Mimi ni Mwalimu, nisome nilivyo

Mimi ni Mwalimu, nisome nilivyo

We unadhani wakati Scorpion akiwa mwanafunzi alikuwaje ? THINK.

'am trying to be ant-scorpion.

Mkuu mi nakubaliana kabisa na hizi adhabu...huu ni upuuzi tunajidai kutetea watoto as if ni mifano bora,mtoto anakosa heshima namna hiyo ashughulikiwe inavyotakiwa...


Bila hizi displine hatuna kizazi hapa,mtoto unabisha mbele ya mwalimu mbele ya darasa?Mwanangu chapeni mpaka tako zichanike akiwa mtu mzima aelewe maana ya heshima ni nini..

Chapeni tu,wehu wakubwa...mitoto imetushinda nyumbani imekua scorpions
 
Teh teh teh teeeeeh!!!
Naona umelauuuuumu walimu, haujaongelea chanzo hata kidogo, kwahiyo hapo bado sana kuelekea huko unakokutaka.
I wish ningeandika kitu fulani sema kitakuwa kirefu sana.

Andika tu binti....inaweza kuwa faida kwa wengine...
 
Halafu naomba niongee jambo moja ambalo naona ndilo mnaona chanzo cha yote.
Unajua bwana sisi ni binadamu kama ninyi, nasi pia tuna mapungufu yetu.

Hivi, mnataka tuwe na mioyo gani ya kuvumilia kejeli hizi mnanzozitoa juu yetu?
Mnadhani tuna mioyo ya chuma au ya mbao?
Mlianza kuongea pumba, tukiwajibu kipumba....ohhh walimu gani hawana maadili!!
Kwahiyo mnachotaka mkiongea pumba, tuwajibu ki-Sista Maria kisa sie walimu?
Hakuna hiyo na wala haitotokea.
Ukija kistaarabu, utajibiwa kistaarabu ila ukija kishari na kinoko, tegemea ushari na unoko.

Mzazi wangu wakati ananilipia ada, wewe ulichagua fani ingine akulipie, iweje leo fani yangu uione ina walakini?
Samahanini, tena ukute wengine nawaheshimu humu, ila ndo heshima itashuka sasa hivi, tumekutana Jf, na tuachane Jf.
Mengine huwa wala hayawahusu na hayawadoboi hata.

Usitegemee toto lako tukutu ambalo umelishindwa nyumbani kwako, likija shule litabadilika haraka, kuna stage za ukuaji wa kiakili na kimwili.
Ila kama limerithi laana zako za ukoo wenu, hata umpeleke akasome IST hatabadilika.

Naomba tusipangiane cha kufanya.
Kama unaona kazi yako ya maana kuliko yangu, anzisha uzi wako wenzako waje kukuchangia.
Nawaambia, mtu aje nimpe viatu vyangu avae hata siku 3 tu, kama hujanirudishia mwenyewe.

Kila kazi na changamoto zake.
Eti "uwe na adabu wakati wa kuongea", nyooooo!!! Wewe kama nani unanipangia?
Unajua nimenunua bando la sh ngapi kuingia humu?
Hata siku moja ushawahi kunirushia vocha hasidi wewe!
Piteni kushoto, wajing.a nyie.
Maisha yangu, kazi yangu na mshahara wangu.
Kwahiyo kaka, dada.....sugua gaga uende kanisani au msikitini mkaswali.

Msitake kujua tulikuwa tunafanya shughuli gani kabla hatujaingia kwenye ualimu.
Mlidhani tulilala tu na kuamka then tukajikuta tuko na kazi hii?
Tumepitia vyuoni kama wewe ulivyopitia.
Tumesomea maadlili na utu, Ila mkileta shombo, mtalinawa tu.
Mxyiuuuuuuu.....!!!!!
 
Sisi waTz ni watu wa kuongozwa na matukio sana.
Toka hii issue imeanza inavyoongelewa ni kana kwamba ndio Mara ya kwanza kutokea
Na haitatokea tena.
Ukaguzi wa shule, vikao vya wazazi na waalim, kamati za shule, school baraza, vikao vya darasa.
Waalim wananyanyaswa sana na wanafunzi/ wazazi, waalim kuwanyanyasa sana wanafunzi, waalim kunyanyaswa na waalim wenzao, maafisa elimu, TSD, waratibu elimu n.k
Na wachangiaji wengi wameonyesha ubinafsi... Kila mmoja anasema angekuwa mwanangu ungenitambua......! " mtoto was mwenzio........"
 
Walimu wamechachamaa kwenye huu uzi
.
Madame b Mtoto wangu anasoma kwenye Shule yako. Jumatatu nakuja twende one to one...tehe
We njoo tu.
Mie mbona sina tatizo na mashemeji na mabinamu zangu?

Sio kuchachamaa, tatizo humu watu wanajigeuza miungu watu, wanataka wanalofanya ndilo lisikilizwe.
Hakuna hiyooooo
 
Sisi waTz ni watu wa kuongozwa na matukio sana.
Toka hii issue imeanza inavyoongelewa ni kana kwamba ndio Mara ya kwanza kutokea
Na haitatokea tena.
Ukaguzi wa shule, vikao vya wazazi na waalim, kamati za shule, school baraza, vikao vya darasa.
Waalim wananyanyaswa sana na wanafunzi/ wazazi, waalim kuwanyanyasa sana wanafunzi, waalim kunyanyaswa na waalim wenzao, maafisa elimu, TSD, waratibu elimu n.k
Na wachangiaji wengi wameonyesha ubinafsi... Kila mmoja anasema angekuwa mwanangu ungenitambua......! " mtoto was mwenzio........"
Yaani changamoto ziko nyingi tu.
Ila hili ndo wamelishikia bendera kama wako kwenye mbio za E-fm
 
We njoo tu.
Mie mbona sina tatizo na mashemeji na mabinamu zangu?

Sio kuchachamaa, tatizo humu watu wanajigeuza miungu watu, wanataka wanalofanya ndilo lisikilizwe.
Hakuna hiyooooo

Uskonde Madam. Kazi mnayofanya kubwa.
Hapa nafikiria unamfundisha Mtoto kutoka Tandale au Tandika, Baba misheni town Mama tia maji tia maji, Kaka teja Mjomba jambazi!!!
 
Tuweke kumbukumbu sawa huyu mwanafunzi yupo kidato cha nne naungana na moghas kwa kufaulu kwakwe haitakuwa rahisi

Leteni jina lake hapa huyo dogo then tukumbushane muda ukifika

Mtoto gan unapigwa vile hata kulia hakuna sijawah kuona aisee pamoja na kuchangiwa na waalimu kibao bado toto halitaki hata kutii lichapwe kawaida huyu mtoto ni mtukutu sana tena naamin sana

Pole mwalimu frank
 
Mtawapiga haohao...mimi bado sijawa na mtoto wa kuja kufundishwa na wendawazimu kama nyie.
Akifikia huko nitampeleka shule za maana atakakofundishwa na sio kupigwa.
hujafa hujaumbika,atakua mwendawazimu kama scorpion.na huko atapigwa tuu maana hakuna namna
 
Wasalaamu wakuu!!

kwanza kabisa napenda kuwa omba mods wasiunganishe huu Uzi licha ya trend tuliyonayo, kwani Mimi ni mwalimu naomba nieleze nilivyo, yes waalimu tulivyo.

Napenda kutoa pole yangu ya dhati kabisa kwa mkuu wa shule kwa yaliyomfika, waalimu waliofikwa na janga na mtoto aliyepatwa.

maisha ya shule yana mengi, nadhani na pia ni hakika kuwa wengi humu tumepita shule ( ndio, hata la saba ni shule), Mimi kama mwalimu na kwa uzoefu wangu niliokaa kazini ningeweza kumwadhibu mtoto kama huyo wa mbeya kwa sababu zifuatazo;
(a) Ameonesha kunigomea mbele ya wanafunzi wenzake.
Kama kawaida hakuna mtu mzima yeyote ambaye anapenda kudhalilishwa mbele ya watoto.
Inatokea mwlm unataka kutoa adhabu kwa mwanafunzi eidha kwa kuwa ana kidemu chake darasani anaamua kuonesha dharau na migomo ya waziwazi. Hapo mi ambacho nafanya ni kupiga kama naua NYOKA ili wenzake wakiona wasijiingize kwenye kosa kama lake kamwe. HII INAITWA HESHIMA KWANZA, KAZI BAADAE.

(b) Mwanafunzi ameletwa Ofisini na Mwalm A ambaye anaonekana mnyonge au mpole hana makuu kwasababu hiyo mwanafunzi anamgomea adhabu eidha ya kupiga magoti au kuchapwa! wanafunzi wa aina hiyo Mimi huwa naomba SUB then naagiza mzigo wa kuni badala ya kupikia nabadili matumizi kwa manufaa ya ofisi.

(c) Nimetoka kwenye ATM nakuta mshahara Wangu umekatwa Tsh 60000 bila maelezo ya msingi, narudi shule nakutana na mtoto aliyeshindikana kwao kajichanganya mbele yangu hapo lazima ni convert tsh 60000 to 60000 sticks of coplar punishment.


Mnaojifanya kutetea humu wengi wenu hii kazi ya ualimu hamuijui au mnadhani kwa vile watoto wenu wanapenda shule, basi mnahisi ni wote dunia nzima.

Hakuna mwalimu kichaa hapa duniani ambaye mtoto hajagomea au kusumbua kupokea adhabu, atapigwa kiasi kile.

wito wngu.

waalimu wenzangu, pesa hatuna bado tunatafutwa kufungwa, unapopiga hakikisha kamera ya simu yako iko ofu.

Mpaka pale wanaotokwa mapovu hapa JF watakapowafunza maadili mema watoto wao na fimbo zitafutika zenyewe.

Kwa ukurya nilionao, ujinga darasani + ukorofi mwanao alionao, ACHUNGE SANA.
Mod delete huu uzi haijandikwa na mwalimu, haifundishi chochote.
Eg unafundisha wapi na shule gani mwalimu? Tukawatoe watoto wetu haraka!
 
Hayo mabadiliko anza nayo wewe kwa kuanza kujifunza kuandika.....
Hujui chochote kuhusu ualimu we kaa celebrities forum tudiscuss mambo ya kina diamond na kiba basi

Eeeeh ngoja na mamboz kiteknolojia za kuwanasa walimu wavivu ziingie kutumika...kitaeleweka tu.
 
Unaonekana huna kazi basi gubu la kiswahili limekukaa!!
ulivyosema walimu hawajui kiingereza nikajua we unajua ! sasa wewe binti na vijiwe vya kahawa wapi na wapi !!

Hahahaaaaaaaa

Mi mkaa kibarazani kusogoa udaku kwa kwenda mbele...shangilia basi.
 
Back
Top Bottom