Nimesoma sana haka ka thread nikaona na mimi nichangie upuuzi wangu japo kidogo,
Katika mahusiano ya siku hizi kuna vitu kadhaa vinavyosababisha mahusiano hayo kutodumu au kuwa na matatizo na migogoro mingi sana. Baadhi ya matatizo haya ni yale ya kawaida ambayo hata zamani yalikuwepo na mengine ni yale yaliyoibuka hivi karibuni. Labda nianze na yale ya kawaida;
Mara nyingi watu wanapoingia kwenye mahusiano huwa wanakuwa na expectations fulani kutoka kwa upande wa pili na pindi inapotokea bahati mbaya zisitokee basi ndipo migogoro huanza kutokea na kufikia kuvunjika kwa mahusiano. Kwa mfano mtazamo wa nje humfanya muhusika mmoja kujenga taswira ya mwenzie na hivyo kuwa na picha ya huyo mwenzie hata kabla hawajawa pamoja, pindi inapotokea kwamba taswira aliyoitengeneza sivyo basi hufadhaika na kuamua kuendelea kutafuta taswira yake hata wakati mwingine akiwa bado na huyu aliyenaye.
sababu nyingine ni mapungufu ya kawaida ya kibinadamu; Haya unaweza kuyataja kwa urefu wake lakini kama mmoja wa upande wa pili hataridhishwa na mapungufu ya upande mwingine basi huweza kupelekea mahusiano kuvunjika. Muhimu kabisa katika mahusiano ni upole hata pale inapotokea kuna jambo baya limetokea, kusikiliza hata pale inakuwa umekosewa na kusamehe kwa kweli bila kuweka kinyongo na kukumbushia kila mara.
Sasa kwa yale ya siku hizi,
Kutoaminiana; Hili limekuwa tatizo kubwa sana siku hizi kutokana na mazingira na hali halisi ya masiha. Watu wanaingia kwenye mahusiano lakini wanakuwa hawaaminiani kitu ambacho kimekuwa kinapelekea watu hao kuwa na multiple relationships. Hii ni kwa pande zote mbili, wanawake wanawalalamikia wanaume na huku upande mwingine wanaume wanawalalamikia wanawake. Mahusiano kudumu hutaka vitu vingi ikiwemo commitment ya hali ya juu sana na sacrifice kwa kiwango fulani. Commitment hufanya mtu awe tayari kusamehe na kuendelea kuwepo na sacrifice humfanya mtu afikirie mara mbili kabla hajafanya kitu huenda anachokipenda lakini kama kinaweza kumkwaza mwenzie.
Relationships for a purpose; Hili ni tatizo kubwa sana, kwa bahati mbaya sana hili liko zaidi kwa mabinti (jinsia ya kike) kila wanapotaka kuingia kwenye mahusiano huangalia zaidi mtu wanayetaka kuingia naye kwenye mahusiano yukoje financially. Sasa tatizo hili limekuwa na kuhamia kwa wanaume ambao sasa wanaamini kabisa kama uko stable financially then unaweza kumpata mwanamke yoyote na since now they see women kama product like a pair of shoes then wakimchoka mmoja wanahamia kwa mwingine na maisha yanaendelea bila kuangalia maumivu wanayoyaacha nyuma yao.
Nimechoka kuandika ntaendelea baadae ngoja nifanye kazi za watu kwanza
CC.
snowhite nimekumiss