Miradi ya Maprofesa wa Bongo

Hio no 9. Kuna Doctor kauza shule, mwingine ni profesa nae ilimshinda miaka 5 iliopita akawapa kanisa. Yaani wachungaji na mapadri wanaweza kuendesha shule kuliko maptofesa.
Inasikitisha sana
 
Professor wanafundisha vyuo vitano kwa wakati mmoja ? Kumbe tuna uhaba wa professors hivi ? Ni mkoa gani huo Mkuu vyuo vitano vipo karibu hadi professor akafundishe kote. Lazima wana pesa sana
 
Kaka tembea uone,SUA hakuna prof masikini nakuambia wale jamaa wanamiradi wanaandika na proposal na yanafadhiliwa vizuri
Basi itabidi siku moja nifike hapo SUA nijionee,pia huwa ninatamani sana kufika hapo nipate moja na mbili kuhusu kilimo na ufugaji
 
Umesema vyema mkuu
 
Kaka tembea uone,SUA hakuna prof masikini nakuambia wale jamaa wanamiradi wanaandika na proposal na yanafadhiliwa vizuri
si kweli, ni wachache waliotoboa kupitia miradi. Wengi maisha yao ni ya kawaida na wengine maisha yao ni magumu zaidi baada ya kustaafu wanahangaika na contracts kwenye private universities. huu ni ukweli niliouona baada ya kufanya nao kazi zaidi ya miaka 10
 
Mbona hiyo faida ndogo sana, kuna wafanya biashara hulipa mishahara ya wafanyakazi wake zaidi ya milioni 70, sasa kama haitoki kwenye faida analipa kutoka kwenye mtaji.
Je unadhani akishalipa mishahara yeye hubaki na fedha chini ya milion 70?

Ndugu yangu kuna watu wamewwkeza vya kutosha, hebu fikilia mtu mmoja anamiliki gari 300 za kazi, na miradi mingine mikubwa alafu unaongelea faida ya milioni 70, ni hela ndogo sana

Ila tukirudi kwenye mada profesa si mfanya biashara, hatupasi kuwafananisha.
 
Miaka hii vyuo kuna vitini
 
Haya ndiyo maisha Watanzania tunapenda! Kutumia muda wetu mwingi kujadili maisha ya watu wengine, kujadili mapenzi, na kujadili habari za Yanga ma simba.

Wakati tunapoteza muda wetu mwingi kujadili useless things, wenzetu wenye ngozi nyeupe wanazidi tu kutupiga gap la maendeleo kupitia raslimali zetu tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu.
 
Uprofesa bila pesa ni ubwege

Shida hamuujui uprofesa. Kila mtu anaongea ya kwake ilimradi kuonesha uprofesa hauna maana. Mpaka ufike uprofesa sio kazi rahisi, ndio maana kwa Sasa Tanzania maprofesa hawazidi 66 ( full professor).
 
Hawa jamaa ni watu wa ajabu pale UD wengine ukienda ofisi zao kuwaulizia usipotaja mwanzoni title ya Prof...

Ukasema Mr...

Wanakukaushia. Jamaa wana mambo ya ajabu sana. Wanapenda sana sifa na kunyenyekewa

Wewe utakuwa una hasira na Maprofesa sio Siri. Unaona shida kumpa mtu title yake ya uprof?. Nenda jeshini basi umwite Major General au Luteni General kwa kutumia Mr. Acheni dharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…