Mimi na wewe huenda tumeshakula sana Vibudu tukifikiri ni Kuku, Tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Inasikitisha sana, hapo zamani ilizoeleka vibudu vya kuku vilikuwa kwajili ya kulishia nguruwe ila sikuhizi mimi na / au wewe huenda tumelishwa sana tukidhani ni kuku tena tukijisifu ni bei rafiki kwa mtanzania.

Ngoja niwasanue wananchi wenzangu

Kwa case study tutachukuloa eneo la Bagamoyo (Mapinga, Kerege, Kiaraka), maeeneo yenye miradi ya ufugaji wakuku

Kuna makundi ya wakina mama na vijana wamebeba ndoo alfajiri wakitokea mashambani kati ya saa moja hadi tatu asubuhi au jioni kuanzia saa 12 hadi 2 usiku.

Mwanzo waweza kudhani wanaenda kununua maziwa katika nashamba ya watu kisha wanayaleta mjini kwa ajili ya biashara, Kumbe baadhi yao zile ndoo zina kuku waliokufa mabandani sasa wanaletwa mjini kwa ajili ya biashara

Ni hivi.., ukiwa mfugaji wa kuku wa nyama wengi (1000, 5000 hadi 10,000) ni kawaida sana kuingia bandani na kukuta kuku 5, 10 , 20, 30 hadi 50 wamekufa asubuhi au Jioni

Sasa utaratibu ni kwamba vijana wa kazi hawaruhusiwi kuwatupa mpaka bosi au meneja aje awashuhudie, awahesabu na kisha asimamie zoezi la kuwafukia kuku waliokufa, Sasa kumbe pale wanapofukiwa kuku waliokufa na bosi akiondoka tu, nyuma yake ndiyo wanaingia wale wamama wenye ndoo, wanauziwa wale kuku waliokufa Tsh 1,000 kwa kila kuku mmoja

Ni fursa nyeusi yenye faida kubwa sana hasa wakipelekwa mjini, kuku wa buku akikatwa katwa vipande faida inaweza kuwa zaidi ya mara na ndio maana hata bei huwa chee sana kiasi cha kustusha

Wenyewe wanasema ukishaweka kitunguu swaumu na tangawizi kujua kuku huyo alikuwa kibudu ni mpaka muuzaji akutonye la sivyo huwezi kujua

Mimi au wewe huenda tumeshakula Vibudu tukifikiri ni Kuku,Tuongeze umakini katika kuchagua na Kununua Kuku.

1694111344631.png
 
Vibudu vyenyewe huenda vimekufa kwa magonjwa kama mdonde na gideri kuku hufa sana, uaminifu hakuna nani ale hasara?
 
 
Back
Top Bottom