Mimba za kutegeshea zinavyoharibu maendeleo.

Habarini za Juma pili wana JF.
Leo napenda kuwasilisha juu ya hili la wadada wanapokua na long time relationship. Mara nyingi huwa wanashauriana eti ukitaka flani akuoe we mzalie mtoto. Utakuta saa nyingine ndio umepanga utamwoa lakini baada either kujiendeleza kimasomo ili uongeze kipato ama kufikia hatua flani ya maendeleo. Sasa baada ya kutegeshewa basi tena hapo kidume huez kufikiria maendeleo ambayo umejiwekea zaidi ya kujiandaa na majukumu ya malezi. Hivi wadada mnajua ni jinsi gani inavyouma kwa mwanaume ukimtegeshea mimba?

Hivi wanategeshaje, au wanaweka sumaku kwa kule !!! :confused:
 
wababa wa hivyo wapo wengi sana,
mimi nina mfano wa mtu wa karibu kabisa ambaye pia baba alimkataa na alikuwa na watoto wengine kwa huyo mke wake. basi mtoto akajilea mwenyewe kuhangaika kusoma, wale ambao alikuwa nao akiwahangaikia hakuna hata aliyemaliza form four, na baba alikuwa na uwezo balaa. sasa huyu mwenzangu mimi ni boss mkubwa sana...... useme na huyo mtu ana roho ya kusamehe sana, sasa anamuhudumia babake na mkewe na watoto na wajukuu zao, lol!

huyu amebarikiwa na moyo wa kusamehe. huyu rafiki yangu aliwah kuniambia siku moja hivi wewe unasema nirudishe moyo nyuma unakumbuka maisha yangu siku za nyuma tukiwa kijijini?? akanikumbusha siku moja baba yake mzazi alikuja shule kuangalia maendeleo ya watoto wake wengine sasa akagoma kabisa kuangalia maendeleo ya huyu kijana baadae kijana akatoka kwenda kumsalimia baba alimwambia siku ukiniona kimbia wala usije ukasema mimi ni baba yako sina mtoto kama wewe can you imagine??..............huyu kaka alilia sana na namshangaa sana mungu kumuacha huyu baba hadi leo ni mzee sana ila sasa anaumaia roho sana manake mtoto wake ni bosi mkubwa sana.
 
ha haaa, rafiki wanasemaga ombea adui yako maisha marefu ili unapofanikiwa ajionee kwa macho, ndo haya sasa......
kama umewahi kukaa kijijini unakumbuka wale watoto ambao wametoka familia bora kidogo wanavyonyanyasa wenzao halafu wanaishia form two? siku hizi ukienda kijijini na prado yako wanasema anaringa kweli! wanasemaga kutesa kwa zamu
 
hata mimi mwenzangu sijazeeka......
wazee wapo kijijini.....
mjini kuna watu wazima tu, lolest!

Hapa sasa umeongea @FP,

Ni wanawake wachache wako kama teacher ambaye hajali hata akiitwa mzee....

Utani wangu mkubwa kwa bibi ni kumwambia kuwa mhhhh....naona speed ya uzee inakukaribia kwa kasi..lol!!

Ila lazima uwe utani kweli kweli, vinginevyo moto wa kuota usiku sitaupata hata nikiomba msaada wa jeshi la malaika!!

khaaa! babu hata ukatae uzee upo tu.........na natakiwa niwe handled kama mzee. si unajua wazee hatunaga purukushani?

ni heshima sana kuwa mzee katika jamii napata faraja pale ambapo hata watu mtaani wanasema kabisa mama fulan yeye ndo atatusaidia si unajua mtu mzima dawa??

Msome tena @FP, wanawake wanapenda kuonekana ni watu wazima lakini siyo wazee...

Labda wewe mwenyezetu ni special edition!!

Babu DC!!
 
Hapa sasa umeongea FP,

Ni wanawake wachache wako kama teacher ambaye hajali hata akiitwa mzee....

Utani wangu mkubwa kwa bibi ni kumwambia kuwa mhhhh....naona speed ya uzee inakukaribia kwa kasi..lol!!

Ila lazima uwe utani kweli kweli, vinginevyo moto wa kuota usiku sitaupata hata nikiomba msaada wa jeshi la malaika!!

Msome tena FP, wanawake wanapenda kuonekana ni watu wazima lakini siyo wazee...

Labda wewe mwenyezetu ni special edition!!

Babu DC!!
hivi kumbe FP hupendi kuitwa mzee?? mbona mm sion tabu labda kama kuna maana nyingine ambayo siijui kiukweli. yaani am happy to be mzee na huwa nasemaga mm ni mzee hata watu wengine huniita bimkubwa lol!
 
Last edited by a moderator:
ha haaa, rafiki wanasemaga ombea adui yako maisha marefu ili unapofanikiwa ajionee kwa macho, ndo haya sasa......
kama umewahi kukaa kijijini unakumbuka wale watoto ambao wametoka familia bora kidogo wanavyonyanyasa wenzao halafu wanaishia form two? siku hizi ukienda kijijini na prado yako wanasema anaringa kweli! wanasemaga kutesa kwa zamu

Kumbe vijiji vyote vinafanana eti?

Kuna wale watoto wa walimu...daaaahh...huwa wana nyodo utadhani ni wateule wa Mungu....

Ila sasa hivi tunapokutana nao wanaishia kujiuma uma...

Kuna mdogo wangu anapenda sana ule wimbo wa akina Rose Mhando...

Last edited by a moderator:
Kumbe vijiji vyote vinafanana eti?

Kuna wale watoto wa walimu...daaaahh...huwa wana nyodo utadhani ni wateule wa Mungu....

Ila sasa hivi tunapokutana nao wanaishia kujiuma uma...

Kuna mdogo wangu anapenda sana ule wimbo wa akina Rose Mhando...

he he heeeeeeee, rafiki kumbe na kwenu wapo?
walitunyanyasa sana wale jamaa, siku hizi wanatamani kutuamkia na wakati either tumelingana au wametupita. full kuwanunulia pombe za kienyeji......... siku ukikasirika unawanunulia creti zima la bia wahangaike nalo
 
Last edited by a moderator:
Hapana kbm, Huyu mdada anaupeo mkubwa tu kuhusu protection na nina hakika kanifanyia kwa makusudi kwani nimesikia kutoka kwa rafiki yake wa karibu.

ndugu yangu yawezeka umeoneka usomeki vizuri. Unajua wanadada wenye nia ya dhati, mara nyingi hawapendi kuvuliwa ch**i alfu uanzekuonyesha kama mpita njia tu, hapo lazima utegeshewe.
 
Sawa mkuu,

Ila kwa ushauri wako...wapige ndoa ndo wajiandae kulea mtoto au kila mtu aendelee na maisha yake halafu wajipange kulea mtoto?

Naona wadada wanaofanya huu mtego wanasahau kuwa kuna hiyo option ya pili!

Babu DC!!

Babu naona umekuwa na maslahi maalumu na huu uzi, umewakusanya wajukuu na wazee wenzio hadi wengine tunabaki tunakuangalia tu, ila umenikonga jinsi ulivyowamudu na kuwapangua.

Mi naona hoja hapo hoja kuu ni mtoto na sio ndoa, hivyo ndivyo kitini chako cha mwaka 1947 ambacho mi nakitumia kama muongozo mpaka sasa ndio kinavyosema,

ndio maana nkamwambia kijana mwenzangu tu as long as mchumba kamtangazia mimba wakati yupo naye hapo hana ujanja ni lazima alee mimba na mtoto azaliwe salama hata kama kabambikiziwa ila ndo hvyo kitanda hakizai haramu alee mtoto, hayo ya ndoa hayapo kwenye mjadala yatategemea sana na mwenendo wa mama mtoto katika kipindi chote cha ulezi huo.
Ni hayo tu babu, nipe maksi zangu kama navielewa vitini vyako ulivyoniachia toka kipindi kile ulivyotoka vitani WW II.
 
Mkuu jouneGwalu,

Sina cha kuongeza...nimekupa A+

Dogo alee mimba (after all atafaidi joto...lol) halafu ajisikiliziea kama kweli bado anahisia za kusogeza majeshi mbele..

Ndoa isiwe katika mazungumzoa ya sasa ingawa....hawa watu wana utundu mwingi ndo maana wale wavivu wa kufikiri huishia kusingizia limbwata!!

Pamoja sana mkuu,

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
mie mtu akiniwekea usiku let say mwaka mzima hatangazi ndoa namtegeshea na akichomoa tu namwambia baba yangu amsomee HALAL BADRI aokote makopo

Eti mwanaume anakutumia weee, kisha anakuja na hadithi, eti wazazi wamemtafutia mke huko kijijini, nyoooo, asiku nhiyo atajua tofauti ya tui na maziwa, au tende na halua

sipendi mie mwanaume kunigeuza shanuo,

Ah mimi ninaomba msaada hapo kwenyye red........mwanaume anakutumia? Anakutumiaje?

Uchumba sugu mnautaka wenyewe, mbona kuna njia nyingi za kumfanya ajicommit bila hata kumtegeshea mimba wala madawa? Mfanye akuone wewe ni mwanamke wa pekee, mfanye aijue thamani yako na atambue kosa atakalolifanya iwapo ataachia apokonywe na mwanaume mwenzake, mfanye ajione yeye ni mwanaume mwenye bahati kuwa nawe kimapenzi. Na zaidi ya yote, mwambie MUNGU haja ya moyo wako.

Nawatakia kila la kheri wanawali wooote mnaotarajia kuwa na wenzi wenu wa maisha, na nyie wenye uchumba sugu, amkeni tokeni usingizini, tambueni thamani zenu, chukueni hatua.
 
Mfanye akuone wewe ni mwanamke wa pekee,

Kwa vipi utamfanya akuone wewe ni mwanamke wa pekee?

mfanye aijue thamani yako

Ni njia zipi utatumia kumfanya aijue thamani yako?

na atambue kosa atakalolifanya iwapo ataachia apokonywe na mwanaume mwenzake

Apokonywe kivipi na mwanaume mwenzake? Ina maana wewe huna usemi wala uamuzi wowote ule wa nani unataka au kupenda kuwa naye?

mfanye ajione yeye ni mwanaume mwenye bahati kuwa nawe kimapenzi.

Kivipi utamfanya ajione yeye ni mwanaume mwenye bahati kuwa nawe kimapenzi?
 
Kwa vipi utamfanya akuone wewe ni mwanamke wa pekee?

NN aksante kwa maswali yako - Kwa mwanamke mkamilifu (Simaanishi kuwa kuna waso wakamilifu) namaanisha mwanamke anayejitambua kuwa yeye ni mwanamke mwenye thamani haweziruhusu kuwa na mtu asiyeziheshimu hisia zake wala mtu wa kumchezea na kumchukulia yeye kuwa poa. Kuna njia nyingi za kumfanya mwanaume akuone wewe ni mwanamke wa pekee - Wanawake wananielewa hapa. Kama utawezasoma misimamo ya Da Kaunga, nyumba kubwa, @ King'ast na wengineo utagundua mwanamke anayeitambua thamani yake.

Kuhusu namna ya kumfanya akuone wewe ni wa pekee ni nyingi, kubwa kujiheshimu na kumuheshimu yeye (sio kumwogopa na kuwa mtu wa Yes kwa kila kitu akitakacho yeye hii inajumuisha pia kuwa na say katika tendo la ndoa including abstaining; using condom and being strictly about no baby before). Wanawake wengi huwa tunaplay 'Without you am doomed" role katika mahusiano yetu mengi. Na once mtu ukishakuwa au kupotray image hiyo kwa mwanaume tayari anakuingiza kwenye kundi la 'King'ang'anizi" wa ndoa ambako ndipo wanawake wengi wapo. Ukifanikiwa kuondoka katika kundi hili (au at least kumwaminisha kuwa si mmoja wapo) utamdhihirishia kuwa wewe ni wa tofauti. (hapa nimesema ziko namna nyingi na hii ni mojawapo tu)

Ni njia zipi utatumia kumfanya aijue thamani yako?
Jamani NN, kwani wewe ukitaka mtu mwingine akuthamini unafanyaje? Si kujiheshimu na kuwa na misimamo inayoeleweka? Mahusiano ya mapenzi ni kama mahusiano mengine tu ambayo ni muhimu kwa kila mtu kujitambua na kujiheshimu/ heshimu wengine pia. hii pia inajumuisha juhudi zako katika maisha na msimamo wako kwa ujumpla. Usitoe nafasi kwa mtu kukudegrade kwa namna yoyote iwe ni kwa kukusudia au kutokukusudia, learn to reason na usiwe mwepesi wa hasira na kukurupukia mambo n.k.

Kwa mwanamke aliye katika mahusiano, uelewa ni muhimu sana iwapo mambo yanatokea hupaswi kukurupuka na kuaibishana hadharani wala kukimbilia kulaumu na kutoa hukumu. Chukua muda wa kusikiliza mwenzi wako kisha mpe nafasi ya kujitetea ili kwamba hata ukiamua kutoa hukumu basi hata muhukumiwa aridhike.

Apokonywe kivipi na mwanaume mwenzake? Ina maana wewe huna usemi wala uamuzi wowote ule wa nani unataka au kupenda kuwa naye?
Samahani hapa haikuwa nia yangu nieleweke hivi bali maana yangu ilikuwa kumfanya awe na woga wa kukupoteza iwapo utamgundua kuwa haitambui thamani yako na wewe ukaamua kwenda kwa mwenye kukuthamini. Yaani ile unakuwa na mtu ambaye s/he is almost perfect na unampenda. Wengine wanapopata mtu wa aina hii hujisahau na kujiona wao ndio wao matokeo yake anakaa na wenzie vijiweni akitangaza ushindi ... yule kwangu hapindui aisee, nikimtema atajiua!' bila kutambua kuwa kufanya hayo ni kuhatarisha mahusiano yao kwani usijeshangaa mwenzako akatake advantage pindi mpenzio akiamua enough is enough.... (wengi tumesikia vilio vya mashost waliopokonyana waume, na nina amini pia zipo japo chache za wanaume ambao waliwatema wenzi wao na marafiki zao wakawapokelea kwa bashasha na mapenzi ya hali ya juu)

Kivipi utamfanya ajione yeye ni mwanaume mwenye bahati kuwa nawe kimapenzi?

Ah jamani NN, na hili nalo nilijibu? kwani how do you make someone you love ajifeel special? those tricks now!
 
Last edited by a moderator:
babu hukumtendea haki huyo dada.
Wewe ulikuwa unajua hatma ya huo uhusiano, na yeye kwa vile alikuwa part and parcel ya huo uhusiano alikuwa na haki ya kujua hatma ya uhusiano. Kama wewe ungekuwa hujui hilo ni swala jingine, lakini ulikuwa unajua kuwa una mpenzi ambaye unampenda sana na unarudi kwake, kulikuwa na ubaya gani kumshirikisha huyu ili ajue hatma yake?
Wakati mwingine na nyie wakaka huwa mnakosea sana, mnadhani nyie ndo mna power ya ku-dictate relationship, mnasahau kuwa mahusiano ni ya watu wawili, na wote mna haki ya kujua status ya relationship yenu. Ndo maana mara nyingi mimi nasisitiza kwenye ndoa huwa tunaoana, hakuna anayemuoa mwenzie, lol!
Mashosti gfsonwin, kongosho, king'asti, cacico, nivea, ciello, madame b, zinduna na mlongo wangu snowhite mje mnitetee hapa babu akinirushia konzi, lol!
ndio maana watoto wetu tuwaweke kwenye maombi sana! Especialy watoto wa kike! Maana wanaume hupumzika na kupita, binti anadhani anapendwa kumbe anadanganywa liveeeeeeeee! Inauma sana, sijui wanangu nitawaficha wapi kwa kweli!
 
Unaona DA....hapa ulicheza kama yule jamaa wa kwenye movies za Rambo,

Hivi mdada anaweza vipi kuishi na lijamaa likijikamulia kwa miezi, miaka hadi inakaribia muongo mmoja bila kukata hata bima ya third party?

Bajaj zenyewe zina bima, iweje hao wadada wanabweteka? Au dozi inawafanya vipofu??

Babu DC!!

Babu muhimu bana wanaume nyie acha kabisa nashindwa kuelewa utakaaje na mtu miaka mitano eti uchumba?? Uchumba gani huo?? aku babu eehhh
 
Back
Top Bottom