MM Nashukuru sana kwa kuleta hii hoja kwenye uwanja wa majadiliano. Mimi ni daktari na kutokana na huo mshaara ushuzi ulioonyeshwa hapo juu nimejiamulia kubwaga manyanga nafanya vitu vingine kabisa. kwa nini nipate dhambi za bure? Kama unashindwa kutimiza wajibu wako hiyo ni dhambi na mimi sikuwa tayari kufanya hivyo.
Kuna neno uzalendo limeimbwa hapo juu but sijui huyo mdau anaanisha uzalendo gani? Kama keki ya taifa ni yetu tugawane wote. Wewe huwezi kusema mbunge wa darasa la nne posho kwa siku laki moja kwa vile maisha magumu halafu daktari unampa laki sita na nusu kwa siku 30! Jamani tumuogope Mungu. Hana vikao, hana posho, hana mafuta hata gloves za kupiga PR na PV hamna pia, mazingira ya kazi magumu, vitendea kazi hamna yeye ni nani haswa hadi akae hapo...
Hawa viongozi wetu wataendelea kufa vifo vya mende. Wanaweza kwenda India kwa Check up na elective procedures lakini akipata heart attack au emergency nyingine hawezi fika hata airport kutoka Kimara achilia mbali India! Kama hakutakuwa na mwamko wa kuimarisha huduma za afya hali itaendelea kuwa mbaya. Wadanganyika nawasikitikia sana.
Kinachotokea sasa kutokana na utandawazi na fursa mbali mbali vijana madaktari wazuri wanaacha kutibu na kufanya mambo mengine yenye kipato. Mnachotakiwa kujua ni kuwa madaktari wengi ni watu wernye akili kuliko watu wa kawaida na akijitune kidogo tu anafanya kazi nyingine vizuri sana kwa hiyo wanaondoka kimya kimya.
Hesabu zinaonyesha kuna kama madaktari 2400 Tanzania lakini wanaotibu najua hawafiki 800. Wapo hapo hapo mjini wanapambana na MKUKUBI wao(Mkakati wa Kupambana na Umaskini Binafsi).
Sintosahau mwaka 2005 wakati tukiwa na mgomo kutaka mshahara uongezwe kutoka laki na nusu(150,000) kwenda milioni moja (1,000,000) Usicheke ukweli ndo huo nilikutana na afisa mwajiri wa Wizara ya afya jina lake nalihifadhi, Tukawa tunamwambia kama Wizara haiongezi hela tunaacha kutibu na kumwambia kuwa tupo adimu, akasema kuwa Nani kakwambia hata mkiondoka Watanzania watatibiwa kwa dharau ya hali ya juu. Niliinua macho juu nikamwambia Mungu niepushe na hawa vihiyo, nikaangalia mbele na sijarudi tena kudai milioni moja baada ya kusoma kwa jumla ya miaka 20! Give me a break.
Tatizo kubwa Tanzania kila mtu anayevaa koti jeupe anaitwa daktari. Hata akiwa mchinja nyama. Mtu akienda hospitali kuanzia karani, mfagiaji, nurse assistance, binzari wote wanaitwa madaktari. Serikali imetumia huu mwaya kuwakanya madaktari sana lakini kwa anayejua kitu ambacho Daktari anachoweza kufanya in relation to Medical Assistant, AMO na kada nyingine anajua namaanisha nini.
Nisijekuwachosha kusoma ila kwa mwendo huu wa serikali yetu kwa kuwa na double standards kwa wafanyakazi wake sioni mwanga. Nilishang'atuka kazi kwenu mliopo kwenye fani. Njaa na maendeleo havipikiki kwenye chungu kimoja.
Naomba kuwakilisha