Mimi ni mzima - Lema

Mimi ni mzima - Lema

Nimeona kwenye mitandao kuwa mimi pamoja na Mkiti wa Vijana Taifa kuwa tumepata ajali, taarifa hizo sio za kweli isipokuwa leo mchana wakati tunajaribu kuwahi mkutano Kahama gari letu lilipata pancha ya kawaida sana na ilituchukua muda mrefu kurekebisha na hivyo kushindwa kufika Kahama.

Sisi ni wazima na sasa niko Dar nimewasili jioni hii..
pole kamanda, kwani humu kuna mijinga ilikuwa imeshaanza kuulizia eti mambo ya uchaguzi mdogo Arusha!! kwa jinsi ulivyotishio kwa Magamba.
 
Mkuu siku zako bado ni nyingi kwasababu nyinyi ndio watu mlio teuliwa kuikomboa nchi kwa wale wanao waombea mabaya kwa sasa wanapoteza muda. Mkuu wewe kufa labda mpaka umalize kazi tuliyo kutuma
 
Pole sana kamanda .mungu akulinde we ndo jembe . Tunakusubiria ars kwa hamu. People'ssssss.
 
Duuuuh vipi hamkuwa na spea tairi? ??? Kamanda anaahirisha mkutano kisa pancha kazi ipo
 
Pole msela wangu mibnafsi nilishitushwa sanaa mpaka now cko poa kivile ila nilipompigia dreva wake akanitoa hofu haleluya ameeeeee huuuuuuuuuu haaaaaa
 
Kamanda,

Nafikiri kuwa umuhimu wa kuwa na Business Continuity Plan (BCP) katika taasisi yenu. Mmepata pancha mkashindwa kufika Kahama, naamini kuna wananchi huko walikuwa wakiwasubiri kwa hamu but impression mliyoiacha uko wanaweza wakafikiri mmewa-ignore. Kuelekea uchaguzi mkuu mnatakiwa kuwa na BCP, akishindwa Lema au kiongozi yeyote kufika sehemu fulani kwa muda fulani then awepo alternative individual(s) ambaye (w)anaweza kwenda kuonana na hiyo audience kuepuka undesired perception kwa chama. Mngekuwa na spare tire naamini mngechelewa kidogo kufika Kahama, but still mngeweza kuonana na wananchi angalau kwa muda mchache. Ni mtazamo wangu tu.

Ni kweli wew unaamini ni pancha ndo imewafanya kushindwa kufika mkuu
 
Nimeona kwenye mitandao kuwa mimi pamoja na Mkiti wa Vijana Taifa kuwa tumepata ajali, taarifa hizo sio za kweli isipokuwa leo mchana wakati tunajaribu kuwahi mkutano Kahama gari letu lilipata pancha ya kawaida sana na ilituchukua muda mrefu kurekebisha na hivyo kushindwa kufika Kahama.

Sisi ni wazima na sasa niko Dar nimewasili jioni hii..

Kweli chadema mna watu wa hovyo hovyo kabisa gari ilipata pancha mkachukua MDA MREFU KUREKEBISHA na kwa sasa mko dar
unajua umbali wa kutoka shinyanga Dar + FOLLEN za Dar mmetumia ndege ?kwa kweli wajinga ndo waliwao pole sana kwa kutudanganya kamanda
 
Mungu azidi kuwapa uzima na muendeleze mapambano
 
Lema, acha uongo yaani pancha tu iwafanye mrudi Dar es Salaam? Sema ukweli tu baada ya kupiga simu mkutanoni ukaambia hamna watu ukaamua kurudi Dar es Salaam.

hahahaha!hata mimi nimeshangazwa na kauli ya Lema.....pancha ya kawaida ni kubadilisha tairi ni zoezi ambalo halimalizi dk kumi na kuondoka ss nashangaa huo uchelewaji ambao umemfanya hadi ashindwe kufika mkutanoni.....tena ameEnda Dar kabisa. Na bado badala yakumuuliza kulikoni kuna watu wala hawafikirishi akili....!wanasiasa wanatufanya wananchi maboya.
 
Back
Top Bottom