Mishahara ya Wake Zetu

Mishahara ya Wake Zetu

hihihiiiii mbona unataka kunibana? leo tunaongelea wanaume bana....

Hahahahahahhahhahahhaha,

Nimekuelewa mdogo wangu BT...Itabidi next time tuchukulie kuwa wanaume na wanawake wanaishi independent of each!
 
natamani nianze kuleeleze babu lakini muda umeshaenda sana!kesho utakuta majibu yangu asubuhi!

Hahahahahahahh...

Umechelewa kwa bed?

Hebu wahi bwana, tumechoka sana kuamua kesi na kushauri kusikoisha!
 
Mkuu, mambo ni mchanyato wanaume wengine hukomba hela zote za wake zao na wengine hawajui hata kiasi gani wanapata na zinafanya nini wengine wanaweka katika kikapi kimoja kisha wanakubaliana watumieje. wanaume wengine ni lazima wasalimishe hela zote kwa wake zao kisha waanze kuomba. mimi nimempa uhuru na hela zake naye nikamwamdia anipe uhuru ma mambo yanaenda vizuri tu. kwa hivo nikitaka kumsaidia yeyete dume au jike ndugu au rafiki sina shida ya kujieleza. sasa wew tafuta lipi linafaa zaidi
 
Mmmh kila mtu anaplan zake.... kwakweli naheshimu hilo. Mimi kwakweli kuchanga na mume kwenye mjengo ni kitu ambacho I will do in writing na any case warithi au wamiliki wanakuwa ni watoto wetu tu. Wanawake wengi weshalizwa, at the time of divorce or death, linatoka rundo la watoto na wote wanahaki kurithi ambapo wewe umetia jasho lako.
MadameX,

Naomba ukasome vizuri sheria ya ndoa au omba wataalamu wakusaidie kutafsiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtoto wa nje ya ndoa hawezi kurithi mali ya ndoa labda kama baba kamwandikia urithi kwenye wosia.

Na pia ujue kuwa mali za ndoa ni za mume na mke 50 kwa 50%.

Kwa hiyo hoja zako hapa zimetoka nje kidogo!

Pesa ya mwanamke hua ni chungu sana, Wabinafsi sana hawa viumbe....

Wewe inaonekana huwajui wanawake. Hakuna watu rahisi wa kula pesa zao kama wanawake. Bahati mbaya watu wengi hawayajui hayo.

Yaani ukimpa imani na kumhandle vizuri....mshahara wote na hata kama kapata deal anakubwagia kitandani uamue cha kufanyia!.. Anaweza pia kuchukua mkopo na kukukabidhi pesa yote.

Tatizo ni kwamba watu hawajui button sahihi ya kubonyeza, wanaishia kubonyeza bonyeza na mwisho wanafanya permanent disconnection ya network!
 
Last edited by a moderator:
wewe mie nshajua unachotaka sema...

sasa mie nakwambieni nyote...mwanamke mwema ni yule ambaye wala hana shida na pato lake ...achilia ATM card lazima mwisho wa mwezi ibaki kwa mume.. mwanamke anabaki na kiasi cha mboga na saloon tu..
Ikumbukwe kuwa mme ndio kichwa cha nyumba....

tuacheni tujenge familia.

Kwa sababu ni kichwa cha familia ndo nimpe ATM card yangu?
 
MadameX,

Naomba ukasome vizuri sheria ya ndoa au omba wataalamu wakusaidie kutafsiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtoto wa nje ya ndoa hawezi kurithi mali ya ndoa labda kama baba kamwandikia urithi kwenye wosia.

Na pia ujue kuwa mali za ndoa ni za mume na mke 50 kwa 50%.

Kwa hiyo hoja zako hapa zimetoka nje kidogo!

Wewe inaonekana huwajui wanawake. Hakuna watu rahisi wa kula pesa zao kama wanawake. Bahati mbaya watu wengi hawayajui hayo.

Yaani ukimpa imani na kumhandle vizuri....mshahara wote na hata kama kapata deal anakubwagia kitandani uamue cha kufanyia!.. Anaweza pia kuchukua mkopo na kukukabidhi pesa yote.

Tatizo ni kwamba watu hawajui button sahihi ya kubonyeza, wanaishia kubonyeza bonyeza na mwisho wanafanya permanent disconnection ya network!

ulijuwaje? hebu wafundishe bana......hata mie mwanzoni ilkuwa hivyo hivyo nikipata chochote naleta hm chote, namkabidhi...ila jamaa hakujuwa button sahihi akabonyezabonyeza, mwisho aka disconnect kabisa....sasa ivi anasikilizia kwenye bomba tu....
 
Mbona ni rahisi tu kamusi,

Tatizo kubwa ni kuwa wanaume wengi huwa tunachukulia mambo kirahisi rahisi na wakati mwingine kujichukulia kwamba sisi ni wajanja sana kuliko wanawake. Kumbe wanawake ni wajanja 100x kuliko sisi!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Basi sawa, sasa napenda uniheshimu, unipende ukae nyumbani UA langu la nyumbani, sio kutangatanga na kutaniana na watu maofisini. Hapo sitakuwa na neno. Mpenzi wangu tulia nyumbani nikutunze kama nilivyoahidi!

Kumbe tatizo ni taniana na watu ofisini!Nikikaa nyumbani nitakuwa nafikiria kizee bwana,nivumilie tu mwenzio niwe naenda kazini basi.!
 
Sawa nenda kazini mpenzi wangu , mke wangu mpendwa, lakini proceeds from that kazi should come to the same kapu for family benefit! Nami proceeds from kazi yangu nitaweka kwenye kapu moja. La sivyo ukae nyumbani unipikie, nisile vyakula vilivyopikwa na msichana wa kazi.
 
Hapo father house ndiyo tunapotofautiana.Mshahara wangu ni wa saloon na kwakuwa mwenyewe unaona nimeweka kucha ndefu,nitaishije bila ya msichana wa kazi?Your understanding please!
 
Mishahara yenu! Basi mrudi kwenu mkale mishahara yenu!

Kwani ulipomuoa mkeo ilikuwa ni kwa lengo la kula mshahara wake? Simama kwenye nafasi yako kama mume. Kumbuka "Mume atalima na kutafuta chakula cha familia yake kwa tabu. Mke atazaa kwa uchungu" Weraaaaaaaaaaaaa
 
Basi ukae uzae, sasa mambo ya kazi tena yanatoka wapi. Kaa unizalie watoto, nami nitafute chakula na matunzo yote.
 
Sawa nitakaa na kuzaa. Najua utatafuta chakula. Najaribu kukusaidia kupata pesa ya kununulia mahitaji yangu madogo madogo kama pamba, wanja, gari ya kuendea clinic, bangili na vitu vinavyofanana na hivyo. Sasa usizitolee macho pesa zangu za mshahara!
 
Hapo father house ndiyo tunapotofautiana.Mshahara wangu ni wa saloon na kwakuwa mwenyewe unaona nimeweka kucha ndefu,nitaishije bila ya msichana wa kazi?Your understanding please!

Hapo understanding itanipiga chenga. Mwanamme conservative mimi! Kucha ndefu sawa, leta mshahara wako tu-budget vyote hiyo kwa kipato cha pamoja!
 
Sawa nitakaa na kuzaa. Najua utatafuta chakula. Najaribu kukusaidia kupata pesa ya kununulia mahitaji yangu madogo madogo kama pamba, wanja, gari ya kuendea clinic, bangili na vitu vinavyofanana na hivyo. Sasa usizitolee macho pesa zangu za mshahara!

Sasa jamani mwili mmoja unawezaje kuwa na mishahara miwili? Si mwili mmoja macho mawili, sasa nazitolea macho ya kutoka wapi. Ina maana mwili huu una macho manne!
 
Back
Top Bottom