Kuzidi kutengwa Israel sambamba na kuundwa mhimili wa Tehran-Riyadh

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Kuzidi kutengwa Israel sambamba na kuundwa mhimili wa Tehran
[https://media]

Faisal bin Farhan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa saudi Arabia alisema hivi karibuni katika mazungumzo yake na Rais Rais Ibrahim Rais wa Iran kwamba: Baadhi ya nchi duniani hazitaki kuona eneo letu linapata amani na maendeleo.

Mwanafalme huyo wa Saudia ambaye hivi karibuni alifanya safari hapa mjini Tehran alibainisha kwamba, kupanuka kwa ushirikiano hivi sasa kati ya Iran na Saudi Arabia, kutapelekea kupatikana matunda yasiyo na kikomo katika kiwango cha nchi za Kiislamu na hilo kuwa bima na dhamana dhidi ya uingiliaji wa taifa wowote kutoka nje katika masuala ya ndani ya eneo letu.

Wakati habari za kushtukiza ya kufikiwa makubaliano ya Beijing kati ya Iran na Saudi Arabia ya kufungua balozi na balozi zao ndogo ndani ya miezi miwili ilipotangazwa, Marekani na utawala wa Kizayuni zilitangaza upinzani wao dhidi ya hatua hiyo na hivi sasa ambapo makubaliano hayo yameingia katika awamu ya utekelezaji na kila siku kumekuwa kukipigwa hatua mpya katika njia ya kurejeshwa katika hali ya kawaida uhusiano wa Riyadh na Tehran hakushuhudiwi tena upinzani wa hilo, licha ya kuwa Washington inafanya bila mafanikio kuzikuribisha pamoja Saudia na utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa muktadha huo tunaweza kusema kuwa, filihali Israel imebakia kuwa mpinzani pekee wa kurejeshwa uhusiano wa kawaida baina ya Iran na Saudia.

Licha ya kuwa, maafisa wa kisiasa na vyombo vya habari vya nchi za eneo hili viliikaribisha ziara ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia nchini Iran na kuiakisi kwa njia chanya na yenye matumaini; lakini mkabala na hilo, vyombo vya habari na viongozi wa Kizayuni, wakiwa na lengo la kufunika kushindwa kwao kisiasa ikilinganishwa na zama za kutangazwa makubaliano ya Beijing ya Iran na Saudia, licha ya kuwa havikuonyesha radiamali kubwa kuhusiana na safari hii lakini hawakuweza kuficha kushindwa kwao kuhusiana na kadhia hii.

[https://media]

Kufuatia ziara ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia nchini Iran, vyombo vya habari vya Kiebrania vilieleza kwamba, kuweko muelekeo mmoja baina ya Iran na Saudi Arabia ni kikwazo katika njia ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Riyadh na Tel Aviv. Duru hizo za Kizayuni zimetangaza kuwa, mtazamo na muelekeo huu mmoja wa Riyadh na Tehran unadhuru maslahi ya Israel na upo dhidi ya jitihada za Israel za kuitenga kisiasa na kidiplomasia Iran katika eneo la Asia Magharibi na ulimwenguni kwa ujumla.

Kila mkutano unaofanyika kati ya maafisa wa Iran na Saudi Arabia au hatua nyingine yoyote inayochukuliwa katika mwelekeo wa kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, moyo wa viongozi wa Kizayuni huzidi kuumia. Licha ya mirengo ya Kizayuni na Kimarekani kuwa na hitilafu kubwa mno miongoni mwao katika masuala mbalimbali, lakini kuhusiana na mpango wa chuki dhidi ya Iran na kuandaa fursa za kuiweka mbali Iran na mataifa ya Kiarabu sambamba na kuikurubisha Israel na Saudia zinafuatilia malengo na siasa za pamoja.

[https://media]Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel

Hivi sasa na baada ya kufunguliwa ukurasa mpya katika uhusiano wa Tehran na Riyadh maadui wa Iran wanaona mipango yao imefeli na kugonga mwamba. Gazeti la New York Times limeandika, kwa miaka mingi sasa Israel imekuwa ikiitazama Iran kuwa tishio na Saudia kuwa ni mshirika na ilikuwa na matumaini kwamba, itakaribia kuanzisha uhusiano rasmi na Riyadh. Ni kwa msingi huo, ndio maana Israel ilipokea kwa mshangao mkubwa, wasiwasi na kuchanganyiwa habari ya kutangazwa kuhuishwa tena uhusiano wa kidiplomasia baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia.

Kila siku kumekuwa kukipigwa hatua moja mbele katika njia ya kuboreshwa zaidi uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudia ambapo athari na matokeo ya hilo inaweza kuwa na maslahi kwa mataifa mengine hususan ya eneo. Itakumbukwa kuwa Iran na Saudi Arabia zilikubaliana mjini Beijing China Machi 10 mwaka huu kuhuisha uhusiano kati yazo na kufungua tena balozi za nchi mbili katika kipindi cha miezi miwili.

Tayari Iran imeshafungua ubalozi wake mjini Riyadh na ubalozi mdogo mjini Jeddah na Saudia inapanga kufungua ubalozi wake mjini Tehran na ubalozi mdogo katika mji wa Mash'had baada ya sikukuu ya Eidul Adh'ha na hilo kukamilisha moja ya hatua muhimu kabisa ya kurejesha uhusiano baina ya mataifa haya mawili muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu

4bmu251f5f7b14nbwo_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom