Bei ya kuku wa kienyeji imekuwa juu sana

MKIBAIGWA

JF-Expert Member
May 25, 2017
520
1,203
Kuna jamaangu mmoja yupo Dar juzikati akaniuliza kuhusu bei ya kuku Dodoma.nikamwambia sijui mana mm nipo mjini ngoja niulizie watu wa vijijini.

Nilivyouliza watu wa vijijini wakaniambia kuku mkubwa kabisa Tsh 7000 hadi 8000. Jamaa akaniomba nikamnunulie kuku 200 nikasema ngoja niende nikajifunze biashara ya kuku,Leo nimeenda mnadani na bodaboda nikakuta kuku bei juu kweli wanaaanzia 12000 jogoo mkubwa kabisa na kuku wa wastani 8000.

Nikaishia kununua kuku 100 Kwa wastani wa 9800 waliobaki nitaenda kununua kesho mnada mwingine. Wameniambia kuku huwa wanakuwa bei chee sana kuanzia mwezi wa 11.

Ila fursa zingine nilizoziona ni ununuzi wa mbuzi na ng'ombe wamasai wanapiga hela sana unakuta Dogo hana hata suruali anauza madume 20 ya ng'ombe.

IMG_20210605_125258_146.jpg
IMG_20210605_095953_032.jpg
IMG_20210605_081012_203.jpg
IMG_20210605_122747_522.jpg
IMG_20210605_094535_222.jpg
IMG_20210605_080954_035.jpg
IMG_20210605_095939_519.jpg
IMG_20210605_110436_000.jpg
IMG_20210605_110440_514.jpg
 
Hapo wastani wanakufa wangapi kabla hawajafika sokoni na unategemea huko sokoni uwauze kwa bei gani na kwa muda gani?

Angalia huyo jamaa yako wa Dar asikulaze mlango wazi....
 
Mnanunua kuku wa kienyeji 7000 - 12,000? Uku kwetu visiwani wa kienyeji alieshiba anaanzia 20,000 hao wa buku 7 huwa wale reject wa Europe na uturuki na ile mikuku ilojazwa upepo kutoka Brazil
Mkuu kama hawa niliowabeba sh ngapi huko kwenu????
IMG_20210605_125258_146.jpg
 
Kuna jamaangu mmoja yupo Dar juzikati akaniuliza kuhusu bei ya kuku Dodoma.nikamwambia sijui mana mm nipo mjini ngoja niulizie watu wa vijijini.

Nilivyouliza watu wa vijijini wakaniambia kuku mkubwa kabisa Tsh 7000 hadi 8000.

Jamaa akaniomba nikamnunulie kuku 200 nikasema ngoja niende nikajifunze biashara ya kuku,Leo nimeenda mnadani na bodaboda nikakuta kuku bei juu kweli wanaaanzia 12000 jogoo mkubwa kabisa na kuku wa wastani 8000.

Nikaishia kununua kuku 100 Kwa wastani wa 9800 waliobaki nitaenda kununua kesho mnada mwingine.
Wameniambia kuku huwa wanakuwa bei chee sana kuanzia mwezi wa 11.

Ila fursa zingine nilizoziona ni ununuzi wa mbuzi na ng'ombe wamasai wanapiga hela sana unakuta Dogo hana hata suruali anauza madume 20 ya ng'ombe.

View attachment 1809341View attachment 1809342View attachment 1809343View attachment 1809344View attachment 1809345View attachment 1809346View attachment 1809347View attachment 1809348View attachment 1809349
Naona SOKO LA WANYONGE lipo poa kabisa wakati MABEBERU wakifanya shopping MLIMANI CITY KWENYE AC, na hao mabeberu nyie ndio mnawapa kura.

Ipande tu, kwanza hiyo ulonunulia ni ndogo, wanyaturu wapandishe tu maana huko mjininmnakula hela sana.
1.jpg
11.jpeg
 
Back
Top Bottom