Miongoni mwa maswali ya UONGO na KIJINGA

Kwa akili za binadamu,huna hata mamlaka kidogo tu ya kutafakari ukubwa wa Mungu,na hivyo majibu ya maswali hayo yatatokea katika upumbavu kama ambavyo maswali yametokea.

Uwezo wetu wa kufikiri una ukomo kama tunavyoona watoto wadogo walivyo na ukomo kwenye kufikiri
 
Kwa kifupi Mola anaweza yote..
Tena andiko lanena..
Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?
Je, anaweza kutengeneza gereza lenye ulinzi mkali ambalo hawezi kutoroka? 😆
 
Mola hawezi fanya hayo yote; lakini Mungu, Jehova Bwana wa majeshi, aliye mtoa mwanawe wa pekee ili tupate uzima mbona anaweza! na siku akija kila Goti litapigwa na kila kinywa kita kiri aah! kweli wewe ni Bwana.

Mola hana mtoto hafananii na kitu chochote hapa Duniani na ahela.
 
Duuh wewe kweli kichwa maji tunajadili "UWEZO " wa Mungu wako kuumba kitu kilichomzidi uwezo , wewe ata ujui tunajadili nini hapa, swali uwezo huo anao ?
Hiki kipindi ulikuwa bado mzima unauliza maswali yaliyoenda shule ya msingi St Patrick siku hizi unauliza na kujenga hoja zilizoenda UDOM university 😅 ni tatizo sana
 
Haya ni maswali ya uongo na ya kijinga,kama yupo anae pinga athibitishe kwamba maswali haya si ya uongo wala sio ya kijinga.

Haya sio maswali ya uongo na kijinga bali ni maswali fikirishi, ni maswali yanayomfanya mtu afikiri ama positive au negative juu ya Mungu.

Watu Wenye faida ni wale wanaofikiri positive.
 
Ujinga ni kinyume cha elimu. Huu ujinga umegawanyika sehemu mbili :

1. Ujinga ambao dhidi yake ni elimu.

2. Ujinga ambao dhidi yake ni hila

Aina zote hizi mbili nimezizingatia katika mada yangu hii.

Ama kuhusu uongo ni kinyume cha ukweli. Huu nao umegawanyika sehemu kuu mbili:

1. Uongo wa Kauli

2. Uongo wa matendo

Hapa katika uongo natilia mkazo kauli ya mja mwema mmoja tena mwanazuoni aliposema "Laiti kama UONGO ungekuwa ni jambo jema na lenye kuruhusiwa basi mimi nisingesema uongo kwa ajili ya kujitakasa"

Uongo ni tabia mbaya,tabia ambayo hatakiwi yeyote yule apambike kwayo.

Baada ya utangulizi huo. Yafuatayo ni maswali ya uongo na kijinga.

1. Je Mola anaweza kuumba kitu sawa na Yeye ?

2. Je Mola anaweza kumtoa kiumbe wake nje ya milki yake ?

3. Je Mola anaweza anaweza kuumba jiwe ambalo hawezi kulibeba ?

4. Kwa kuwa Mola ameumba viumbe baada ya kutokuwepo viumbe hivyo hapo kabla,Je Mola anaweza kuona au kujua kitu tu ambacho hakipo ?

Haya ni maswali ya uongo na ya kijinga,kama yupo anae pinga athibitishe kwamba maswali haya si ya uongo wala sio ya kijinga.
HE GOT IT ALL IN HIS HANDS WE ARE JUST UNDERLINE WHAT IS WRITTEN, WE HAVE NO ONE 2 BLAME, ECCEPT U DUIN THNGS ON U'R OWN
 
Hiki kipindi ulikuwa bado mzima unauliza maswali yaliyoenda shule ya msingi St Patrick siku hizi unauliza na kujenga hoja zilizoenda UDOM university 😅 ni tatizo sana
Mimi kama maji shapeless , najua udhaifu na uimara wa kila mmoja wenu hivyo amunisumbui
 
Haya sio maswali ya uongo na kijinga bali ni maswali fikirishi, ni maswali yanayomfanya mtu afikiri ama positive au negative juu ya Mungu.

Watu Wenye faida ni wale wanaofikiri positive.
Thibitisha.
 
Thibitisha.

Kwanza ni hivi; kujenga maswali na kujiuliza au kuuliza ndiyo asili ya sifa au tabia ya akili ya mwanadamu, viumbe hai wengine minghairi ya wanadamu hawana akili yenye sifa hiyo na ndiyo maana sisi wanadamu huwa tunajitambua kila mtu kwa kadiri ya utambuzi wake aliojaliwa na Allah na ni kutokana na utambuzi wetu huo ndipo tukawekewa Sheria na Allah na hatimaye twende kuhukumiwa siku ya Qiyama, viumbe wengine kamwe hawahusiki na Qiyama.

Sasa, uongo au ujinga wa mtu hutokea baada mtu kujiuliza maswali na kupata jawabu la maswali hayo, kama jawabu ni la uongo au ujinga ndipo hapo utakapo sema mtu huyo ni muongo au mjinga, mfano mtu aulize je Allah anaweza kuumba Mungu mwingine atakayefanana naye??--- hilo sio swali la uongo kwasababu lipo na wala sio la kijinga kwasababu linahitaji mantiki kupata jibu, mantiki inakataa kutokana na sifa hizi za Allah kwamba Yeye ni mmoja na wala hana mshiriki na hafanani na chochote hivyo kamwe hawezi kumuumba Mungu mwingine ili wafanane na wawe sawa na juu yote hata tufanye aweze kumuumba bado mmoja atakuwa kaumbwa (kiumbe cha mmoja) na mwingine atakuwa Muumbaji hivyo hawatofanana kwa sifa. Sasa akitokea mtu akasema kuwa Allah anaweza kuumba Mungu mwingine kama yeye hapo sasa huyo mtu huwa ndiye Mjinga na Muongo na hapo wa kulaumiwa sio swali bali ni matokeo ya swali (jibu) na muhusika wa hilo jibu, kinyume chake ni mtu atakaye toa majibu ya kimantiki basi atapongezwa yeye pamoja na majibu yake.

Kama nitakuwa nimekuelewa, hivyo ndivyo nionavyo.
 
Kama nimekuelewa ni kwamba maswali yote yapo , ya uongo na ya kijinga na hapa ndipo hekima inapotakiwa kuyajibu ili muulizaji aweze kujua kama aliuliza swali la kijinga au la uongo.
Mfano wa swali lililoshikiliwa sana humu ni " Mungu anaweza kuumba kiumbe kinachozidi uwezo wake ?"
Ni dhahiri kuwa Mungu hakuanza na wala hana mwisho sasa iweje aumbe kiumbe kinachomzidi !
Tayari hicho kiumbe hakitakuwa kinamzidi kwa kuwa kimekosa sifa ya kutoanza hivyo hilo swali muulizaji kama angemjua Mungu wala asingeuliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna swali la kijnga bali kuna mtu mjinga tu na mtu mjinga anapouliza swali anataka kujua ill li ujinga wake uondoke.

Hilo swali lako ni swali fikirishi la mtu mjinga anayehitaji kuelimishwa tu na sio vingjnevyo.
 
Back
Top Bottom