Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?

Sijaisoma maandishi yako. Roho mtakatifu kaniongoza nikuambie oaneni tu kwa sababu wote mnaamini ktk kristu
 
mimi niongelee juu ya swali Zima la imani. Ninavyofaham mimi wokovu una misingi yake miiko yake. kwani wewe una miaka mingapi katika wokovu? kitu kilicho mfanya Mfalme Suleimani kukosana na Mungu ni pale alipooa wanawake wa mataifa mengine hao walikuwa wakiamini miungu mingine( imani tofauti na suleimani). Maandiko pia yanasema usifungiwe nira pamoja na wasioamini! wewe waamini wokovu yeye je? vipi siku moja akikwambia unanipigia makele ya kuomba mimi nimelala utajisikiaje? siku akija na bia home utasemaje? maana wakatoliki wanakunywa! uamzi ndugu unabaki kwako wewe mwenyewe maana yeye hatakuwa na shida hata kidogo ila wewe! hata hivyo wahenga walisema ndege wa rangi moja huruka pamoja! nawakilisha!

Hapo kwenye red.....

Huu ndo ushetani nambario moja...Huyu Yesu ninaye muabudu hakuna mahali ansema nisifungamane na wasio amini...Hivi nikuulize swali wewe mwana mtoka kuzimu Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi au watu wote...? Je Yesu alifungamamana na watu gani...Wema au waouvu....Wewe ndo ibilisi nambari moja na Mfarisayo ambaye Yesu alipata shida sana na nyiynyi watu...

Halafu huo mstari ulio u-quote nafikiri unapatikana kwenye kitabu cha Waroma....Sasa kabla ya kuonesha upumbavu wako jaribu kupitia hya mambo yafuatayo...
.Waroma walikuwa waatu gani....?
Kwaninin Mt. Paulo aliwandikia barua hiyo Waroma...
Jiografia ya Waroma katika kipindi hicho....


Usisome Biblia kwa kukurupuka ndugu HAo Wachungaji wenu makanjaja wamewajaza sumu....
 
... lakini namwona ni mwanamke mnyenyekevu sana kuliko wengi niliokutana nao makanisani
Una maana wasichana wa Efatha sio wanyenyekevu kama huyu Mkatoliki? Basi ondoka huko kwa wasio wanyenyekevu uanze kusali Roman Catholic church kwa wanyenyekevu
 
...wewe uko tayari kubadili dini na kusali ROMA ama wataka yeye awe kondoo wa Mwingira?

hii dini huwa siilewi .RC..EFATHA..MLIMA WA MOTO..MZEE WA UPAKO..ANGLIKANA na madhehebu mengine HAWA WOTE NI DINI GANI?
 
Kwahiyo ujui kuwa roma ndiyo kanisa kristu aliloacha? Ujui kuwa roma ndiyo ukristu wa kweli? Achana na conspiracy theories , tena fanya research juu ya catholic church...nenda catholic.com, whyimcatholic.com utapata majibu juu ya imani ya kikatoliki na siyo mataptap ya wasabato na wapteotestanti aka waasi...

nilizani RC imeelezewa ndani ya biblia
 
Walokole tu ndio mlio safi? Mfundishe na yeye kuishi maisha ya kitakatifu kama unayoishi wewe then weka ndani.
 
Aiseh! Hawa Digitali wana story za kusisimua jamvini. Hadi raha!!:focus::focus::focus::focus::focus::focus: . Tatizo Dini, mfanye zoezi la kusali kila siku ya kuabudu, uone commitment.
 
Watu wengi wakiwemo wakatoliki wanakosea sana..Wanadhani ukarismatic ni aina fulani ya upentekoste au ulokole ndani ya kanisa..na wamefikia kuact kama vichaa wa kilokole na kipentekoste..charismatic siyo na wala haifanani hata kidogo na heresy kama za kilokole na waprotestanti

wewe unasali wapi
 
ukristu ni ukristu tuuu, ulokole jina, au dhehbu Yesu ni yesu, mbona unahangaika weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
hatujaongea hilo kwa undani,ila yupo tayari kwenda na mimi efatha

Ee bhana ee.....kazi ni kwako, kusuka au kunyoa inategemea akili yako kwani wewe ndie unayemjua kuliko sisi.

Funga na uombe kwa siku 7 jibu utapata
 
Hivi walokole tu ndo wameokoka? naomba msaada kujua hili.
 
epatha nini?au ni miungu flan hiv wakatolik wanakatazwa kuabudu miungu
 
Mkristo mchanga!!!
Kumuoa mtu wa nje ya imani yako ni upungufu mkubwa wa kushindwa kuhimili mikiki ya shetani na maanisha shetani anakuwa amekutawala hadi kumfikilia huyo mtu!
Kama si kanisa unalo amini wewe akibadili dini na kuja kwako kwa akili yako unafikiri amefuata dini au wewe? na kama kakuona wewe ni zaidi ya Mungu wake aliyekuwa anamwabudu unafikiri wewe anashindwa kukusaliti? au unadhani huyo Mungu wako anashindwa kumsaliti? Usiishi kwa kumtegemea mwanadamu bali bwana aliye juu mbinguni, katika jina la Yesu naomba huyo pepo mchafu aliyeyatawala mawazo yako aondoke sema Ameni!!!!!!!!!
Usimuoe shinda tamaa zako za kimwili mrejee mwokozi wako na tubu kwa kuweka hisia nje ya maandiko unayo yaamini usijilinganishe na Muumba wako yaani dunia nzima umetafuta wa imani yako umekosa?
 
Kuokoka si dini ni kuikana dhambi na kumkiri Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, na kuishi maisha ya utakatifu. Yaani kuwa ndani ya Yesu. Mambo mengine yasikutatize. Ishi Kristo tu. Ila inabidi usome neno sana na umwombe Roho Mtakatifu akufafanulie ili usije ukakengeuka!! Period!
Hivi walokole tu ndo wameokoka? naomba msaada kujua hili.
 
Ulokole ni dhana..naoma ujiulize maswali haya je ulipomwona kwa mara ya kwanza uliona dini yake au? Na pia unataka kuoa mtu au dini yake? Is your relationship emotional or physical?
 
Ulokole ni dhana..naoma ujiulize maswali haya je ulipomwona kwa mara ya kwanza uliona dini yake au? Na pia unataka kuoa mtu au dini yake? Is your relationship emotional or physical?

Haya ni maswali yanayoenenda kwa hekima ya kibinadamu na kumweka Mungu kando. Majuto ni mjukuu.
 
Haya ni maswali yanayoenenda kwa hekima ya kibinadamu na kumweka Mungu kando. Majuto ni mjukuu.

Hekima ya Mungu ni ubaguzi maana fulani hasali sehemu fulani...Maajabu haya....Hebu niambie Yesu(Mungu) hatukumchagua sisi ila yeye alituchagua sisi bila ubaguzi, je alikuja duniani kwa ajili ya watu fulani...?

Ubaguzi ndo Yesu alituachia... ?....Kweli sasa nimeamini Upendo wa Agape ullikuwa kwa Yesu pekee.....
Una-propagate dhambi ya ubaguzi kwa kisingizio cha kuongozwa na Roho...

Pathetic Fool..
 
Pole bosi wangu hilo jina lokole mnajiita tu liko sawa na kama wajiitao ccm ,twanga pepeta,tmk,ngwasuma etc.hebu tafuta njia sahihi upate pepo ya mwenyezi mungu (acha kuidhulumu nafsi yako bro)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom