zipompa
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 12,078
- 26,008
hahahhh we jamaa umevurugwasala yako hata Mungu hawezi isikiliza coz now anasikiliza BBC !! Niko town hata kama sio Dar
hahahhh we jamaa umevurugwasala yako hata Mungu hawezi isikiliza coz now anasikiliza BBC !! Niko town hata kama sio Dar
nilikuwa sitaniwi na mtoto, na wala sikuwa na ukaribu nao, wakisikia nipo kila mtu anashika adabu....! miaka hiyo hadi Afisa elimu wa mkoa alikuwa ananijua....!Umchukulie mtoto wakati jitu linakukunjia na ngumi
Kuwa mwl ni kazi kweli, kuna mwalimu alishikiwa jiwe na mtoto wa darasa la sita, na mwingine manati akiwa ni mwanafunzi wa darasa la tano kwa walimu tofauti na siku tofauti, haya yote nimeyaona huku kwetu mtaani lakini wazazi wanapoambiwa watoto wao wanafanya hayo huwa tunakataa hata kama umeona, pia kuna mzazi alishamfuata mwalimu mkuu kwa gudi(fimbo ya kuchungia ng'ombe) na sime kwa kuwa huyo mwalimu alimuadhibu mtoto wake, Leo hii mtoto kaishia darasa la nne na ni dereva bodaboda na muuza cha arusha. Ndomana nasema kikombe hiki kiniepuka nisiwe mwalimu wa school bora nianze kufikiria kuwa mwl wa chuo.Hahahha
Haya bhana
Kikulacho chako umewahi kujiuliza kwanini hali imefikia hapa? Wapi tulikosea na wapi parekebishwe?Andika tu binti....inaweza kuwa faida kwa wengine...
Kwa asiyepitia au kujua kinachotendeka mashuleni, atachukulia simple tu, Ila jamani tunakutana na changamoto za kila aina.Kuwa mwl ni kazi kweli, kuna mwalimu alishikiwa jiwe na mtoto wa darasa la sita, na mwingine manati akiwa ni mwanafunzi wa darasa la tano kwa walimu tofauti na siku tofauti, haya yote nimeyaona huku kwetu mtaani lakini wazazi wanapoambiwa watoto wao wanafanya hayo huwa tunakataa hata kama umeona, pia kuna mzazi alishamfuata mwalimu mkuu kwa gudi(fimbo ya kuchungia ng'ombe) na sime kwa kuwa huyo mwalimu alimuadhibu mtoto wake, Leo hii mtoto kaishia darasa la nne na ni dereva bodaboda na muuza cha arusha. Ndomana nasema kikombe hiki kiniepuka nisiwe mwalimu wa school bora nianze kufikiria kuwa mwl wa chuo.
hahaha. i am a best teacher???!! lol. teacher go back to school please.Sasa ndio umeandika nini hapa? Mi nakwambia we mwalimu kanyaboya tu.
Oooh walimu sijui wana matatizo kisa walifeli sijui nini hivi kuna sekta nchi hii haina matatizo? Madaktari wangapi wanaua wagonjwa kwa uzembe? Mara huyu kapasuliwa kichwa badala ya mguu, haujakaa sawa mgonjwa kapelekwa mochwari akiwa hai nk nk. Mainjinia ndio majengo yanatudondokea kila siku, barabara za lami zinaota mimea katikakti ya lami, mikataba ya ovyo ovyo inasainiwa na wanaojiita wanasheria, nk nk nk nk!! Si ndio hawakufeli hao!!!We njoo tu.
Mie mbona sina tatizo na mashemeji na mabinamu zangu?
Sio kuchachamaa, tatizo humu watu wanajigeuza miungu watu, wanataka wanalofanya ndilo lisikilizwe.
Hakuna hiyooooo
Alafu utegemee huyo mtoto awe wa aina gani?Uskonde Madam. Kazi mnayofanya kubwa.
Hapa nafikiria unamfundisha Mtoto kutoka Tandale au Tandika, Baba misheni town Mama tia maji tia maji, Kaka teja Mjomba jambazi!!!
Wake hatofundishwa na sie wendawazimu maybe ana walimu wake special kutoka mbinguni.hujafa hujaumbika,atakua mwendawazimu kama scorpion.na huko atapigwa tuu maana hakuna namna
Hahahaaaaaa!!! Haki yo nuts.Mkeo yuko na Kiba kule Celebrity, si unajua Kiba anapanda jukwaa moja na Chriss!
We kuchaguliwa hutaki ila unachagulia wenzio!! Kakushauri tu, tena ni ushauri wa msingi mno uchukue utakusaidia.Hahahaaaaaaa
Eti unanichagulia eeeeeh kituko
atoto, mie nimeshamalizana nao.Kikulacho chako umewahi kujiuliza kwanini hali imefikia hapa? Wapi tulikosea na wapi parekebishwe?
Lawama inaanza kwa wazazi kwa namna wanavyolea watoto wao, wengine hawawalei kabisa wameishia kuwatupia wengine hiyo mizigo wawalelee!
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, wazazi mmewalea watoto wenu kibandidu since utotoni,toto linakula bakora tangu akiwa na mwaka mmoja unategemea nini? Mtoto unamuita 'mbwa'sijui mbwa anazaliwa na kuku! So mtoto anakulia katika mazingira ya aina hiyo kiasi kwamba asipopigwa anajihisi kama anawashwa atalitafuta la kulitafuta tu ilimradi aguswe.
Mimi binafsi sipendi kuchapa as natokaga malienge kwenye mikono na naumia mkono pia, na kabla sijamchapa mtoto namuelezea kwanza kosa lake na nampa nafasi ya kujitetea, mwisho namuuliza 'nikikuchapa nitakuwa nimekuonea?' lazima atasema hapana,then anakula bakora na adhabu nyingine kama ipo, lazima atakuja kuomba msamaha tu(kama ni mtoto wa kufundishika)
Pitia post yangu humu nimeandika kuhusu watoto fulani nunda, hao watoto ilifikia hatua mkuu wa shule akasema tumuachie ahangaike nao yeye, ila mwisho wa siku aliwanawa, alikuwa anawaita 'waganga wa kienyeji'(jina la utani not on their presence tho), watoto hao ilinicost alot hadi kufikia wakabadilika, na ilinicost money and time too, so they were lucky!
Shuleni kwetu tuliwahi kuamua kutokutumia fimbo atleast for a month, aisee after 2weeks ilibidi fimbo zirudi maana watoto walitaka kutupanda vichwani. Ni rahisi sana kuongea kama sio mwalimu au hukuwahi kuwa mwalimu, na kuhisi kuwa maybe tunawakomesha watoto or what, tunawapenda sana hawa watoto na tunahangaika nao sanaaa hope mngelitambua hilo, mwalimu ni kila kitu yaani, hadi kesi za majumbani tunaletewa tuhangaike nazo.
Usisahau kuwa hata mwalimu ni binadamu ana breaking point, linapomfika hufanya jambo ambalo hata yeye hapendelei litokee.
Kwa upande wa serikali inaleta siasa tuuuu hata katika masuala ya msingi na muhimu kama elimu, angalia tu sera za elimu ni tafrani tu, kila mtu akikurupuka anakuja na lake, elimu ya msingi imepoteza ile dhana ya umsingi wake.
Msitegemee mshindwe kuwalea watoto katika maadili then utegemee miujiza ikafanywe na walimu, ndio hawa mwisho wanakunjana na walimu wao, wakitoka hapo akina scorpion na panya road. Wazazi wamelega mnooo ktk kutimiza wajibu wao, huo wajibu unaouongelea kabla hamjawanyooshea walimu vidole hebu mjitafakari kwanza nyie kama wazazi. Kwa upande wangu nikidai haki yangu naidai kwa nguvu zooote maana najua wajibu wangu natimiza tena yawezekana zaidi ya nilivyopaswa.
Kweni WAZAZI kwa watoto wenu kabla hajamtafuta mchawi kwanza.
Kuna rafiki yangu yeye linambia mtoto mtukutu shuleni wazazi huwa wanamtetea, alipofika darasa la saba akawa hautaki hata kwenda shule, wazazi kwa kuiogopa serikali kule vijijini huwa mtoto akikataa kuja shule huwa wanaanza na mzazi, sasa mzazi anakwenda kumsemea mtoto wake kwa mwalimu mkuu, eti mwanangu kachana kaptula hataki kuja shule, hivi mimi kama ni mwl. naanza kumchapa na huyu mzazi kama ninammudu kama si mmudu ningemtimua kama kicheche ila kwa busara walimu walimkalisha na kumsaidia Yule mzazi na mtoto akamaliza shule, ila wakampa dongo kaburi ulilochimba uanza kuingia mchimbaji. Poleni walimu, Hivi mkulu halikuwa hawachapi hawa wahuni wa shule?Kwa asiyepitia au kujua kinachotendeka mashuleni, atachukulia simple tu, Ila jamani tunakutana na changamoto za kila aina.
Za aibu, za kufurahisha, za kuhuzunisha yaani ilimradi tu.
Nakumbuka nilipata kesi ya mwanafunzi wa kidato cha 3 aliyeachiwa nyumba na mama yake mzazi, baada ya mama kuhisi ati huyo mwanae wa kike anatembea na baba yake.
Mama alihama kabisa nyumba.
Ilikuwa kazi kumrudisha, ila kwa weledi tuliokuwa nao, tulifanikiwa.
Hivo hawa wanaobeza beza humu, nawaangalia kwa dharau tu mkuu.
Maybe wakitulaumu wanapata relief, so let them be.atoto, mie nimeshamalizana nao.
Mwenye masikio amesikia na mwenye macho ameona ulichomalizia.
TABIA YA MTOTO INAANZIA NYUMBANI.
Hata makanisani tunaambiwa kuwa, tabia mbaya ya mtoto ni urithi aliopewa na wazazi wake.
Wasitegemee tabia ya kurithi itaachika moja kwa moja, itapungua tu na kuisha kidogokidogo, maana hata wahenga walinena, "tabia ni kama ngozi ya mwili, huwezi kuibadili"
Mzazi mfunze mtoto siha na adabu njema tangu utotoni.
Nina imani mtoto mtiifu na anayejua nini amefata shule, huwa hatuhangaiki nae.
Walimu ni ziada, ila mzazi ndie mwenye jukumu la kumuangalia mtoto wake anatenda nini na nini hatendi.
Sisi pia ni wazazi na watoto wetu wanasoma kama wenu tunavyowafundisha ila mbona tuko waelewa tu?
Wapi pagumu?
Aliyekusikia kakusikia, asiyetaka kukabilianana huu ukweli, basi aende sehemu ingine akajiaminishe.
Ila ukweli utabaki pale pale, wazazi kwa % kubwa, wanachangia katika kuwaharibu watoto/vijana wao aidha kitaaluma au kiakili.
Kuna msemo unaosema, "kama rahisi, unda yako utumie, kama ni lesi....ashone yake aivae"Oooh walimu sijui wana matatizo kisa walifeli sijui nini hivi kuna sekta nchi hii haina matatizo? Madaktari wangapi wanaua wagonjwa kwa uzembe? Mara huyu kapasuliwa kichwa badala ya mguu, haujakaa sawa mgonjwa kapelekwa mochwari akiwa hai nk nk. Mainjinia ndio majengo yanatudondokea kila siku, barabara za lami zinaota mimea katikakti ya lami, mikataba ya ovyo ovyo inasainiwa na wanaojiita wanasheria, nk nk nk nk!! Si ndio hawakufeli hao!!!
Wasijifanye wajuaji, kwanza tunajitolea sanaaaa maana kwanza kazi haifanani na maslahi alafu bado mtu anajitia uduwanzi!! Kawe mwalimu nawewe kama inadhani rahisi hivyo.
soothe urself mwalimu njaa. hahahahhaI used article "a" to mean best among many !! you want me use specifer, You know me? Bushbaby eyed hooligan!!!
Kwa kweli, acha tu waendelee kupoza machungu yao.Maybe wakitulaumu wanapata relief, so let them be.
Tumeshapoa.Kuna rafiki yangu yeye linambia mtoto mtukutu shuleni wazazi huwa wanamtetea, alipofika darasa la saba akawa hautaki hata kwenda shule, wazazi kwa kuiogopa serikali kule vijijini huwa mtoto akikataa kuja shule huwa wanaanza na mzazi, sasa mzazi anakwenda kumsemea mtoto wake kwa mwalimu mkuu, eti mwanangu kachana kaptula hataki kuja shule, hivi mimi kama ni mwl. naanza kumchapa na huyu mzazi kama ninammudu kama si mmudu ningemtimua kama kicheche ila kwa busara walimu walimkalisha na kumsaidia Yule mzazi na mtoto akamaliza shule, ila wakampa dongo kaburi ulilochimba uanza kuingia mchimbaji. Poleni walimu, Hivi mkulu halikuwa hawachapi hawa wahuni wa shule?
Leo suala la walimu kila mtu kageuka msemaji na mwanasaikolojia!! Chaaaah! Waje watumie hizo saikolojia zao basi, au wangeanza kuzitumia kwa watoto wao.Kuna msemo unaosema, "kama rahisi, unda yako utumie, kama ni lesi....ashone yake aivae"
Vyuo vya ualimu bado vipo, waende wakasome, waje kufundisha.
Mbona simple tu?
Mbona kila kazi ina madudu?
Washasahau ishu ya makontena bandarini.
Ishu ya Tanesco, sakata la Muhimbili bado kuna hili la askari, ila kwa kuwa wameshashikishwa ukuta kwa wanavyoviamini.
Acha waendelee kuamini.
Ila ukweli tunaujua sisi ambao tuko na hao wanafunzi wao.