Mishahara ya madaktari wetu; wanastahili nini?

sasa wewe hujiulizi nini chanzo cha hizo lugha mbaya?ni frustrations za kuwa na maisha maduni.kama tungekuwa na system nzuri in place,tungelipwa vizuri,na kuwa na monitoring system ya maadili ya wafanyakazi hilo lisingetokea.mbona na wabunge na mawaziri pia wana lugha chafu sometimes?mfano hiyo kesi ya mlinzi wa ult sec.na siyo wote wana lugha chafu,usi generalize.
 
Hivi unajua Waziri Mkuu wa Tanzania akistaafu au akiondoka (hata kwa kujiuzulu kwa kashfa kama Lowassa) analipwa pensheni (hata kama amekaa siku moja ofisini?). Unajua hesabu ya pensheni yake hupimwaje? Ukiangalia utaona kuwa mishahara ya Watanzania imeshaboreshwa... tatizo ni kuwa Watanzania hao ni wanasiasa na watawala wanaotokana nao!

Yes; Waziri mkuu aliyestaafu bila kujali lini alistaafu, analipwa pension kwa scale ya yule aliyepo madarakani kwa muda ule. That is normal all over the world. Hapa tunaongelea majority ya watu na si ofisi moja au institution moja kama ya waziri mkuu. Huwezi ukaelezea maendeleo na maisha bora ya Marekani kwa kuangalia Bill Gates anapata kiasi gani na ukafananisha na wamarekani wote! Kuna maskini, wanakufa kwa baridi mitaani kule. Mambo ya waziri mkuu wa Tanzania achana nayo, kwani kwa namna yoyote nchi itakavyokuwa, leo au 1000 years to come, bado yeye atakuwa juu tu.

Bado turudi kwenye point. Madaktari ni sawa kabisa kabisa na mwalimu wa shule ya msingi aliyeko Kamsamba ndani huko ambako labda fuso inapita once a week. Afterall ndiye aliyemfanya akawa daktari. Kwa hiyo hakuna aliye bora kuliko mwenzake na kwa hiyo hap tuongele kuhusu modest life kwa kila mtanzania. Je wewe mzee mwanakijiji ume-play part yako kuifanya nchi iweze kuzalisha na kupata enough income kuweza kuwalipa watu wake modestly?

Tusitwange mdomo tu, kama tulivyozoea hapa Tanzania.
 
madaktari wetu hawalipwi kama madaktari wa uk/usa kwasababu hata serikali yetu haina kipato kama uk/usa

daktari wetu anapata tsh 650,000 kianzia na UK anapata £50,000 kwa mwaka kianzio apprx. £4000/month

governor wetu anapata $180,000 kwa mwaka,governor wa UK anapata £300,000=$450,000(appx fig)

angalia hata kwa wenzetu daktari anapata £50,000(junior dr) while governor anapata £300,000

polisi,walimu na manesi wanapata(kianzio) £18,000,kwahio unaweza kuona sio tz tu ni dunia nzima mtumishi wa umma analipwa hela kidogo,wakati huyu governor wa uk anapata £300,000 kuna CEOs wa benki kama barclays,lloyds,rbs,hbsc wanapata up to £7 million per year more than ten times ya huyu governor

ni muhimu tujiulize kwanza utendaji wetu kabla ya kutaka mishahara kama ya mtu/taasisi/nchi fulani

serikali inalipa kulingana na uwezo wake,hata mbunge/waziri wa tz hapati hela nyingi kama waziri/mbunge wa uk na daktari(wa kawaida serikalini) halipwi mshahara sawa na waziri wa uk,labda wa usa watupe salary zao

Hebu angalia maneno yako niliyoyatia rangi nyekundu. Baada ya hapo;
Sifa ya mtu kuwa mbunge ni -Kujua kusoma na kuandika.
Kipato cha mbunge - ~TShs 7 million/mwezi.
Matibabu bure
hakatwi kodi

Hapo unaweza ukasema hiyo inalingana na utendaji wao? Unategemea output gani toka kwa mtu ambaye anajua kusoma na kuandika tu!

Bajeti yetu inataja rasmi kila mwaka 2% ni mambo ya siasa. Siyo huduma za jamii!

Huyu spika anayeonekana kama eti anapinga mafisadi, alisema wazi kwamba lazima wabunge waishi kwa raha (IQ=0)
 
kwa sisi ambao bado vijana na tumejionea hayo yote yakitokea na yakiendelea kutokea Tz naona umefika wakati wa kila mtu kutumia mbongo yake, maana huu wimbo haujaanza leo na cha ajabu unaimbwa bila wahusika kupata ujumbe au wanaupata ujumbe bali wanapuuza. Kama unapata chance ya kupiga mzigo nje ya nchi we songa mbele, zipo nchi kibao zinataka madaktari na zinatoa huduma nzuri, haya mambo ya kupiga kelele uzalendo na wakati unateseka au unaingia kwenye vishawishi vya kutenda dhambi kwa kupokea rushwa au kufanya mambo kinyume na sheria mf kujihusisha na kutoa mimba hayana maana. Umefika wakati ambao mtu mwenye taaluma yako hautakiwi kuumiza kichwa sana, ya nini kusoma miaka kibao then unasumbuka namna hiyo, dunia sasa hv ni kama kijiji kimoja unaweza kufanya kazi popote pale wanapokuhitaji, hata kama utatakiwa kuukana utanzania we ukane tu hamna neno kuliko kuumia moyoni huku unamuona anayekunyonya huyo anapita barabarani.....
 
Kwani na wao ni "The best trained people and individuals with highest intergrity in the society" kama wale wa BOT?

Kama sio hawastahili zaidi ya wanachopata

Mtu mzima mmoja alipata kuniambia kuwa vitu vyote muhimu duniani havina thamani. Drogba na wenzake walipokuwa hapa walifanyiwa dhifa ya kitaifa na mkuu wa nchi pale golden tulip. Haitatokea hali kama hiyo ikiwa atakuja kutembelea Tanzania daktari bingwa wa magonjwa ya moyo toka India au Ufaransa

Hapo umenena! umenena! Ktk nchi yoyote, Central Bank tunailinganisha na Central Nerve motor. Hapo lazima kuwa na the best in the profession.

Hapo TZ BOT ni kichaka cha uchafu. Walio wengi ni Rubbish.

Kumbuka kesi ya wakurugenzi inayoendelea, inahusu kuchapisha noti za ziada. Mmoja katika hao wakurugenzi, Simon Jengo ni division Zero (0) ya form six then akaanza kusoma kwa 'mission town' ghafla tunamsikia ni mkurugenzi!

Hao ndo tunawasikia wakilipwa handsomely.
 
kwa sisi ambao bado vijana na tumejionea hayo yote yakitokea na yakiendelea kutokea Tz naona umefika wakati wa kila mtu kutumia mbongo yake, maana huu wimbo haujaanza leo na cha ajabu unaimbwa bila wahusika kupata ujumbe au wanaupata ujumbe bali wanapuuza. Kama unapata chance ya kupiga mzigo nje ya nchi we songa mbele, zipo nchi kibao zinataka madaktari na zinatoa huduma nzuri, haya mambo ya kupiga kelele uzalendo na wakati unateseka au unaingia kwenye vishawishi vya kutenda dhambi kwa kupokea rushwa au kufanya mambo kinyume na sheria mf kujihusisha na kutoa mimba hayana maana. Umefika wakati ambao mtu mwenye taaluma yako hautakiwi kuumiza kichwa sana, ya nini kusoma miaka kibao then unasumbuka namna hiyo, dunia sasa hv ni kama kijiji kimoja unaweza kufanya kazi popote pale wanapokuhitaji, hata kama utatakiwa kuukana utanzania we ukane tu hamna neno kuliko kuumia moyoni huku unamuona anayekunyonya huyo anapita barabarani.....
PingPong....Hii imetulia.
Maadam napenda kuishi Africa na nimesoma hapo juu kuwa Rwanda kwa Kagame MD alipwa us$2400,naamini specialist atakuwa anadondoka na mshiko mnene tu.But,wait a minute......Banyamulenge waliisha kabisa kule,,maana hii maneno ya hawa jamaa mwanawane ...haifai kabisa kuisogolea....
 
Dah inatia uchungu sana tena mno umesahau walimu waliopo vijijini shule ya nyasi nyumba ya mwalimu ya nyasi sakafu vumbi kwenda kuchukua Mshahara anatumia siku 4 sehemu zingine anatemnbea km 80 ili afike wilayani. Sijui nani atawakumbuka hawa wafanyakazi walimu na Madaktari.
Na hao mapolisi wetu maisha wanaoishi ni balaa tupu,ndiyo maana polisi,madaktari na walimu hawajitumi vema waishia kuomba RUSHWA.
 
Yes; Waziri mkuu aliyestaafu bila kujali lini alistaafu, analipwa pension kwa scale ya yule aliyepo madarakani kwa muda ule. That is normal all over the world.

Ungesema ni asilimia ngapi ya yule aliyeko madarakani sasa; na kwa vile umelinganisha na nchi "nyingine", je tunapima pensheni za watu wa chini kama wanavyofanya nchi nyingine au za wale wa juu tu?
Hapa tunaongelea majority ya watu na si ofisi moja au institution moja kama ya waziri mkuu. Huwezi ukaelezea maendeleo na maisha bora ya Marekani kwa kuangalia Bill Gates anapata kiasi gani na ukafananisha na wamarekani wote! Kuna maskini, wanakufa kwa baridi mitaani kule. Mambo ya waziri mkuu wa Tanzania achana nayo, kwani kwa namna yoyote nchi itakavyokuwa, leo au 1000 years to come, bado yeye atakuwa juu tu.

Well... that is exactly the point.. kwanini na hawa wengine nao tusiwanyanyue juu! au walio juu kuwashusha chini?

Bado turudi kwenye point. Madaktari ni sawa kabisa kabisa na mwalimu wa shule ya msingi aliyeko Kamsamba ndani huko ambako labda fuso inapita once a week. Afterall ndiye aliyemfanya akawa daktari. Kwa hiyo hakuna aliye bora kuliko mwenzake na kwa hiyo hap tuongele kuhusu modest life kwa kila mtanzania. Je wewe mzee mwanakijiji ume-play part yako kuifanya nchi iweze kuzalisha na kupata enough income kuweza kuwalipa watu wake modestly?

Of course.. unafikiri kwanini tunapigana na ufisadi na kuwakatalia wakubwa kula kama mchwa? Halafu hii hoja ya kulinganisha "madaktari" na "walimu" ni hoja isiyo na msingi; ni hoja isiyo ya kiakili. Huwezi kumlinganisha Daktari na mwalimu wa shule ya msingi na kama haya ndio mawazo basi tuna kazi kubwa zaidi!
 
Hizi posts zinanilegeza kabisa nguvu...ila anyway,itabidi nirudi kwanza Tz nikajionee,nikiona uzushi ni huu huu...dah faster sana natimka.
Ila sipendi hii weather ya huku...maanake winter basi ni barafu...wewe na penguin hamchekani,,summer 36 centigrade....food classification:eek:rganic n non organic,,organic res'ts haziingiliki.Nina miss sana natural Ugali wa dona na vegs + kuku wa kienyeji......pia figure za kibantu mwanawane,za Kondoa zile,Tanga,Pare.WaArusha..Chagga...hehe Pemba...acha bwana,hizi za huku zinanizingua tu
Lakini pouwa tu,,tutaingia kwa Muzee Wa Msituni Kagame..au Botswana.
 
madaktari wetu hawalipwi kama madaktari wa uk/usa kwasababu hata serikali yetu haina kipato kama uk/usa

daktari wetu anapata tsh 650,000 kianzia na UK anapata £50,000 kwa mwaka kianzio apprx. £4000/month

governor wetu anapata $180,000 kwa mwaka,governor wa UK anapata £300,000=$450,000(appx fig)

angalia hata kwa wenzetu daktari anapata £50,000(junior dr) while governor anapata £300,000

polisi,walimu na manesi wanapata(kianzio) £18,000,kwahio unaweza kuona sio tz tu ni dunia nzima mtumishi wa umma analipwa hela kidogo,wakati huyu governor wa uk anapata £300,000 kuna CEOs wa benki kama barclays,lloyds,rbs,hbsc wanapata up to £7 million per year more than ten times ya huyu governor

ni muhimu tujiulize kwanza utendaji wetu kabla ya kutaka mishahara kama ya mtu/taasisi/nchi fulani

serikali inalipa kulingana na uwezo wake,hata mbunge/waziri wa tz hapati hela nyingi kama waziri/mbunge wa uk na daktari(wa kawaida serikalini) halipwi mshahara sawa na waziri wa uk,labda wa usa watupe salary zao

Hata ukilinganisha na governor was UK bado tanzania madaktari wanalipwa hela ndogo mno. Ukipiga hesab kutumia namba zako, daaktari UK analipwa poundi 50,000 na governor wa UK analipwa kianzio cha pound 300,000. Kwa hiyo mshahara wa governor ni 6X ya mshahara wa UK doctor, unanipata?
Sasa turudi bongo, mshahara wa dactari wa kuanzia ni kama $ 450/mo au $5400 kwa mwaka. Na governor wa TZ anakama $180,000 kwa mwaka. Kwa hiyo mshahara wa governor wa TZ ni 33X ya mshahara wa daktari. Income inequality kama hii ni kubwa mno. Madaktari ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yeyote ile, they should be paid accordingly!!
 
Polisi wetu je? Nilikuwa na ndugu yangu pale Kilwa Road, kuna siku nilikwenda kumsalimia nilikoma kubanmwa haja... Choo ambacho kimo ndani ya madarasa (wanayoita nyumba) kilikuwa na funza wanazagaa kila mahali. Hapo hujaongelea sehemu wanayolala, wamefanya partion ya ceiling boards, sasa ukute jirani yako ameopoa kicheche huwezi kulala!

Cha ajabu kabisa hawa ndio wanatumiwa kuzima madai ya wananchi wenzao kudai haki kutoka kwa watawala...
 
Ndio maana madaktari wengi wanakimbilia kwenye siasa, takwimu za mwaka juzi zinasema kuna upungufu wa madaktari 33,000.

Naomba Mungu isije kutokea wanasiasa wakafanya kama waliyoyafanya kwenye elimu wakatuletea madaktari wa "voda fasta"

Nina imani yangu kipato cha madaktari na wauguzi kikiimarishwa kitapunguza rushwa kwenye eneo hili muhimu la utabibu. Sote tunakumbuka kilichomfika Hawa ngulume pale Muhimbili. Mimi mwenyewe binafsi nina ndugu yangu alipata ajali ya pikipiki Korogwe Tanga amekuwa akisumbuliwa sana nashukuru kwa kuwa nimewahi kufanya kazi kwenye Industry ya utabibu na kujuana na baadhi ya watumishi wa umma wa afya niliweza kusaidiwa japo kwa kiwango kidogo. Nikajiuliza ikiwa mtu unatumia influence pia huduma ina kuwa ya kusuasua watu wanataka chcochote mkono mtupu haurambwi. Yule mgonjwa alitakiwa kuwekewa waya wa meno ili ku align taya zake alipigwa nenda rudi za maana na hatimae siku walioamua wakamfanyia. Alihitajika afanye CT Scan baada ya kurudi fahamu zake vizuri na kuruhusiwa kwenda nyumbani alipewa tarehe ya mwezi desemba taree za mwisho alipoenda wakamwambia hakuna huma watu wameenda sikukuu akapangiwa January. January akaenda wakampangia mwezi huu kwenye tarehe za mwishoni mwa february sijui mara hii watamfanyia au watampiga kalenda mpaka March. Tuombe Mungu ila hali kwenye sekta ya afya hususan hizi za serikali hali ni mbaya sana.

http://www.reliefweb.int/rw/fullmaps_af.nsf/luFullMap/C977583C1A70AA4DC12573D10038F42D/$File/who_HLT_tza080114_c.pdf?OpenElement

moz-screenshot-11.png
 
Back
Top Bottom