Uhusiano wa US na Saudi Arabia unazidi kuwa mbaya sana, tutarajie nini siku za usoni?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Nyufa mpya katika uhusiano wa Saudi na Marekani

Ahmad Kazemzadeh wa gazeti la Financial Times ameandika, akinukuu vyanzo vya habari, kwamba Saudi Arabia, ambayo haikufurahishwa na masharti yaliyotolewa na Marekani kwa ajili ujenzi wa kinu cha nyuklia nchini humo, inachunguza mapendekezo ya China, Russia na Ufaransa ya kujenga kinu cha nyuklia nchini Saudia.

Mohammed bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, yuko tayari kuanzisha ushirikiano na kampuni inayomilikiwa na serikali ya China kwa ajili ya kufunga mkataba wa kujenza kinu cha nyuklia nchini Saudia iwapo mazungumzo na Marekani yatafeli.

Awali, gazeti la Wall Street Journal, liliwanukuu maafisa wa Saudi Arabia na kuripoti kwamba, Kampuni ya Kitaifa ya Nyuklia ya China inayojulikana kwa jina la "CNNC" imetoa pendekezo kwa Riyadh kujenga kinu cha nyuklia katika mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo, karibu na mpaka na Qatar na UAE.

Rais wa China na mrithi wa ufalme wa Saudia

Marekani haiko peke yake katika suala hili, kwani hata utawala wa Kizayuni, ambao umeanzisha jitihada kubwa kwa ajili ya kuanzisha uhusiano rasmi na Saudi Arabia, sasa na baada ya serikali ya Riyadh kutaja suala la kupata nguvu za nyuklia kuwa ndilo sharti la kuanzisha uhusiano na utawala huo ghasibu, kadhia hiyo imeibua hitilafu kubwa ndani ya Israel na hivyo kuzidisha mizozo ndani inayozidi kuitafuna Israel.

Tunaporejea kenye kadhia ya uhusiano wa Marekani na Saudia tunaona kuwa, ushahidi uliopo unaonyesha kwamba, uhusiano huo unazidi kudhoofika siku baada ya siku, na Saudi Arabia inatafuta washirika wapya na mbadala katika kanda ya Mashariki ya Kati na dunia. Gazeti la Telegraph limendika kuhusiana na suala hilo kwamba, sasa baada ya miaka 13, kumekuwa na mabadiliko duniani na miungano mipya inajitokeza kwa kasi. Katika dunia inaozidi kuwa na kambi nyingi, Saudi Arabia inatafuta washirika wengine wa usalama ambao hawasumbuliwi na machafuko na ukosefu wa utulivu wakati wa uchaguzi, au wasioikosoa sana Saudia kuhusu masuala ya haki za binadamu.

Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, utegemezi wa Washington kwa mafuta ya Ghuba ya Uajemi umepungua kwa kiwango kikubwa, na kwa upande mwingine, uzalishaji wa nishati ndani ya Marekani umeongezeka kwa kadiri kwamba, kwa sasa Marekani inaagiza chini ya asilimia sita ya mahitaji ya mafuta yake kutoka Saudi Arabia.

Kwa msingi huo tunaweza kusema kwamba, mlingano wa "mafuta mkabala wa usalama", ambao ulikuwa nguzo muhimu ya uhusiano wa Saudi na Marekani kwa miongo kadhaa, sasa umetoweka na haupo tena.

Mvutano katika uhusiano wa Saudi Arabia na Marekani ulishika kasi pale viongozi wa Saudia walipoamua kupunguza uzalishaji wa mafuta licha ya Ikulu ya White House kuamini kuwa, imekubaliana na Riyadh juu ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Rais Joe Biden wa Marekani na Bin Salman

Kwa upande mwingine, uhusiano mkubwa wa Riyadh na Beijing unaonyesha mabadiliko katika masoko ya nje ya mafuta. China imekuwa muagizaji mkuu wa mafuta ya Saudia mwaka 2022 kwa kununua mapipa milioni 1.75 kwa siku. Kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia, Aramco, pia imeongeza uwekezaji wake wa mabilioni ya dola nchini China.

Hamu ya Saudi Arabia ya kuwa mwanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na kundi la BRICS na kualikwa Saudia na pia Umoja wa Falme za Kiarabu kujiunga na kambi ya BRICS vinaonyesha taswira nyingine ya jinsi nchi hizi mbili zinavyoendelea kujitenga na kuwa mbali na Marekani.

Uhusiano wa nchi kama Imarati na Saudi Arabia na China katika mfumo wa BRICS na hata Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai unaonyesha kuwa, washirika wakuu wa nchi za Magharibi katika Ghuba ya Uajemi wametia mguu kwenye njia ya mashirikiano mapya na kuendeleza uhusiano na jumuiya na kambi zote; na kwa ufahamu sahihi wa mchakato wa kubadilika uwiano wa nguvu na kuongeza idadi na uzito wa wachezaji muhimu wasio wa Magharibi katika dunia ya sasa, Saudia na Imarati zinajaribu kufanya kazi na nchi na kambi zote na sio kujinyima faida za kuwa na uhusiano na wachezaji na kambi nyingine.

Katika muktadhaa huo, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimejitenga na mtazamo wa Marekani katika masuala kama vile uzalishaji wa mafuta, vita vya Ukraine, na uhusiano wao na Iran na Syria. Inaonekana kwamba, Saudi Arabia, - kwa kujua kwamba haipaswi kuweka mayai yake yote kwenye kapu la nchi za Magharibi,- inataka kuwa na msimamo wa kujitegemea na kuwa huru zaidi katika mfumo wa kiuchumi na kisiasa wa dunia ya siku zijazo.

Kutokana na kujiunga Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu katika kundi la nchi za BRICS, muungano huo sasa unajumuisha wazalishaji na wauzaji wakuu wa mafuta duniani, na jambo hili litaiwezesha BRICS kuwa na nafasi nzuri zaidi katika kufutilia mbali sarafu ya dola ya Marekani.



Mchakato wa kufuta sarafu ya dola ya Marekani katika miamala na biashara ya kimataifa ni matokeo ya mienendo mibaya ya Marekani yenyewe. Katika miaka ya hivi karibuni, vikwazo vya kifedha vya upande mmoja vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi mbalimbali vimezidisha ulazima na udharura wa kutupiliwa mbali dola, jambo ambalo sasa limekubaliwa kimataifa kwa jumla.

Viongozi wa nchi za BRICS daima wanasisitiza umuhimu wa matumizi ya sarafu za ndani katika biashara ya kimataifa, ubadilishanaji wa fedha kati ya nchi za BRICS na washirika wao wa kibiashara, na kuhimiza uimarishaji wa mitandao ya benki kati ya nchi za BRICS na kadhalika.

Wakati nguvu ya kisiasa na kiuchumi ya taasisi za Marekani na Magharibi kwa ujumla inadhoofika, viashiria vinaonyesha kuimarika kwa madola na jumuiya zinazoibukia kwa kasi kama vile BRICS.

Ukitoa Afrika Kusini, nchi nyingine nne wanachama wa BRICS ni miongoni mwa nchi saba zinazoongoza kwa kuwa na eneo kubwa na ni kati ya nchi 10 duniani zinazoongoza kwa idadi ya watu na Pato la Taifa. Majeshi matatu kati ya matano makubwa duniani ni wanachama wa BRICS. Vilevile nchi tano wanachama wa BRICS zinaunda karibu 40% ya jamii ya watu wote duniani, zina takriban robo ya Pato la Taifa na karibu theluthi moja ya ardhi ya dunia.

Kwa kutilia maana haya yote tunaweza kusema kuwa, mwelekeo wa Saudi Arabia na Imarati wa kujitenga na Marekani na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wao na madola yanayoibukia kwa kasi kawa manachama wa BRICS ni sahihi kabisa na unaendana na mabadiliko na hali ya kimataifa, na vilevile unadhamini maslahi ya nchi hizi.

4c3oee864d43692crms_800C450.jpg
4c3oe93d1aca462cra7_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom