Bila shaka asilimia kubwa hapa mnatambua tabia za introvert, hizo tabia zimepelekea jamii inayo nizunguka kuniona ni mtu wa ajabu sana. Huenda ni sababu ya wao kukosa uelewa kuhusu watu walio katika kundi la Introvert. Hizi ni baadhi ya tabia zinazo wafanya wanione mtu wa tofauti sana kulinganisha na wao.
Sipendi kuchangamana na watu, yaani napenda niwe peke yangu mimi kama mimi. Na muda mwingi niko bize na simu yangu nikiperuzi JamiiForums, sijawahi kutumia Facebook, Instagram wala Twitter. Ata hii JamiiForums nilijiunga baada ya mara kwa mara kila nikisachi kule Google lazima itokee kwahiyo nikaona bora nijiunge. Kwahiyo mara nyingi niko na simu nikichoka kuperezu nachukua kitabu najisomea kwaajili ya kuongeza maarifa. Nasoma vitabu vilivyo andikwa na waandishi kama Robert Greene, Eric Jorgenson, James Clear, Daniel Carnegie, Robin Sharma, Robert Kiyosaki, Morgan Housel. Kwahiyo mara nyingi niko bize na kitabu sitaki kuwa karibu na watu kabisa.
Jambo linaweza tokea mtaani nawala nisiwe na habari nalo mi niko bize na mambo yangu. Mfano anaweza kuja mtu mashuhuri watu wakajazana kwenda kumuona lakini mimi sina huo upumbavu.
Ni mtu mkimya sana sina shobo na mtu na sitaki mazoea na mtu, niko bize na mambo yangu. Ata jirani yangu sijui anaitwa nani wala anajishughulisha na nini.
Siendi kwenye sherehe yoyote ile wala sihudhulii kwenye msiba wowote ule, kifupi sipendi kujichanganya na watu napenda niwe peke yangu nikitafakari mambo muhimu.
Najiamini na kujikubali sana, hii hali imepelekea jamii kuniona mtu mwenye dharau kwao. Hii sio sawa ila ndio njisi nilivyo. Tabia zinazo wafanya wanione tofauti ni nyingi sana hizo ni baadhi tu.
Je mwana introvert mwenzangu unapitia changamoto zipi katika jamii inayo kuzunguka.