Tukabidhi miradi na taasisi kwa wawekezaji na sisi tusilipe kodi bali tulipie huduma

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
4,140
3,767
Awamu ya tano wamekuja na miradi ya PPT yaani muwekezaji anapewa mradi anaujenga kwa gharama zake kisha anaweka gharama za utumiaji ili kurejesha gharama alizotumia plus faida labda kwa miaka 30 baadae ule mradi ndio unarudi kwa serikali.

kwa maelezo ni miradi mizuri tu hata Congo ndio wanafanya ila wenyewe wachina wana chaji kipindi kabla haujaisha na ukiisha wanaendelea kukusanya. Congo ilikuwa ni njia za tope kwa miaka mingi lakini uwepo wa hii miradi umesaidia sana kujengewa barabara na wachina.

Sasa bongo tukabidhi taasisi kama Moruwasa wapewe wachina watuuzie maji na wajilipe wenyewe gharama za uendeshaji nafikiri maji tutapata hadi Kingolwira na kitungwa.bila kukatika maana kukosekana kwa maji ndio hasara kwao.

Kama tunawaza hivi, serikali ichukue kodi kwenye bandari ndio wagharamie mambo yote halafu sisi wananchi tusiwe na kodi kwa kuwa hospital tushalipia bima ya wote.elimi kuna hao wahisani watatoa vitabu na ujenzi umeshakamilika mpaka watoto hawapo wa kuandikishwa barabara wawape wachina watuchaji kila tunapotumia.

Nafikili kwetu kingolwira barabara zitajaa tele.
 
Back
Top Bottom