zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,154
- 28,890
Habari za weekend wanajukwaa
Kumekuwa na kelele nyingi sana kutoka kwa wafuasi wa JPM kwamba miradi itakufa ama miradi haitofanyika sababu JPM hayupo. Na wengine wameenda mbali sana na kusema hakuna aliyewahi kufanya miradi kama ilivyofanyika awamu ya tano. Hapo chini nimeweka mifano tu ya miradi awamu ya nne kwa kuweka rekodi sawa kuwakilisha awamu zingine zilizopita kabla ya JPM.
1. Mradi wa Bomba la gesi ulicost matrilioni ya fedha na ulifanyika enzi za JK na Leo hii umeme wa Tanzania kwa 60% unategemea Bomba lile la gesi.
2. Barabara za lami zilijengwa almost Kila mkoa Ili kuunganisha mikoa jirani; pamoja na madaraja ya kumwaga kama Malagarasi n.k. So kama ni miundombinu ya barabara kikwete aliwekeza sana.
3. Mfumo wa Barabara za mwendokasi uliasisiwa kipindi hiki na serikali ya JK Ilimwaga mabilioni kujenga mwendokasi na kuagiza mabasi husika.
4. Airport ya J.K Nyerere Airport ilipanuliwa awamu ya nne. Leo hii tuna Airport yenye Hadhi ya kimataifa jambo ambalo halikufanyika tokea uhuru!!
5. Uzalishaji umeme ulipanuliwa kwa kujenga kituo Cha kufua umeme wa gesi pale Kinyerezi. Hatua hii iliongeza capacity ya uzalishaji umeme kuliko awamu zote zilizopita!!
6. Kulifanyika mradi mkubwa wa kutoa Maji ziwa Victoria kuelekea mikoa ya Kanda ya kati. Mradi ule umefika mpaka mkoa wa Tabora na Sasa unaelekea Singida!! Hayo ni mabilioni na ubunifu wa hali ya juu licha ya kelele kutoka kwa mataifa kama Misri yaliyopinga kabisa kuguswa Maji ya ziwa Victoria.
Hii ni mifano tu ya haraka haraka kwenye eneo la miundombinu. Kwahiyo tuache hizi propaganda kwamba miradi ilianza awamu ya 5 na imeisha awamu ya 5 ni uzembe tu wa kufikiri. Hiyo miradi tajwa hapo juu ingefanyika awamu ya 5 nadhani kelele zingekua nyingi mnoo.
Ni vizuri tuheshimiane Kila awamu, alipoishia Nyerere, mkapa aliendeleza and so on hata Mama Samia anaendeleza anapoweza so tusijikweze kweze na kelele nyingi as if JPM alikua Alpha na Omega.
Naomba kuwasilisha