Miongoni mwa maswali ya UONGO na KIJINGA

Miongoni mwa maswali ya UONGO na KIJINGA

Kwahiyo unatuthibitishia kuwa kitendo cha Mungu wako kuumba kitu kilichomzidi au sawa na yeye STATUS yake inakuwa imeshuka au imepanda ? nataka kujua unaelewa nini juu ya STATUS

Kweli Wewe ndugu utakuwa ni mgumu kuelewa, sasa nikuulize aumbe hicho unachotaka kikiuke sifa zake za ukuu na umoja wake ili iweje??---- Si atakuwa Mungu kigeugeu na hata hatakuwa tena na hadhi ya kuabudiwa tena kwa sifa za; , Allah akbar au Allah ahad, kwa sababu tayari atakuwepo kisha umba MKUBWA WAKE ambapo jambo hilo kamwe haliwezekani kufanywa na Mungu Mungu ni mwivu sana na UMOJA wake na ndiyo maana mtu atakayefanya Shirk hapa duniani siku ya hukumu Mungu hato msamehe huyo mtu, hivyo sasa Mungu hawezi kuumba kiumbe mwingine zaidi yake ili kujiwekea heshima na utukufu wake kwa KANUNI zake mwenyewe.

Mfano leo Magufuli hawezi kuteua Raisi mwingine mkubwa awe juu yake kwa sababu kanuni (katiba) inamkataza na kama akifanya hivyo wewe utamuelewa???🤣🤣-- take that analogy and work on it.
 
Mkuu sijajua Quran inasemaje
Lakini Bible inasema kabla ya uasi kifo hakikuwepo ila baada ya uasi wa Adam ndio uwepo wa kifo ukatokea
Nakupa faida kutoka katika Qur'aan juu ya kifo.

Anasema Allah aliye juu :

78. Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu. Na likiwafikilia jema wanasema: Hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na likiwafikilia ovu wanasema: Hili limetoka kwako wewe. Sema: Yote yanatokana na Mwenyezi Mungu. Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno? ( an Nisaa : 78 )
 
Ili nikuonyeshe kwamba uongo wa swali hilo uko wapi,naomba ujibu swali hili "Kwanini unataka aumbe kitu kilicho mzidi ?

Ili iweje ? Je akiumba kitu kilicho mzidi ndio kitaonyesha ukamilifu wake au udhaifu wake wa kuumba kitu kilicho mzidi ?

Kuumba kikicho kuzidi maarifa au uwezo huonyesha ukamilifu au udhaifu ?
1.kwanini unataka aumbe kitu kilichomzidi?
Jibu: Kwasababu Mola ametangaza anaweza kuumba apendavyo na atakacho , ndio nikataka kujua anaweza kuumba kitu kilichomzidi yeye

2.Akiumba kitu kilichomzidi ndio ataonyesha ukamilifu wake au udhaifu wake ?
Jibu : kama uwezo wa kuumba kitu kilichomzidi anao kweli basi atakuwa msema kweli , kinyume chake ni muongo

3.Kuumba kilichokuzidi maarifa huonyesha ukamilifu auq udhaifu
JIbu : huonyesha ukamilifu maana umeyaishi unayoyanena , kuwa anaweza kuumba kitu chochote atakacho
 
Very good point, aumbe kitu kilichomzidi bila sababu!! ??🤣🤣
 
Kweli Wewe ndugu utakuwa ni mgumu kuelewa, sasa nikuulize aumbe hicho unachotaka kikiuke sifa zake za ukuu na umoja wake ili iweje??---- Si atakuwa Mungu kigeugeu na hata hatakuwa tena na hadhi ya kuabudiwa tena kwa difa za; , Allah akbar au Allah ahad, kwa sababu tayari atakuwepo kisha umba MKUBWA WAKE ambapo jambo hilo kamwe haliwezekani kufanywa na Mungu Mungu ni mwivu ssna na UMOJA wake na ndiyo masna mtu atakayefanya Shirk hapa duniani siku ya hukumu Mungu hata msamehe huyo mtu, hivyo sasa Mungu hawezi kuumba kiumbe mwingine zaidi yake ili kujiwekea heshima na utukufu wake kwa KANUNI zake mwenyewe.

Mfano leo Magufuli hawezi kutrua Raisi mwingine mkubwa awe juu yake kwa sababu kanuni (katiba) inamkataza na kama akifanya hivyo wewe utamuelewa???🤣🤣-- take that analogy and work on it.
Hivi wewe una utimamu wa akili kweli !!.kinyago umechonga mwenyewe unakiogopea nini !! yaani Mungu gani anaogopa kuumba kiumbe kilichomzidi akili ? yaani anaogopa kinyago chake mwenyewe hopeless kabisa Mungu wako
 
1.kwanini unataka aumbe kitu kilichomzidi?
Jibu: Kwasababu Mola ametangaza anaweza kuumba apendavyo na atakacho , ndio nikataka kujua anaweza kuumba kitu kilichomzidi yeye

Sasa kama unakubali Mola anaumba anachokitaka au anachokipenda,sasa kwanini wewe utake kumpangia kuumba unachokitaka wewe ?

Sasa subiri siku akitaka au kupenda kufanya hivyo.

Pili,hivi kutaka au kupenda kuna uhusiano gani na kutoweza ?

Je mwenye kuweza,kutaka au kupenda vipi asiweze ?
2.Akiumba kitu kilichomzidi ndio ataonyesha ukamilifu wake au udhaifu wake ?
Jibu : kama uwezo wa kuumba kitu kilichomzidi anao kweli basi atakuwa msema kweli , kinyume chake ni muongo

Hapa naona umeenda kinyume na uhalisia na kuukataa ukweli.

Unaweza kuniambia mwanadamu amesha tengeneza kitu kilicho mzidi maarifa au uwezo ?

Ni lini na ni wapi ulishawahi kuona kilichozidi uwezo wa mtengenezaji huonyesha ujuzi na kuweza kwa mtengenezaji ?
3.Kuumba kilichokuzidi maarifa huonyesha ukamilifu auq udhaifu
JIbu : huonyesha ukamilifu maana umeyaishi unayoyanena , kuwa anaweza kuumba kitu chochote atakacho

Nazidi kuamini ya kuwa hakuna nazi iliyo shindana na jiwe.

Chukulia mfano,ingekuwepo vipi maana ya mjenzi asie weza kukimiliki alichokijenga na kuki control ?
 
Unaweza kuniwekea hapa hilo andiko ?

Kwetu sisi Waislamu tuna amini ya kuwa kifo ni kiumbe pia na mwanadamu ni kiumbe wa mwisho kuumbwa,kwa maana hiyo ni kuwa kifo kilikuwepo hata kabla ya mwanadamu kuwepo bali kilinza kifo ndio ukafata uhai.
Walianza kufa baada ya kula tunda na kutolewa bustanini
 
Sasa kama unakubali Mola anaumba anachokitaka au anachokipenda,sasa kwanini wewe utake kumpangia kuumba unachokitaka wewe ?

Sasa subiri siku akitaka au kupenda kufanya hivyo.

Pili,hivi kutaka au kupenda kuna uhusiano gani na kutoweza ?

Je mwenye kuweza,kutaka au kupenda vipi asiweze ?

Hapa naona umeenda kinyume na uhalisia na kuukataa ukweli.

Unaweza kuniambia mwanadamu amesha tengeneza kitu kilicho mzidi maarifa au uwezo ?

Ni lini na ni wapi ulishawahi kuona kilichozidi uwezo wa mtengenezaji huonyesha ujuzi na kuweza kwa mtengenezaji ?

Nazidi kuamini ya kuwa hakuna nazi iliyo shindana na jiwe.

Chukulia mfano,ingekuwepo vipi maana ya mjenzi asie weza kukimiliki alichokijenga na kuki control ?
1.Mola wako ametangaza mwenyewe kuwa anaweza kuumba kitu chochote , tunapohoji kuumba kitu kilichomzidi uwezo mnasema maswali ya uongo mambo yakiwa magumu mnasema subir akiamua mwenyewe kuumba ataumba , kuhusu kutaka na kuweza lazima ufahamu atujamwambia aumbe sasa tunataka kujua huo uwezo anao wa kuumba kilichomzidi ?

2.Mwanadamu ametangaza wapi kuwa anao uwezo wa kuumba kitu chochote ? sisi tunadeal na alietangaza uwezo wa kufanya anao kumbe ni dhaifu wa kuogopa vinyago vyake

3.Mungu wako anapotangaza jambo kuwa anao uwezo wa kulifanya alafu waumini mnasema hawezi kwa.sababu itakuwa ni udhaifu kwake hii inachekesha sana
 
Umepata wapi hayo maneno ?
Mwanzo 2:16 BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
 
Mwanzo 3: 17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
 
Mwanzo 2:16 BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

( وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ )

الأعراف (19) Al-A'raaf

Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu.

( فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ )

الأعراف (20) Al-A'raaf

Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele.

( وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ )

الأعراف (21) Al-A'raaf

Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini.

( فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ )

الأعراف (22) Al-A'raaf

Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa dhaahiri?

( قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ )

الأعراف (23) Al-A'raaf

Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.
BAADA YA KULA TUNDA MAAGIZO NDIO AYA YA KWANZA kuwa sasa wataishi muda mfupi tu ardhini baada ya kutolewa bustanini

( قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ )

الأعراف (24) Al-A'raaf

Akasema: Teremkeni! Mtakuwa nyinyi kwa nyinyi maadui. Na kwenye ardhi itakuwa ndio makao yenu na starehe yenu mpaka ufike muda.

( قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ )

الأعراف (25) Al-A'raaf

Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa.
 
Kwahiyo unatuthibitishia kuwa kitendo cha Mungu wako kuumba kitu kilichomzidi au sawa na yeye STATUS yake inakuwa imeshuka au imepanda ? nataka kujua unaelewa nini juu ya STATUS
Hakuna kitu ambacho kipo juu ya Mungu,yeye mwenyewe anasema Mimi ni Wa Kwanza na Mwisho,Mimi ni Yehova.
 
Back
Top Bottom