Mishahara ya madaktari wetu; wanastahili nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara ya madaktari wetu; wanastahili nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 21, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwa vile wafanyakazi Benki Kuu wanastahili maisha ya juu kama ya wale wa Benki za nchi zilizoendelea na wabunge wetu nao wanastahili maisha kama ya wabunge wa nchi zilizoendelea; na kwa vile wapo watu wanaostahili katika utumishi wa umma maisha ya kimagharibi.. naomba kuuliza je madaktari wetu wanalipwa mishahara inayolingana na madaktari kama wa nchi za US na UK?

  Je itakuwa vibaya kama na wao wakiamua kudai "mastahili" yao kutoka kwa watawala?

  au hawastahili nyumba nzuri zenye mabwawa nje na magari na posho kubwa zaidi? Labda niulize tu kwa wastani daktari wa Tanzania analipwa kiasi gani na kiasi kinalinganishwa vipi na daktari wa US.
   
 2. m

  msabato masalia Senior Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa Hivi watakuja na kusema wewe mchochezi. Serikali haina priorities.Ma-klassmate wangu walimalinza interniship mwaka jana hapo Mbeya Referal hospital,wakapata ajira hapo hapo,two months later wakaacha kazi,shida,wamechoka kuandamana kudai mishahara. Hadi "wapachimbe" ndo kieleweke.
  Inasikitisha.Ubinasfi,kushibisha matumbo ndo vitu vinavyowamaliza watanzania.Angalia mshahara wa Dr. pale Rwanda.What goes around comes around, wanakwiba ili wajenge,wakatibiwe nje. It is a failed social security system. Vitambi, Diabetes, Hypertension, Hyperlipidemia, Sedentary life, Nyumba ndogo...........list goes on vitawamaliza. Even how much you steal,you will end up in cheap hospitals in India not even in South Africa.Guess what,you will die at the end.:mad:
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Na wahandisi je??????????
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah inatia uchungu sana tena mno umesahau walimu waliopo vijijini shule ya nyasi nyumba ya mwalimu ya nyasi sakafu vumbi kwenda kuchukua Mshahara anatumia siku 4 sehemu zingine anatemnbea km 80 ili afike wilayani. Sijui nani atawakumbuka hawa wafanyakazi walimu na Madaktari.
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  the list will end to mention all professional ila la msingi ni moja, watu walipwe kulingana na mazingira ya nchi na hili lianzie kwa viongozi wa serikali mpaka mfagiaji ktk ofisi ya umma, ukweli uko wazi serikali haiwezi kulipa mishahara kama ulaya, kulazimisha ivyo ni kama kuiambia serikali ifanye miujiza!
  uzalendo ndio kitu cha muhimu kuliko vyote! we need to change people mentality especially hawa viongozi wetu wanaoishi maisha ya kuigiza!
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Sijui kwa wengine ikoje...lakini maisha ni magumu kinoma, sometimes huwa nafikiria nikijiuliza mtumishi wa umma au Serikali analipwa shilingi laki moja labda kwa mwezi, anaishi vipi hapa mjini akiwa na familia ya mke na watoto wawili na kwenye nyumba ya kupanga?

  Kuna jamaa yangu mmoja mfanyakazi wa ngazi ya kati katika kampuni fulani, alibakiwa na shilingi laki tatu ya matumizi wiki moja kabla ya tarehe ya mshahara...alihisi dunia imemuelemea, alikuwa mnyonge ile mbaya. Sasa hao wa laki moja kwa mwezi inakuwaje?

  Serikali ya Tanzania, inashindwa kulipa watumishi wake wengi mishahara itakayowategemeza kwa kisingizio cha Umaskini, but kuna 'Special Ones' humo humo serikalini na idara zake, wanalipwa pesa za kufuru. Sijui hela hizi wanazitoa wapi?
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unajua tanzania kwa sasa hakuna tunachokijali zaidi ya siasa na UANASIASA!kwasababu huko ndiko kuna ''mianya ya fedha''!

  TAALUMA KAMA UALIMU na UDAKTARI hazithaminiwi kabisa...!
   
 8. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh !! Mkuu sikupenda kuchangia mada hii leo lakini hapo kwenye nyekundu umepiga kiuhakika sana..Ni wachache wenye kupona mkuu.. Na huanza hivi hivi mara kaanguka mara kizunguzungu mara sijui uchovu wa safari...By the End utasikia habari yake !!!!!
   
 9. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hapa sina la kuongeza, maana ujumbe wako ni mfupi lakini umejitosheleza kila kona.

  Pengine niongeze kidogo tu kuwa badala ya kufikiria kuwa madaktari wetu walipwe kama wale wa Ulaya na US, kwanza tujiulize kipato cha mmarekani(income per capita)kwa mwaka ni kiasi gani na cha mtanzania ni ngapi. Vile vile waweza kujiuliza kuwa viwanda nchini Marekani vinaingiza asilimia ngapi ya GDP ya nchi, na ugeuke kwa Tanzania katika swali hilo hilo. Maswali kama hayo yanaweza kujaza ukurasa, na na na.

  Tuepuke propaganda katika maswala muhimu kama haya. Kama tuko makini tujilinganishe na nchi za ulimwengu wa tatu, hususan zile zinazofanya vizuri katika maeneo hayo katika Afrika.

  Tusitegemee kuwa Mungu atateremsha Madola $ toka mbinguni. Tusiishi kwa miujiza.
   
 10. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Je mwajua mshahara wa daktari akimaliza internship? Ni shs 650,000/- kwa mwezi sasa fanya hesabu zile bil 1.5 zilizotumika kujenga nyumba ya gavana zingeweza kuwaongezea mara mbili madaktari wetu 2,308 mshahara wao na kuwa 1,300,000/- na hata kwa kiwango hicho bado hakijafika nusu ya mshahara anaolipwa daktari Rwanda US$ 2400.......Hadithi ni hiyo hiyo kwa wahandisi, walimu n.k
  Na wala serikali haina haja ya kupandisha kodi kuongeza mapato NI FAIR distribution...punguza posho na mishahara ya mawaziri, wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi.......tutaweza lipana mishahara sawia!
   
 11. T

  TheUchungu Member

  #11
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni tatizo kubwa sana, madaktari,walimu na watumishi wengi wa umma...mpaka mapolisi wanalipwa kidogo sana, ndio maana hata rushwa haitisha maana wanataka kujikimu, na hili pia linashusha ufanisi katika taaluma zao sana....
   
 12. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  mie sioni niseme nini tena katika hili...ila ni busara kila mtu awe mwizi wa mali ya umma., ale rushwa kadri ya uwezo wake....watokee warloads wakamate himaya zao watu wakipita wawalipe road tolls na kila aina ya uchavu hata tufikie level ya somalia....nitafurahi sanaaaaa...we millions got nothin to lose...nchi ikiwa haikaliki ndipo kila mtu atatia akili kichwani na kumheshimu kila tom,harry and dickens aliyemzunguka
   
 13. N

  Nanu JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yaani, vipaumbele vya serikali yetu ndiyo tatizo. We need reformation!!!!!!!!!!!!!
   
 14. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,787
  Likes Received: 20,729
  Trophy Points: 280
  madaktari wetu hawalipwi kama madaktari wa uk/usa kwasababu hata serikali yetu haina kipato kama uk/usa

  daktari wetu anapata tsh 650,000 kianzia na UK anapata £50,000 kwa mwaka kianzio apprx. £4000/month

  governor wetu anapata $180,000 kwa mwaka,governor wa UK anapata £300,000=$450,000(appx fig)

  angalia hata kwa wenzetu daktari anapata £50,000(junior dr) while governor anapata £300,000

  polisi,walimu na manesi wanapata(kianzio) £18,000,kwahio unaweza kuona sio tz tu ni dunia nzima mtumishi wa umma analipwa hela kidogo,wakati huyu governor wa uk anapata £300,000 kuna CEOs wa benki kama barclays,lloyds,rbs,hbsc wanapata up to £7 million per year more than ten times ya huyu governor

  ni muhimu tujiulize kwanza utendaji wetu kabla ya kutaka mishahara kama ya mtu/taasisi/nchi fulani

  serikali inalipa kulingana na uwezo wake,hata mbunge/waziri wa tz hapati hela nyingi kama waziri/mbunge wa uk na daktari(wa kawaida serikalini) halipwi mshahara sawa na waziri wa uk,labda wa usa watupe salary zao
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tungelijua jinsi demand ya watu hawa ilivyojuu ulimwengu mzima tungelianza kuweka mikakati wasitukimbie kwenda nje. Kuna kipindi hapa wanasiasa waliwafukuza madaktari wote eti wakawapata wengine jeshini na maeneo mengine.
  Sijawahi kuona.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hizi takwimu umezipika ama mmbebabox ?

  Hakuna ukweli eti bila aibu
  Fanya tafiti kabla ya kuweka yasiyo na ukweli
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hili ya madaktari na wauguzi limeshagazungumziwa sana huko nyuma na migomo wameshaitisha lakini wapi. La muhimu hapa ni kuondoa madarakani serikali ya CCM na kujaribu serikali inayoongozwa na chama kingine. CCM wameshalewa madaraka kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu waamini kuwa hakuna mwingine zaidi ya CCM anayeweza kutawala na kuongoza. Kuitoa CCM madarakani itakuwa mwanzo mzuri. Bakisha CCM endeleza status quo na endelea kulalamika.
   
 18. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #18
  Jan 21, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mshahara wa daktari intern ni 450,000,na kwa anayeanza kazi kama registrar mshahara una anza na TGS G,ambayo ni kama 550,000,bila makato.kodi ambayo daktari wa tGs G analipwa mshahra wa 720,000, na baada ya makato ya kodi inakuja kwenye 580,000 net.yaani kodi tunayolipa ni kubwa zaidi ya mfanya biashara kila mwaka.na ile tume ambayo ilundwa na mh mkapa ilpendekeza serikali ina uwezo wa kumlipa daktari 1.2 milion bila wasi wasi wowote.sijui hizi commision ambazo ziliundwa zilikuwa za ku peana hela tu,kwa sababu hakuna pendekezo lililofanyiwa kazi.kwa kweli daktari ana hali ngumu,kila kukicha the life is in danger due to serious infections encountered everyday esp in government hospitals.god bless tz doctors.otherwise they will all one day leave this country for greener pastures.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Bila wafanyakazi kuamka na kugoma watawala wataendelea kutawala with impunity. Wafanyakazi wa TZ ndio pekee wataweza kuwalazimisha watawala kwa kupitia migomo kuijangalia na kufanya masahihiyo yanayotakiwa. Hii ndiyo historia ya mabadiliko duniani.
   
 20. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimekugongea senksi kule !!
   
Loading...