Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,243
- 44,524
- Thread starter
- #21
Nimekugongea senksi kule !!
Na wao wagome!!!
Nimekugongea senksi kule !!
Hizi takwimu umezipika ama mmbebabox ?
Hakuna ukweli eti bila aibu
Fanya tafiti kabla ya kuweka yasiyo na ukweli
Je mwajua mshahara wa daktari akimaliza internship? Ni shs 650,000/- kwa mwezi sasa fanya hesabu zile bil 1.5 zilizotumika kujenga nyumba ya gavana zingeweza kuwaongezea mara mbili madaktari wetu 2,308 mshahara wao na kuwa 1,300,000/- na hata kwa kiwango hicho bado hakijafika nusu ya mshahara anaolipwa daktari Rwanda US$ 2400.......Hadithi ni hiyo hiyo kwa wahandisi, walimu n.k
Na wala serikali haina haja ya kupandisha kodi kuongeza mapato NI FAIR distribution...punguza posho na mishahara ya mawaziri, wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi.......tutaweza lipana mishahara sawia!
Hizi takwimu umezipika ama mmbebabox ?
Hakuna ukweli eti bila aibu
Fanya tafiti kabla ya kuweka yasiyo na ukweli
mshahara wa daktari intern ni 450,000,na kwa anayeanza kazi kama registrar mshahara una anza na TGS G,ambayo ni kama 550,000,bila makato.kodi ambayo daktari wa tGs G analipwa mshahra wa 720,000, na baada ya makato ya kodi inakuja kwenye 580,000 net.yaani kodi tunayolipa ni kubwa zaidi ya mfanya biashara kila mwaka.na ile tume ambayo ilundwa na mh mkapa ilpendekeza serikali ina uwezo wa kumlipa daktari 1.2 milion bila wasi wasi wowote.sijui hizi commision ambazo ziliundwa zilikuwa za ku peana hela tu,kwa sababu hakuna pendekezo lililofanyiwa kazi.kwa kweli daktari ana hali ngumu,kila kukicha the life is in danger due to serious infections encountered everyday esp in government hospitals.god bless tz doctors.otherwise they will all one day leave this country for greener pastures.
Tatizo ni kwamba Tanzania hatuna scales, natural or artificial, zilizo equitable au reasonable. Hatuna scales, hatuna uchumi rasmi unaoeleweka, hatuna bajeti, hatuna watchdogs, hatuna pressure groups, hatuna civil society, hatuna wa kusema mbunge na gavana si muhimu zaidi ya daktari (zaidi ya sauti chache za hapa na magazeti machache sana).
Hatuna, hatuna hata sensa ya kujua tuna wafanyakazi wangapi wa serikali na wangapi ni madaktari, walimu etc.
Hatuna.
Nikaogopa kwamba tusije kukosa hata mtu wa kusema hatuna, nikasema hatuna.
Kwani mishahara ya madaktari kwenye hospitali na kliniki binafsi ni kiasi gani? Maana hapa tunazungumzia wanao fanya kazi kwenye hospitali za serikali....
Yaleyale tu mkuu km kuna tofauti basi elfu 50.....
Kiranga kuna hotuba moja ambayo Nyerere aliitoa in 1970s ambapo alilazimisha kupunguzwa mishahara ya watumishi wote wa serikali. Hotuba ile imepigwa marufuku (in effect) na kizazi cha Watanzania wengi hawajawahi kusikia kuwa imewahi kutolewa!
Kwa sababu kila kitu sisi tunalaumu serikali tu. Kwani serikali inapanga hata mishahara ya sekta binafsi?
Kwa nini madaktari wengi wasianzishe practice zao wenyewe....kwa nini makanisa yasianzishe hospitali zao yenyewe. Mimi majuu sijawahi kwenda hospitali ya serikali. Kwanza sijui hata kama kuna hospitali za serikali....
Yes sir! Inapanga kima cha chini hadi cha mfanyakazi wako wa nyumbani! Just like in the US.. the federal govt inapanga kima cha chini ya kitaifa, na majimbo yana uhuru wa kupanga kima chao cha chini as long as hakiwi chini ya kile cha kitaifa.
........Mishahara ni maumivu hapa bongo kwa wafanyakazi wa public sector, wanaofaidi ni wakubwa wa nchi na watu wanaofanya kazi kwenye NGO na private sector.
Inasikitisha nchini kwetu eti kima cha chini cha mshahara ni laki moja, hii kweli itamfikisha wapi mtu mwenye family!!