Mimi ni Mwalimu, nisome nilivyo

Mimi ni Mwalimu, nisome nilivyo

Wasalaamu wakuu!!

kwanza kabisa napenda kuwa omba mods wasiunganishe huu Uzi licha ya trend tuliyonayo, kwani Mimi ni mwalimu naomba nieleze nilivyo, yes waalimu tulivyo.

Napenda kutoa pole yangu ya dhati kabisa kwa mkuu wa shule kwa yaliyomfika, waalimu waliofikwa na janga na mtoto aliyepatwa.

maisha ya shule yana mengi, nadhani na pia ni hakika kuwa wengi humu tumepita shule ( ndio, hata la saba ni shule), Mimi kama mwalimu na kwa uzoefu wangu niliokaa kazini ningeweza kumwadhibu mtoto kama huyo wa mbeya kwa sababu zifuatazo;
(a) Ameonesha kunigomea mbele ya wanafunzi wenzake.
Kama kawaida hakuna mtu mzima yeyote ambaye anapenda kudhalilishwa mbele ya watoto.
Inatokea mwlm unataka kutoa adhabu kwa mwanafunzi eidha kwa kuwa ana kidemu chake darasani anaamua kuonesha dharau na migomo ya waziwazi. Hapo mi ambacho nafanya ni kupiga kama naua NYOKA ili wenzake wakiona wasijiingize kwenye kosa kama lake kamwe. HII INAITWA HESHIMA KWANZA, KAZI BAADAE.

(b) Mwanafunzi ameletwa Ofisini na Mwalm A ambaye anaonekana mnyonge au mpole hana makuu kwasababu hiyo mwanafunzi anamgomea adhabu eidha ya kupiga magoti au kuchapwa! wanafunzi wa aina hiyo Mimi huwa naomba SUB then naagiza mzigo wa kuni badala ya kupikia nabadili matumizi kwa manufaa ya ofisi.

(c) Nimetoka kwenye ATM nakuta mshahara Wangu umekatwa Tsh 60000 bila maelezo ya msingi, narudi shule nakutana na mtoto aliyeshindikana kwao kajichanganya mbele yangu hapo lazima ni convert tsh 60000 to 60000 sticks of coplar punishment.

Mnaojifanya kutetea humu wengi wenu hii kazi ya ualimu hamuijui au mnadhani kwa vile watoto wenu wanapenda shule, basi mnahisi ni wote dunia nzima.

Hakuna mwalimu kichaa hapa duniani ambaye mtoto hajagomea au kusumbua kupokea adhabu, atapigwa kiasi kile.

wito wngu.

waalimu wenzangu, pesa hatuna bado tunatafutwa kufungwa, unapopiga hakikisha kamera ya simu yako iko ofu.

Mpaka pale wanaotokwa mapovu hapa JF watakapowafunza maadili mema watoto wao na fimbo zitafutika zenyewe.

Kwa ukurya nilionao, ujinga darasani + ukorofi mwanao alionao, ACHUNGE SANA.
Wewe ndiyo umetoa povu sasa!

Pole sana na masaibu yako/yenu

Wezi wako wengi ila anaekamatwa ndiye zimefika 40 zake.

Hapo unasemea kesi ya kupigwa kwa mtoto, subiri iishe halafu na wewe/ninyi/au mhusika achukue hatua anazoona zinafaa, hata akihukumiwa adhabu Rufaa ni haki yake!

Hakuna sababu ya kujiuguza magonjwa ya kutokwa povu hapa JF.
 
Tulipomaliza masomo waliofeli wote ndio wakaenda ualimu sasa sijui unaongea nini? By the way walimu walionifundisha mimi wengi wao walikuwa timamu, hawakuwa na akili kama zako. Na nikikutana nao mpaka kesho wanakula lager za kutosha kisha wanaondoka na nauli ya taxi.
Waliofeli wote eti!!
Unatukanaaaa alafu mwisho wa siku hao hao waliofeli ndio unawapelekea wanao wakufundishie!! Au unawafundisha mwenyewe?
 
Matokeo ya mwaka jana, Serikali Ilitukalia kooni.
Walitaka tufanyaje na kizazi chenyewe kama cha akina Frank?
Hapo kwenye matokeo ndipo wananikeraga hatari, mitoto yenyewe inakuja sekondari haijui hata kusoma kiswahili tu achilia mbali kiingereza, alafu wanatarajia walimu watende miujiza.
Matokeo yakiwa mazuri ni ya serikali yakiwa mabaya eti ni ya walimu, hovyo kweli.
 
Au wanadhani kuonekana katika runinga wakizindua aina mpya za simu za smartphone ni ujanja?
Mawaziri wa kizazi kipya wanaosubiri taarifa toka smartphone?
Waje huku vituoni
Hata wakija hawana la maana, utasikia 'walimu tunajua hali ni ngumu ila mjitahidi tu,tena kuna watu wanatamani hata hizo nafasi mlizonazo'
Yaani bora wabakie huko huko kuliko kuja kuchafuana.
 
Mwalimu Evelyn Salt mwalimu atoto na mwalimu madam d mumenifurahisha sana mlivyofunguka,yaani toka Jana nikiangalia watu wajinga wanavyotukana walimu humu hasira zilinizidi nguvu,watanzania ni wanafki sana,yaani eti wanaona yule kibaka ndo amepigwa vile,walimu wakilalamika hakuna anayewatetea,ila walimu wakionekana wamekosea hayo matusi yake ni balaa,KWA JINSI MLIVYONIFURAHISHA NJOO HAPA CITY PUB MBEYA MPATE KAKOKA BARIIIIDI EEEEH.
 
Hahaaaa!! Ngoja nicheki kama panga boy inakuja huko nije fasta.
Watanzania sisi ni wanafiki kweli, hatuangalii the big picture tumeshupalia matokeo tuu hatuangalii chanzo!!
 
Mi enzi zangu mwalimu akinipiga kibao bila sababu ya msingi namrudishia kwani hakuna sheria inayosema nipigwe vibao,hata wakinipa mkongoto sijali mradi hata mimi nimemzaba kimoja,liwalo na liwe kuna walimu wanatafutaga sifa za kuitwa wakali au wachapaji wazuri,lazima tuheshimiane.
 
QUOTE="moghasa, post: 17953852, member: 141630"]mi sio Mywether kupigana ngumi za show off !! ukileta ujinga hata dawati inakuwa nyenzo believe me!! na ndo maana sijawai kupingwa!

Kila kazi ina changamoto, kama kweli ualimu ni wito kwako kwa nini una dhana ya ukatili kiasi hiki kwa wanafunzi? A Best teacher ever in doing what? Corporal/Capital punishment or molesting girls?
 
Waliofeli wote eti!!
Unatukanaaaa alafu mwisho wa siku hao hao waliofeli ndio unawapelekea wanao wakufundishie!! Au unawafundisha mwenyewe?

Mkuu hyo shule yako noma maana hayo matukio yote dah poleni sana

Wakati nipo std 6 jamaa mmoja huyo alimgomea ticha kumchapa,ticha kampeleka ofisini ile kufika kwa ofisi jamaa akaona ampige ticha mbele ya staff it was worst aisee baadae alitokea ticha mmoja akatoa kampani yule mwana akapigwa sana mpaka midamu kibao halafu wakamfukuza shule

Baada ka ya mwez walimrudisha akamalizia la saba akaingia mtaani akaendeleza harakati zake

Naamin sometime ticha ni mtu kama wewe unavyoweza kuwa na hasira na yeye pia kwake ipo hivyo sasa anatokea mtoto eti sijui mnatetea ni balehe manina hata mimi namkamua kisawasawa
 
QUOTE="moghasa, post: 17953852, member: 141630"]mi sio Mywether kupigana ngumi za show off !! ukileta ujinga hata dawati inakuwa nyenzo believe me!! na ndo maana sijawai kupingwa!!
Kila kazi ina changamoto, kama kweli ualimu ni wito kwako kwa nini una dhana ya ukatili kiasi hiki kwa wanafunzi? A Best teacher ever in doing what? Capital punishment or molesting girls?[/QUOTE]
Ualimu ni ajira, wito aliondoka nao mwalimu nyerere.
Msitunyanyase na huo wimbo wa 'wito'mshindwe malezi alafu mje msingizie wito, hata sisi ni binadamu.
 
Kila kazi ina changamoto, kama kweli ualimu ni wito kwako kwa nini una dhana ya ukatili kiasi hiki kwa wanafunzi? A Best teacher ever in doing what? Capital punishment or molesting girls?
Ualimu ni ajira, wito aliondoka nao mwalimu nyerere.
Msitunyanyase na huo wimbo wa 'wito'mshindwe malezi alafu mje msingizie wito, hata sisi ni binadamu.[/QUOTE]
Mrudisheni mtoto kwa huyo mzazi aliyeshindwa kumpa malezi, kuliko kumtia kilema au pengine kuua, na wewe kupoteza ajira na maisha yako.
 
Mkuu hyo shule yako noma maana hayo matukio yote dah poleni sana

Wakati nipo std 6 jamaa mmoja huyo alimgomea ticha kumchapa,ticha kampeleka ofisini ile kufika kwa ofisi jamaa akaona ampige ticha mbele ya staff it was worst aisee baadae alitokea ticha mmoja akatoa kampani yule mwana akapigwa sana mpaka midamu kibao halafu wakamfukuza shule

Baada ka ya mwez walimrudisha akamalizia la saba akaingia mtaani akaendeleza harakati zake

Naamin sometime ticha ni mtu kama wewe unavyoweza kuwa na hasira na yeye pia kwake ipo hivyo sasa anatokea mtoto eti sijui mnatetea ni balehe manina hata mimi namkamua kisawasawa
Unajua kama jambo haujakutana nalo ni rahisi sana kuongea, ni kama uwanjani tu mtazamaji ni rahisi kusema 'sasa pale kashindwa vipi kufunga goli?' Akiingia yeye hata mpira hatougusa.

So acha waongee tu maana hawakuanza leo, tunatukanwa hadi na wasiosoma kabisa, ila wht mataz kazi tunaendelea kufanya, wao wasimamie nafasi zao kama wazazi alafu waone kama kutakuwa na tatizo.
 
Ni heri primary unakua unapigiwa kelele na watoto, kuliko hizi ngedere ambazo zikiota vooz zinajiona zimekua, yani mtoto anakudindia utadhani anakupandaga shwain
Kama wanadhani kulea adolescents ni rahisi mbona wao wanawashindwa! Mtu anashupaa kabisa eti 'ningemchukulia ni mtoto anaekuwa'
Thubutuuuu, rahisi sana kuongea, yakikukuta mbona utajitafuta.
 
Ualimu ni ajira, wito aliondoka nao mwalimu nyerere.
Msitunyanyase na huo wimbo wa 'wito'mshindwe malezi alafu mje msingizie wito, hata sisi ni binadamu.
Mrudisheni mtoto kwa huyo mzazi aliyeshindwa kumpa malezi, kuliko kumtia kilema au pengine kuua, na wewe kupoteza ajira na maisha yako.[/QUOTE]
If it was just easy like that unadhani hayo yote yangetokea?
 
Back
Top Bottom