Houth nao sasa hawashikiki. Meli zawaka moto na nyengine yazama. Saudia waachia kombora liende mpaka Eliot

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,200
10,948
Kila siku zinavyokwenda mashambulizi ya Houth dhidi ya Israel na washirika wake yanazidi kupamba moto.

Hali hiyo inaongeza mashaka juu ya uwezo na athari ya yale mashambulio ya kila mara yanayofanywa na meli za kivita za Marekani na Uiengereza.

Meli kubwa ya mizigo iliyopigwa Jumatatu inakisiwa kuwa imezama tayari.

Siku mbili baadae hapo mapema leo meli nyengine ya mizigo ambayo nayo ina uhusiano na Uiengereza imepigwa na kuwaka moto.

Uwezo wa kurusha makombora ya ballisitic wa Houth haujatetereka hata kidogo kwani kombora la leo limeweza kupenya mpaka mji wa kusini wa bandari wa Israel wa Eliot.

Israel imetangaza kuliwahi kombora hilo angani kwa mfumo wake wa ulinzi wa angani.

Siku za mwanzo za kuanza kwa mashambulizi ya Houth mfumo wa ulinzi wa anga wa Saudia uliwahi kuyatungua makombora hayo ya Houth yasielekee Israel.

Makombora ya Houth kuelekea Israel ni lazima yatambao magharibi mwa Saudi Arabia au yaruka juu yake.

Hata hivyo Katika siku za karibuni kazi ya kupambana na makombora hayo imeachiwa Israel ifanye peke yake.

Muhimu katika mabadiliko haya na ukali unaopanda wa wanamgambo wa Houth katika kuitetea Palestina ni kuwa ama meli za kivitaj baharini haziwezi kupigana kikamilifu na mbabe yeyote anayepigana kutoka ardhini.

Au meli hizo zimeishiwa na zana za kuendelea na vita na au vyenginevyo Houth ameanza kupokea misaada ya silaha kutoka mataifa mengine hasimu na Marekani mbali na misaada ya kutoka Iran.

Uwezekano wa mwisho ni kuwa nchi kama Saudi Arabia na Misri zimeanza kuunga mkono juhudi za Houth katika namna za sirij ikiwemo kutoshughulishwa na mashambulizi yao dhidi ya Israel na Marekani pindi yanapofanyika.

Houthi rebel attack sets cargo ship ablaze, forces Israel to intercept another attack near Eilat

Kwamba Houth anaweza kubadili chochote kwa mgogoro wa Palestina na Israel? Hayo makombora ambayo Houth anapiga anapiga watu gani pale Israel?
1. Raia wote wa Israel?
2. Wanajeshi wa Israel?
3. Wanasiasa wa Israel?
4. Maghara ya silaha ya Israel?
Kesho Israel akilipiza kisasi Yemen akaua raia wa Yemeni( watoto, vijana, wazee, vijana, wababa, wamama) msianze free Yemen, mara mzayuni anaua watoto na wazee, akirusha makombora kwenda Yemen hayachagui kuwa huyu ni mtoto wala mzee, silaha haina macho.
 
Hakuna ambacho Marekani hajafanya kwa Houth na bado jamaa wapo wanaendelea na shughuli zao.
Siku ya mwanzo tu Marekani na Uiengereza walipiga vituo 85
 
Wanamgambo wa Hauth wanaishi kwenye mapqngo ya mawe na majabali kwaiyo ukishambukia vituo unapoteza mda bure.

Trump na ubishi wake wote lakin aliomba poo
Ni nchi ya kihistoria kwa mapango ya milimani.Wahouth wanatumia vyema neema waliyoopewa
 
Kwamba Houth anaweza kubadili chochote kwa mgogoro wa Palestina na Israel? Hayo makombora ambayo Houth anapiga anapiga watu gani pale Israel?
1. Raia wote wa Israel?
2. Wanajeshi wa Israel?
3. Wanasiasa wa Israel?
4. Maghara ya silaha ya Israel?
Kesho Israel akilipiza kisasi Yemen akaua raia wa Yemeni( watoto, vijana, wazee, vijana, wababa, wamama) msianze free Yemen, mara mzayuni anaua watoto na wazee, akirusha makombora kwenda Yemen hayachagui kuwa huyu ni mtoto wala mzee, silaha haina macho.
Houth Wanachofanya wao ni meli zisiende Israel, Meli zisipoenda Israel zinaathiri Uchumi wa Israel na Uchumi ukiathirika na wapo Vitani ina maana wamewapunguza Nguvu.

So far Uchumi wa Israel umeshuka kwa Asilimia 19.4 kama ilivyorepotiwa na Israel

Ukumbuke Wameingia Vitani hivi karibuni kama miezi miwili tu ila effect ni kubwa hivyo, sasa Imagine same effect iendelee kwa miezi kama 6 hali itakuwaje?

Sio Wajinga Israel kuja kukomba watu Africa huku,
 
Marekani kama kweli wanataka hii mbungi na houthi basi wapeleke jeshi ardhini,,, lkn kwa kutumia ndege wataishia kupiga majabali tu jamaa hawana cha kupoteza,, ila linapokuja sasa suala la askari wa miguu marekani na washirika wake mdebwedo,, mfano halisi hapo gaza ambapo wanapambana na hamas wasiokuwa hata na kifaru kimoja, je itakuwa houthi wenye kila aina ya silaha na misaada juu
 
Niliona twitter- meli iliyoshambuliwa inazama, yaani walitoa watu wote- kitu kikaenda chini- inatisha sana, nikakumbuka TITANIC movie
 
Unaposikia Israel inalazimisha kupiga Rafah ili vita viishe au kuondosha vikosi si kwamba wamepata ushindi au wamewamaliza Hamas kama anavyodhani MK254 na wenzake lakini hali zao zimekuwa ngumu.
Wameshauona ukweli kuwa hawana safari ndefu mbele yao hasa ikizingatiwa misaada kutoka Marekani nayo imeingia kipindi kigumu na si ya kutegemea teana
 
Niliona twitter- meli iliyoshambuliwa inazama, yaani walitoa watu wote- kitu kikaenda chini- inatisha sana, nikakumbuka TITANIC movie
Walitangaza wataivuta kuipeleka Gjibout.Ni mbali sana na ilikuwa huku nyuma kwa dereva kumeshakwenda chini.
Wameamua wakae kimya tu.
 
Marekani kama kweli wanataka hii mbungi na houthi basi wapeleke jeshi ardhini,,, lkn kwa kutumia ndege wataishia kupiga majabali tu jamaa hawana cha kupoteza,, ila linapokuja sasa suala la askari wa miguu marekani na washirika wake mdebwedo,, mfano halisi hapo gaza ambapo wanapambana na hamas wasiokuwa hata na kifaru kimoja, je itakuwa houthi wenye kila aina ya silaha na misaada juu
Kuiangusha Israel na kuisambaratisha kunataka nyongeza ndogo tu ya nguvu kuongezea hizi za Houth na Hizbullah
 
Back
Top Bottom