Mimi ni Introvert, jamii inanichukulia tofauti sana

Mimi ni Introvert, jamii inanichukulia tofauti sana

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,189
Reaction score
5,821
Bila shaka asilimia kubwa hapa mnatambua tabia za introvert, hizo tabia zimepelekea jamii inayo nizunguka kuniona ni mtu wa ajabu sana. Huenda ni sababu ya wao kukosa uelewa kuhusu watu walio katika kundi la Introvert. Hizi ni baadhi ya tabia zinazo wafanya wanione mtu wa tofauti sana kulinganisha na wao.

Sipendi kuchangamana na watu, yaani napenda niwe peke yangu mimi kama mimi. Na muda mwingi niko bize na simu yangu nikiperuzi JamiiForums, sijawahi kutumia Facebook, Instagram wala Twitter. Ata hii JamiiForums nilijiunga baada ya mara kwa mara kila nikisachi kule Google lazima itokee kwahiyo nikaona bora nijiunge. Kwahiyo mara nyingi niko na simu nikichoka kuperezu nachukua kitabu najisomea kwaajili ya kuongeza maarifa. Nasoma vitabu vilivyo andikwa na waandishi kama Robert Greene, Eric Jorgenson, James Clear, Daniel Carnegie, Robin Sharma, Robert Kiyosaki, Morgan Housel. Kwahiyo mara nyingi niko bize na kitabu sitaki kuwa karibu na watu kabisa.

Jambo linaweza tokea mtaani nawala nisiwe na habari nalo mi niko bize na mambo yangu. Mfano anaweza kuja mtu mashuhuri watu wakajazana kwenda kumuona lakini mimi sina huo upumbavu.

Ni mtu mkimya sana sina shobo na mtu na sitaki mazoea na mtu, niko bize na mambo yangu. Ata jirani yangu sijui anaitwa nani wala anajishughulisha na nini.

Siendi kwenye sherehe yoyote ile wala sihudhulii kwenye msiba wowote ule, kifupi sipendi kujichanganya na watu napenda niwe peke yangu nikitafakari mambo muhimu.

Najiamini na kujikubali sana, hii hali imepelekea jamii kuniona mtu mwenye dharau kwao. Hii sio sawa ila ndio njisi nilivyo. Tabia zinazo wafanya wanione tofauti ni nyingi sana hizo ni baadhi tu.

Je mwana introvert mwenzangu unapitia changamoto zipi katika jamii inayo kuzunguka.
 
Kuna vitu sio vyakujisifu kabisa! Ati ahuzulii misiba mara akija mtu mashuhuri huendi kwani hauna huo upumbavu!..

Mi nafikiri Kuna tatizo kwenye ubongo wako ukikua utajua umuhimu wa kuchangamana na jamii.

Kwa mtu mwenye akili timamu hivi vitu lazima viwe balance upo upande wa mambo yako na upande wa jamii,Kama unajiona wewe ni Bora Sana kaishi msituni huko!.

Mnapokuwa mkuwe na akili sio mnakuwa miili tu.
 
Hutu tu maneno maneno twa kizungu tumeleta matatizo sana siku hizi, maana kila mwenye kitabia chake cha ajabu anakitafutia jina la kizungu.

Kuna ubinafsi, uchoyo na kujiona bora kuliko wengine utasikia 'introvert.

Mcharuko, kuongea bila ya break, kila kitu kujua wewe, utasikia 'extrovert.

Jitu linabadilisha mahusiano kama nguo. Analalana ovyo na kila mtu, utasikia 'outgoing'.

Jitu halijielewi leo analala na mwanaume kesho mwanamke kesho kutwa mnyama utasikia 'bisexual'.

All in all uzungu umetuletea maneno ya kuhalalisha upumbavu kwa majina mazuri mazuri. Enzi za mababu zetu hutukusikia ujinga huu.

Wewe mtoa mada ni limbukeni wa maisha hakuna cha introvert wala nini. Subiri siku likutokee tatizo halafu uone kina Robert Greene waje kukusaidia.

Kila binadamu haijalishi uwezo wake wa kiuchumi anahitaji watu wengine kwa njia moja au nyingine.

Kuna baadhi ya mambo kwenye jamii yanaweza tatuliwa na watu wengine tu na si pesa yako wala kazi yako, mathalan kupatwa na janga la moto ghafla, sasa wewe na kujiona huna upuuzi wa kujichanganya unaweza jikuta umekuwa ndafu watu wakikuangalia tu.
 
Mimi ni introvert........ila Kuna line nyembamba sana kati ya Introvert na arrogant au Pride lakini mkuu una Pride na arrogance

Mimi najitenga sababu najikuta sina story nakua bored haraka...Lakini haninyimi kushiriki kwenye event za kijamii huwa Kuna parts hata kufanya usafi na barakoa yangu au kwenda kunawisha watu maji

Nasoma vitabu sana lakini pia Nina Marafiki wachache naopata muda naongea nao....Nina mawazo makubwa ila kilicho akilini nakiwakilisha vizuri kwa kuandika kuliko kuzungumza

Nimekuwa nikipitia Changamoto Kazini wengi uniona Nina Pride na classes za watu naozungumza nao Sasa sababu sio wakwenda huku na huku kujitetea wengi wanaamini hvyo ingawa wachache wamenielewa

What i see mkuu unalelea muonekano wa Kiburi na arrogance Haitakiwi kuwa hivyo
 
Bila shaka asilimia kubwa hapa mnatambua tabia za introvert, hizo tabia zimepelekea jamii inayo nizunguka kuniona ni mtu wa ajabu sana. Huenda ni sababu ya wao kukosa uelewa kuhusu watu walio katika kundi la Introvert. Hizi ni baadhi ya tabia zinazo wafanya wanione mtu wa tofauti sana kulinganisha na wao.

Sipendi kuchangamana na watu, yaani napenda niwe peke yangu mimi kama mimi. Na muda mwingi niko bize na simu yangu nikiperuzi JamiiForums, sijawahi kutumia Facebook, Instagram wala Twitter. Ata hii JamiiForums nilijiunga baada ya mara kwa mara kila nikisachi kule Google lazima itokee kwahiyo nikaona bora nijiunge. Kwahiyo mara nyingi niko na simu nikichoka kuperezu nachukua kitabu najisomea kwaajili ya kuongeza maarifa. Nasoma vitabu vilivyo andikwa na waandishi kama Robert Greene, Eric Jorgenson, James Clear, Daniel Carnegie, Robin Sharma, Robert Kiyosaki, Morgan Housel. Kwahiyo mara nyingi niko bize na kitabu sitaki kuwa karibu na watu kabisa.

Jambo linaweza tokea mtaani nawala nisiwe na habari nalo mi niko bize na mambo yangu. Mfano anaweza kuja mtu mashuhuri watu wakajazana kwenda kumuona lakini mimi sina huo upumbavu.

Ni mtu mkimya sana sina shobo na mtu na sitaki mazoea na mtu, niko bize na mambo yangu. Ata jirani yangu sijui anaitwa nani wala anajishughulisha na nini.

Siendi kwenye sherehe yoyote ile wala sihudhulii kwenye msiba wowote ule, kifupi sipendi kujichanganya na watu napenda niwe peke yangu nikitafakari mambo muhimu.

Najiamini na kujikubali sana, hii hali imepelekea jamii kuniona mtu mwenye dharau kwao. Hii sio sawa ila ndio njisi nilivyo. Tabia zinazo wafanya wanione tofauti ni nyingi sana hizo ni baadhi tu.

Je mwana introvert mwenzangu unapitia changamoto zipi katika jamii inayo kuzunguka.
Introvert sio sifa nzuri sana ,pia wako kwenye risk kubwa ya kujiua hivyo jitahidi kujichanganya
 
Hutu tu maneno maneno twa kizungu tumeleta matatizo sana siku hizi, manaa kila mwenye kitabia chake cha ajabu anakitafutia jina la kizungu.

Kuna ubinafsi, uchoyo na kujiona bora kuliko wengine utasikia 'introvert.

Mcharuko, kuongea bila ya break, kila kitu kujua wewe, utasikia 'extrovert.

Jitu linabadilisha mahusiano kama nguo. Analalana ovyo na kila mtu, utasikia 'outgoing'.

Jitu halijielewi leo analala na mwanaume kesho mwanamke kesho kutwa mnyama utasikia 'bisexual'.

All in all uzungu umetuletea maneno ya kuhalalisha upumbavu kwa majina mazuri mazuri. Enzi za mababu hutukusikia ujinga huu.

Wewe mtoa mada ni limbukeni wa maisha hakuna cha introvert wala nini. Subiri siku likutokee tatizo halafu uone kina Robert Greene waje kukusaidia. Kila binadamu haijalishi uwezo wake wa kiuchumi anahitaji watu wengine kwa njia moja au nyingine. Kuna baadhi ya mambo kwenye jamii yanaweza tatuliwa na watu wengine tu na si pesa yako wala kazi yako, mathalan kupatwa na janga la moto ghafla, sasa wewe na kujiona huna upuuzi wa kujichanganya unaweza jikuta umekuwa ndafu watu wakikuangalia tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mpe vidonge vyake huyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom