1. Ng'ombe wawili wa maziwa
2. BAR
3. LODGE
4. Mbogamboga nusu heka
5. STESHENARI (Vitini vinapatikana hapo tu na vitabu vyake)
6. DALADALA
7. SHULE (huyu amejitutumua sana ila kusimamia hawezi)
8. Tax
9.Kukodisha viti na matenti
10.Bucha kwa wale wa SUA.
Ongezea
Wabongo bwana!
Unataka profesa afanye biashara gani ya maana itakayompa muda wa kufundisha, kufanya utafiti na kuisimamia vyema? Mtaji wa kufanyia biashara kubwa kubwa (za kimataifa) atautoa wapi kama mshahara wake ni milioni tatu? Hata kama huo mtaji anao, huo muda wa kuisimamia hiyo biashara mpaka ikasimame katika mazingira haya ya Tanzania atautoa wapi? Au unafikiri ukiwa profesa basi milango yote inafunguka na kila kitu ni rahisi tu?
Umeshatembea nje ya Tanzania
hasa huko duniani ukaona hao maprofesa hata kama wana muda wa kufanya biashara?
Kazi kubwa ya profesa ni nini? Unajua profesa anapatikanaje?
Hebu nenda Marekani au Ulaya (Asia sina uhakika) ukatafute profesa ambaye anafanya biashara yake binafsi ....mbali na pengine consulting ambayo nayo chuo ni lazima kijue.
Wenzetu wanajua kuwa kazi kuu ya profesa ni kunoa kizazi kijacho, kufanya utafiti na kuandika mawazo yake ili kundeleza maarifa ya jamii. Na profesa hategemewi kutajirika wala kuwa mfanyabiashara. Ndiyo maana elimu yao imewasaidia
Hawa wa kwetu inabidi wajaribu hizi biashara kwa sababu jamii inaamini kuwa msomi bila kutajirika elimu yake haijamsaidia....haijalishi kama ameandika vitabu na machapisho yatakayosomwa na vizazi vingi vijavyo! Yaani hatujui hata elimu yetu hii inapaswa kutufanyia nini. Na kama lengo lake pekee ni kuwatajirisha waipatayo basi kama jamii we are doomed! Na ni mtazamo huu huu kengeufu wa jamii ndiyo unaimarisha ufisadi huu wa kutisha. Kila mtu akisoma na kupata ka cheo anachangamka aibe haraka haraka atajirike ili asije akachekwa na jamii huko mbele ya safari. Hatuheshimu decent work ya wasomi wetu ambao wametumia elimu yao kwa manufaa ya jamii. Kila kitu kinapimwa katika mizani ya utajiri hata bila kujali utajiri huo umepatikanaje halafu watu wakiiba mpaka trillions tunaanza kulalamika 😬
Hata akina Einstein, Maxwell, Bohr, Newton, Currie na magwiji wengine wa sayansi na taaluma zingine wangetokea kuishi Afrika/Tanzania wangeishia kuchekwa tu maana wengi wao hawakuwa na biashara zo zote na wala hawakuwahi kutajirika....lakini michango yao imenufaisha si jamii zao tu bali dunia nzima!
Tuwaache maprofesa watufundishie watoto wetu. Tuwaache wawasimamie na kuwaongoza watoto wetu katika tafiti zao za uzamili na uzamifu. Tuwaache wafanye tafiti zao. Tuwaache waandike vitabu na makala ili watuachie maarifa yao. Na ikibidi tuwaongezee mishahara na marupurupu ili waachane na hivi vibiashara uchwara ambavyo vinawapotezea muda wao bure tu; na wawe na hadhi kama wenzao huko duniani maana maprofesa wenyewe sijui kama wanafika hata 1,000!