kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
Maafisa wa kijeshi wa Iran, Saudia wajadiliana kuhusu ushirikiano
Aug 17, 2023 11:08 UTC
Maafisa wa kijeshi wa Iran na Saudi Arabia wamekutana kwa mara ya kwanza tangu mapatano yaliyofikiwa mwezi Machi baina ya pande mbili mwezi Machi mwaka huu wa 2023 kwa upatanishi wa China.
Kwa mujibu wa taarifa, kikao hicho kilifanyika kati ya Naibu Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh na Msaidizi wa Waziri wa Ulinzi wa Saudia Talal bin Abdullah al-Otaibi pembezoni mwa Mkutano wa 11 wa Moscow kuhusu Usalama wa Kimataifa.
Mkutano huo ulijumuisha makubaliano kati ya pande mbili juu ya kubadilishana waambata wa kijeshi "haraka iwezekanavyo."
Kwa mujibu wa Televisheni ya Press TV wakati wa mkutano huo, viongozi hao walitilia mkazo "azma ya pande mbili ya utekelezaji" wa makubaliano ya maridhiano.
Maafisa hao wa kijeshi wa Iran na Saudia waliyataja makubaliano ya mwezi Machi kuwa yanayolingana na maslahi ya Tehran na Riyadh na nchi nyingine za eneo na ulimwengu wa Kiislamu.
Maafisa hao wa ulinzi wa Iran na Saudia pia walisisitiza umuhimu wa jukumu ambalo linatekelezwa na vikosi vya jeshi la nchi mbili katika utekelezaji sahihi wa maelewano.
Aidha wamesema ni muhimu kwa nchi kuendeleza mazungumzo yao na kujitahidi kuelekea "kupatikana kwa ramani sahihi katika uwanja huo."
Uhusiano wa Iran na Saudia ulivurugika baada ya Saudia kuchukua hatua ya upande mmoja ya kuukata mnamo Januari 2016, baada ya waandamanaji wa Iran, waliokasirishwa na kunyongwa kwa kiongozi mashuhuri wa Shia Sheikh Nimr Baqir al-Nimr na serikali ya Saudi Arabia, kuvamia ubalozi wa Saudia jijini Tehran. Kufuatia upatanishi wa China mwezi Machi, Iran na Saudia ziliafikiana kurejesha tena uhusiano. Tayari balozi za nchi mbili zimefunguliwa Riyadh na Tehran na hii leo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian yuko ziarani nchini Saudia kuendeleza mchakato wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili.