja kuingia nchini miaka 20 baadae huko huko ttcl.Hata hapa ilipo ttcl mumshukuru mungu wengine mmezaliwa mmeikuta bado ila kwa kifupi Ilipewa adhabu ya kifo bahati mbsya kitanzi kilikatika kabla haijafa
 
Back
Top Bottom