Miriam Ndayishimie: Nilianza kunuka kutokana na vidonda vya majeraha ya kupigwa na muajiri wangu

Messenger RNA

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,103
3,023
Na Dinna Gahamanyi
BBC Swahili

G

Safari ya Miriam Ndayishimie ya kuelekea Saudi Arabia ilikuwa imejaa matumaini ya kuepukana na umasikini aliouacha nyumbani.

Ilikuwa ni safari iliyojaa matumaini ya kutafuta riziki na kubadilisha maisha, lakini iligeuka kuwa dhiki na makovu yasiyoweza kufutika.

Mwezi Agosti, 2018 ndipo Miriam Ndayishimiye, mwanamke kutoka Burundi alipowasiliana na mtu fulani wa Burundi ambaye alimueleza kuwa anaweza kumkutanisha na mmiliki wa kampuni ya mawakala kutoka Kenya inayowapeleka watumishi wa nyumbani kufanya kazi katika mataifa ya Kiarabu na Mashariki ya Kati na hasa katika nchi ya Saudia Arabia.

Mpango wa kwenda Saudi Arabia uliokuwa wa siri kati yake, na mwakili wa kampuni ya mawakala ya Kenya raia wa Burundi iliiva.

Wawili hao walifanya mazungumzo ya mara kwa mara kwa njia ya simu ili kufanya maandalizi ya safari.

‘’Kwenda Saudi Arabia kwangu ilikuwa ni ndoto kuu kwani nilikuwa nimesikia habari kwamba mtu akienda Saudia analipwa mshahara mzuri, kwahiyo nilijua nikienda tu, maisha yangu yatabadilika na kuwa mazuri, hasa kutokana na kwamba nchini Burundi sikua na ajira’’, anasema Bi Miriam.

Miriam ni mmoja wa wanawake kutoka Burundi ambao wamesafirishwa kwenda katika mataifa ya Arabuni kufanya kazi hasa za nyumbani, na matarajio ya wengi wao ni kwamba kufanya kazi katika nchi za Arabuni hasa Saudia ni mwanzo wa kuondokana na dhiki ya umasikini.

g

Miriam anasema sikio lake lina kovu ambalo alilipata kutokana na kupigwa na muajiri waje wa Saudi arabia
Burundi ambayo ni mojawapo ya nchi masikini zaidi barani Afrika inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira, huku pia mfanyakazi wa kawaida wa serikali akilipwa mshahara wa chini ya dola 100.

Kwa Miriam ilikuwa ni fursa kuu ya kubadili maisha, hivyo hakuchelewa kuchukua uamuzi wa kufunga safari ya kuelekea nchini Kenya , ili kukutana na mmiliki wa kampuni ambaye angempeleka Saudia.

Alipofika Kenya Miriam alipokelewa na mwanamke ambaye alianza mchakato wa kuwasiliana na mawakala wa makampuni ya Saudi Arabia yanayowatafutia wanawake kutoka mataifa ya Afrika Mashariki kazi za nyumbani.

‘’Nilipofika Kenya nilienda kwa mwanamke tuliyekuwa tumewasiliana anitafutie kazi Saudia, [mmiliki wa kampuni ya mawakala], akanipeleka nyumbani kwake na hapo niliwakuta wanawake wengine wengi, kutaka katika mataifa ya Afrika Mashariki ,Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Kenya -sote tukaishi nyumbani kwake…kula ilikuwa ni shida, maisha yalikuwa magumu, maana yeye sasa ndio aliyekuwa anatutunza.’’

‘’Kuishi nyumbani kwa mwanamke yule kwa muda mrefu kulinifanya nifikirie sana, na kujiuliza iwapo kweli nitafika Saudia au ndio mwisho wa safari yangu ya kutafuta maisha?’’

Waswahili wanasema kila lenye mwanzo lina mwisho. Hatimaye Bi Miriam alipata muajiri nchini Saudia na kulipiwa tiketi ya ndege ya kuelekea huko.

‘’Nilifurahi sana nilipopewa tiketi yangu ya ndege ya kuelekea Saudi Arabia, nijua sasa ndoto yangu imetimia’’ anasema Bi Miriam.

Maisha Saudia Arabia​

G

Moja ya picha za majeraha ya mwili wa Miriam ambayo anasema aliyapata kutokana na kupigwa na kuteswa na muajiri wake wa kike nchini saudi Arabia

Miriam alipowasili nchini Saudi Arabia alipokelewa na kampuni ya mawakala inayowapokea wanawake kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika wanaotafuta ajira nchini humo, na mara hii hakuchelewa kupelekwa kwa mwajiri wake wa kwanza ambako alianza kazi ya kuwa mfanyakazi wa nyumbani.

‘’Mara baada ya kuwasili kwa mwajiri wangu ambaye alikuwa mwanamke Mwarabu alinipokonya pasipoti na simu, nikaambiwa nivikabidhi mara moja kwa mwajiri, hili lilinishangaza lakini nikawa mpole, nikasema ni sawa tu, ili mradi nilipwe mshahara wangu.’’

Miriam alifanya kazi vyema na mwanzoni, kwani kulingana naye kazi za nyumbani ni kazi aliyoifanya vizuri.
Hata hivyo anasema baada ya muda, alianza kuona mwajiri wake ambaye alikuwa mwanamke, akianza kumkaripia mara kwa mara.

‘’Mwajiri wangu alianza kuonyesha ukali kwangu na kufoka mara kwa mara na kunitusi bila sababu…nilijitahidi sana kukaa kimya, maana nilijihisi mwenye hofu kubwa’’, Miriam anakumbuka.

Baada ya muda wa miezi michache ya kutukanwa na kufokewa, Miriam aliamua kuondoka kwa mwajiri wake wa kwanza na kutafuta kazi ya nyumbani kwa mtu mwingine.

Mwajiri alimrejeshea paspoti yake na simu na hivyo Miriam alikua huru kuondoka kwenda kumtafuta mwajiri mwingine.

Muajiri wa pili​

Miriam alipata muajiri ambaye alimpokea, ambaye anasema alikuwa ni mwanamke wa Kiarabu.

Alipofika nyumbani mara moja alipokonywa pasipoti pamoja na simu yake: ‘’Alichukua pasipoti yangu na simu sawa na mwajiri wangu wa kwanza. Aliniambia nisijali atanirudishia baadaye na kwamba huo ndio ulikuwa utaratibu kwa wafanyakazi wote wa nyumbani nchini Saudi Arabia,’’ anakumbuka Bi Miriam.

‘’Nilikubali kumpatia simu na pasipoti, maana nilikuwa nimebadili mazingira, na nilikuwa nimejawa na matumaini kwamba nimeondokana na adha ya matusi na kufokewa mara kwa mara …Nilijua sasa walau nitaweza kupata ndoto yangu iliyonileta nchini Saudia ya kubadilisha maisha yangu’’, anasema.
Miriam alianza kufanya kazi, lakini kadri siku zilivyokwenda aligundua kuwa mambo huenda yasiwe kama alivyotarajia.

‘’Nilifanya kazi mwezi wa kwanza, sikulipwa mshahara, nikasema labda mwajiri wangu amechelewa tu kunilipa atanilipa baadaye, niliendelea kufanya kazi na kumtii mwajiri wangu. Mwezi wa pili pia sikulipwa mshahara pia, hii ikaanza kunitia wasiwasi.’’ Anakumbuka Bi Miriam.

Ulipotimia mwezi wa tatu Miriam aliamua kuzungumza na muajiri wake na kumuomba amlipe mshahara wake wa miezi mitatu, aliyomfanyia kazi, na hapo ndipo Miriam anasema masaibu yake yalipoanza.

‘’Nilipomuuliza tu mwajiri wangu kuhusu mishahara yangu , hapo ndipo hali ilipoanza kuwa ngumu... alianza kuwa mkali na mkatili zaidi kwangu, nilifokewa, na kutukanwa hovyo’’.

‘’Nililimwambia anilipe pesa yangu niondoke kwake, lakini alikataa. Nilipoendelea kusisitiza ninataka mshahara wangu, alianza kunipiga, na kuninyima chakula'' anasema na kuongeza kuwa, ''Nilipigwa mijeledi na kurushiwa vifaa vya nyumbani kama masufuria, na vikombe na masahani, kila mara nilipomuuliza muajiri wangu kuhusu mshahara’’, anasema.

‘’Nilipigwa kila siku mwili, ukaanza kutoka vidonda, nikaanza kunuka, nilifika mahali vidonda vikaanza kuoza na kunuka kama panya aliyeoza'', anasema.

Bi Miriam hakumfahamu mtu mwingine yoyote nchini Saudi Arabia na Ubalozi wa Burundi nchini Saudi Arabia haukufahamu uwepo wake Saudia, kwasababu aliingia nchini humo kwa mipango yake binafsi ya siri, kwa hiyo hakuwa na mtu yeyote wa kumuelezea masaibu yake.

‘’Nilipigwa kila siku, na nikanyimwa chakula, ikabidi nianze kwenda majalalani na mitaani kutafuta chakula kichafu…’’, anasema Miriam huku akilia, na kuongeza kuwa: ‘’Niling’ang’ana kuendelea kuishi katika nyumba ile kwasababu sikutaka kuondoka bila kulipwa pesa yangu ya mishahara ya miezi mitatu,’’anasisitiza.

Hali iliendelea kuwa ngumu kwa Bi Miriam kadri siku zilivyokwenda, anasema: ‘’Muajiri wangu alinipiga kiasi kwamba mwili wangu ulianza kutokwa vidonda hasa mgongoni kwangu, nilikuwa ninarushiwa vitu, na wakati mmoja nilipigwa na kitu cha chuma kwenye sikio langu nikaumia vibaya…damu nyingi ikaanza kutiririka kutoka kwenye sikio. Kutokana na kupigwa na kukosa chakula, tumbo langu lilianza kuvimba...nadhani ilikuwa ni utapiamlo.

''Nilianza kunuka vibaya kutokana na vidonda vya majeraha ya kupigwa na muajiri wangu’’, anasema.
Baada ya kuona kuwa harufu ya vidonda imekithiri, mwajiri wangu aliamua kunichukua na kunitupa mtaani mahali ambapo sikuwa napajua.''

''Baada ya kutupwa nilihangaika sana ...nilikuwa nikiomba chakula kwenye migahawa ,hoteli na watu mbali mbali, baadhi walinionea huruma na kunipa chakula na wengine walinifukuza na kunitukana…nilipokosa kabisa kitu cha kula nilikwenda kwenye majalala ya Waarabu na kula vyakula vichafu.
Kwenye mitaa na majalalani marafiki zangu waligeuka kuwa paka. Ulipofika usiku nilihofu sana, lakini baadaye nikazoea. Paka walinizoea na mimi nikawazoea.’’anasema.

‘Sitasahau mwanaume aliyenisaidia’​

g

Bi Miriam anasema alikuwa amezoea kula vyakula vya jalalani kutokana na kunyimwa chakula na muajiri wake
Siku moja kama kawaida Bi Miriam aliamka kutoka mtaani na kwenda kuomba chakula katika mgahawa mmoja uliokua karibu na mtaa alikokuwa amelala.

‘’Niliamka asubuhi jua lilipochomoza, nikiwa na njaa kali, nikaenda kuomba chakula kwenye mgahawa mmoja. Wateja na wafanyakazi walinifukuza kwasababu nilikuwa mchafu sana, na baadhi yao walisema ondoka! Unanuka!.’’anakumbuka.

Lakini Bi Miriam anasema kulikuwa na mwanaume mmoja miongoni mwao ambaye alimuonea huruma: ‘’Alisema acheni kumfukuza huyo mtu, hamumuonei huruma mtu kama huyu, hamuoni kuwa ana njaa. Mungu atawalaani mkimfukuza mtu kama huyu. Aliniita akaniuliza unataka nini?, nikamwambia ninataka chakula nina njaa sasa…akasema nipewe chakula ninichotaka, nilipewa chakula nikala nikashiba. Nilifikiria sana nikajiuliza, inawezekana kuna Waarabu wazuri hivi?’’, anasema.

Baada ya kula chakula, mwanaume yule aliketi na Bi Miriam na kumwambia kuwa yuko tayari kumpeleka kwake ampatie chakula na aishi na familia yake. Miriam alimwambia anachomuomba ni kumfikisha kwenye ubalozi wa nchi yake Burundi. Hata hivyo mwanaume yule alisisitiza kuwa ni vyema akae kwake kwa muda.

‘’Niliishi na familia yake vizuri sana, japokuwa nilikuwa ninanuka, hawakunitenga, walinionyesha upendo mkubwa sana, nikaanza kujihisi kuwa mtu ten… Kuna Waarabu wenye utu, lakini ninasema ni wachache sana!. Namsukuru sana mwanaume yule.’’

‘’Nikiwa katika familia ile, siku moja nilijitazama mgongoni kwenye kioo , nikaona majeraha ya kupigwa na muajiri wangu, na baadhi ya vidonda ambavyo vilikuwa vinatiririka damu, niliangua kilio, maana sikufahamu kuwa nilikuwa na majeraha mengi mgongoni mwangu!, nikamuonyesha binti wa mwanaume yule ambaye pia alipiga kelele , akamuomba baba yake anipeleke hospitalini, walinipeleka hospitali nikapewa dawa.

Ingawa mwanaume yule na familia yake wamuonyesha upendo , Bi Miriam kusisisitiza kuwa, ninataka kwenda kwenye ubalozi wa Burundi. Hatimaye aliutafuta mwanaume yule ubalozi kwa njia ya Google, akapata mahala ulipo. ’’Alinitafutia usafiri nikaenda kwa teksi hadi kwenye ubalozi…nilihisi moyo wangu umetulia’’.

‘’Nilipofika ubalozini nilijitambulisha kuwa mimi ni Mrundi, nilipokelewa vyema, nikawaeleza maafisa wa ubalozi masaibu niliyopitia nchini Saudia, walinisikiliza na ubalozi ulinisaidia kupata matibabu, nikaanza kuhisi vyema kimwili na kisaikolojia kwa muda wa miezi takriban sita, niliambiwa sasa umepona na unaweza kurejea nyumbani Burundi, na hivyo ndivyo nilivyorejea nyumbani kutoka Saudi Arabia’’.

‘‘Ninaweza kusema kuwa binafsi ninaishukuru serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake nchini Saudi Arabia kwa kuniwezesha kurejea nyumbani Burundi.

Bi Miriam ni mmoja wa wanawake wengi wa Burundi na mataifa Afrika Mashariki wanaowenda katika nchi za kiarabu ikiwemo Saudi Arabia kutafuta ajira husuan na kazi za nyumbani.

Hata hivyo baadhi yao hujipata katika matatizo kama vile kutendewa ukatili pamoja na kunyimwa mishahara, na baadaye kukosa usaidizi wowote kutokana na kwamba wengi huingia Saudia kwa siri , na hivyo waajiri wao wanapowanyang’anya simu na paspoti hushindwa hata kuwasiliana na jamaa zao wanapoteswa.
Hatahivyo nchini Burundi, serikali imeanzisha mpango wa kuwasaidia wanawake wa Kirundi wanaotaka kwenda Saudi Arabia kuepuka ukatilialiofanywa Bi Miriam

g

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Burundi Bi Ines Sonia Niyubahwe anawasihi wanawake wa Burundi kuacha kwenda Saudi arabia kisiri

Akizungumza na BBC, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Burundi Bi Ines Sonia Niyubahwe anasema serikali ya Burundi pamoja na serikali ya Saudi Arabia wameweza kuunda kamati ya pamoja ya wataalamu itakayohakikisha Warundi wanaokwenda Saudi Arabia wanatendewa haki kulingana na makubaliano ya awali baina ya muajiri na muajiriwa.

‘’Tatizo ni kwamba wengi kama Bi Miriam wanaondoka nchini kwa siri na kwa njia zisizo halali, kwahivyo inakua vigumu kufuatilia maisha yao wanapoingia saudi Arabia, tunachowaomba wanawake wa Burundi wanapokwenda Saudia watufahamishe. Sasa tuna kampuni ya Global Consulting ambayo tunafanya nayo kazi ambayo itaweza kuwafuatilia siku hadi siku kwa muajiri wao na kuhakikisha hawatesi kama Bi Miriam na haki zao zinalindwa . Tutashirikiana na kampuni hii pamoja na makampuni ya Saudi Arabia yaliyowapekeka kuhakikisha wako salama’’, anasema Bi Niyubahwe.

'Siwezi kusahau ukatili nilioupitia Saudia'​

g

Bi Miriam anasema hali ngumu ya maisha na ukosefu wa ajira ni mambo yanayowasukuma wanawake wengi kutumia njia za siri kwenda Saudia kutafuta riziki, lakini anasema kwa kuwa sasa serikali ya Burundi imeweka mkakati wa ufuatiliaji wa mikataba na maisha ya Warundi wanaofanya kazi Saudia, huenda hali ikawa afueni.

Je, Miriam anaweza sasa kurejea Saudia kufanya kazi baada ya serikali yake kuweka utaratibu wa kulinda haki za raia wake wanaofanya huko? , jibu lake ni: ‘’Hapana Mwarabu ni Mwarabu tu!, atakutesa tu, ukishafika mikononi mwake utateswa tu!’’

Kwa upande mwingine anasema hawezi kumwambia kila mtu anayetaka kwenda Saudi Arabia asiende, kila mtu ana bahati yake, aende huenda akapata bahati ya ya kuajiriwa na muajiri ambaye ni mzuri.

‘’Nina makovu ya mateso niliyopata Saudia, nashukuru kwa sasa ninaendelea kupona, sitasahau kamwe ukatili niliotendewa kwasababu makovu ninayaona kila siku!... siwezi kusahau ukatili nilioupitia saudia’’, anasema Bi Miriam.

BBC Swahili
 
nimeumia lakini ukweli ni kwamba waafrika wataendelea kuwa watumwa tu kwa waarabu haitabadilika hata tujipendekeze kwa namna gani ndivyo wanavyoamini.
nafikiri la msingi ifike mahali lazima waafrika tufikirie ni kwa jinsi gani tunaweza kujikomboa na kuwakomboa wengine.
binafsi naamini bado hatujafanya kazi kwa kiasi cha kutosha ikiwa ni pamoja na kufikiri kwa upana zaidi.
huwenda wengi wetu tunatumika labda kwa 5% ya uwezo wetu hebu tujaribu kutafakari na tuondoke katika unyonge tulionao na kupunguza kujilalamisha (tulalamike lakini tusikae kwa muda mrefu).
 
Ni kweli Saudia hakafai kwa wafanyakazi wa majumbani ila hii simulizi hiajakaa sawa either mwandishi kayumba au ndio hivyo muelezeaji amezidisha chumvi.
 
Warabu wote washenzi sana na ni majoka yasiyo na huruma hata kidogo hasa kwa ngapi yetu nyeusi

Kuna wamatumbi kisa wamekuwa brainwashed na dini ya waarabu,basi wakisalimiana slamakeko,na kuvaa kanzu bhalagashia na kobazi,huwaambii kitu kuhusu hao waarabu wanawaona kama miungu wao na malaika kutoka kwa mungu wao ala.
 
Back
Top Bottom