Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

Mila hizi za Kichaga mnazionaje wenzangu

Kuna watu hapa Tanzania wana mila na desturi hao Wachagga ahata tone hawafikii...
Mkuu kama wanafikia au hawafikii hii sio hoja. Hapa hoja ni hizi mila wewe unazionaje? Kama kuna makabila mengine yana mila zinazohitaji mjadala unaweza kuzianzishia uzi wake maalum.

Kwa wale ndugu zangu wachaga mimi nawaomba msichukulie huu uzi kama vile una lengo la kuwachafua, chukulieni kama ni changamoto tu. Nadhani tatizo labda ni kutaja kabila husika. Huenda ingewekwa bila kutaja kabila ingekuwa bora zaidi.
 
Yalinikuta mwaka jana;nimeoa mchaga kumbe mama yao akulikuwa mzaliwa wa pili,wa kwanza alifariki bila kuolewa.Kimila muoaji anapaswa kuoa yule marehemu kwanza kisha ndio aoe mzaliwa wa pili.Na watoto wa mzaliwa wa pili wanakuwa wa mzaliwa wa kwanza ambaye ni marehemu/mzimu.Hivyo ni watoto wa mzimu!!na wanatabia za mizimu sasa kutoa hizo roho za mzimu asikwambie mtu,hawa manabii maarufu walishindwa.Karismatik ubungo ndio waliweza alikuwa zaidi ya kichaa.Sitakaa nikasahau!!!
 
Acha uongo wewe chasaka yani karne hii kunakurithiana kweli ?labda ulienda musoma wizi mtupu.
 
Ukikumbuka ya ndege ya Malaysia, naamini utairekebisha hiyo phrase..
Jamani, hivi hii ndege bado haijajulikana ilko na abiria wake? Hata vyombo vya habari havizungumzii hii ndege tena! Hivi wale waganga wa kibongo wanaojitangaza kuweza kutoa dawa za kumvuta mtu aliye mbali na kurudisha mali iliyopotea wako wapi? Kwanini wasiitafute hii ndege?
 
Acha uongo wewe chasaka yani karne hii kunakurithiana kweli ?labda ulienda musoma wizi mtupu.
Kama sikumwelewa vibaya, MtiMawazo mtimawazo Hakurithi bali alimuoa (marehemu kiroho) na mdogo wake kimwili...mdogo wa marehemu alipozaa mtoto wa kwanza huyo mtoto (alizaliwa kiroho) kwa mama marehemu.
 
Wewe Mpuuzi muda wako unatumia vibaya fanya kazi za kukuingizia kipato cha wewe na wanao! Njaa kali wewe!
 
Mengi yamezungumzwa lakini ukweli utabakia kuwa ukweli. Mila na desturi zinaendana na mahali husika na kwa wakati husika. Hata kama Wageni wasingekuja tungefika mahali tuache moja baada ya nyingine.

KWENDA MOSHI
Sio lazima Desemba kila mwaka kwenda Moshi na sio wote, kwanza inabidi kujiandaa. Lengo kubwa ni kupumzika baada ya shughuli nzito za mwaka mzima. Unaweza kwenda mahali popote mwenyewe au na familia kama mfuko wako unaruhusu. Wengine hata nje ya nchi wanaenda! Sasa kwa kwenda mlimani ndiko mahali utakapokutana na ndugu na marafiki wengi kwa kuwa ndiko ulikokulia ukasoma hadi ukaanza kwenda nje ya kwenu! Na hii inaleta afya kwa kweli hata kama huna kitu mfukoni ile kuonana na unaowafahamu wengi huleta faraja. Kama kuna wanaoenda kutoa kafara kwa kipindi watakuwa wachache sana. Na mnapokutana ndugu wengi mbuzi au ngombe watachinjwa kwa kitoweo! (Sio kafara). Kuku ndio usiseme! Mbege na vinjwaji vingine vitanywewa kipindi chote hadi siku ya kurudi kwenye mahangaiko.

KUZIKWA MOSHI
Hii vilevile inategemeana na uwezo wa wafiwa. Sehemu ya kuzikwa ni uamuzi wa mtu na wakilazimisha kukupeleka ambako hukusema janga lingine huwa linatokea. Moshi sasa hivi ardhi hakuna na mbaya zaidi kama ulibahatika kupewa sehemu yako itabidi ukazikwe hapo sio walipozikwa au watakapozikwa wazazi wako. Kwa mantiki hiyo maeneo mengi sasa ni makaburi!
Hii ya kufukua makaburi kutoa mifupa imeshaachwa tangu miaka ya sitini (1960) kama wapo wanaofukua kwa sasa ni wachache sana.
Hata hiyo ya kuzika watoto wadogo bikira kwa ajili ya mapatano iliachwa mapema sana labda baada tu ya Wazungu kuingia. Kumbuka hii haina tofauti na mwananmke mzinzi anapopigwa mawe hadi kufa kwa upande wa Waislamu ila tu hao watoto walikuwa hawana hatia yoyote! Na hii ilikuwa ni ya kuogopesha sana na hivyo vijiji hawakupigana tena asilani.

KUKEKETA WANAWAKE
Hii ni wachache sana wanafanya sasa hivi na lengo kuu waliamini kuwa inapunguza hamu ya kujamiiana itakayosababisha kupata watoto wengi bila mpango. Suala la kujaamiiana lilichukuliwa kama kitendo kitakatifu na sio starehe ila kwa sasa ni mwendo mdundo!

KITOVU CHA MTOTO
Zaidi ni imani na hata sasa hivi ni wachache sana wanapeleka vitovu vyo watoto wao Moshi. Na hakuna madhara yoyote yatakayompata mtoto kwa kutopeleka kitovu. Na ujue hizo ni imani walisema kitovu kikidondokea dhakari ya mtoto anakuwa hanithi. Sasa kwa sababu ya imani inatokea hivyo lakini usipoamini mtoto anakuwa rijali kama kawaida.

KUCHINJA
Hata kuchinja kulikuwa na miiko yake na kama hujafundishwa huruhusiwi kusogea na kisu lakini siku hizi ni mwendo mdundo hata ukianzia mguuni mradi nyama ipatikane. Na vilevile sehemu fulani ya nyama inakuwa ya mtu Fulani ila kwa siku hizi wewe kama ulitegemea kidari ukipata paja au mbavu unashukuru.

NDOA
Yameshazungumzwa ya kutosha ila kwa wakristu biblia inasema mkatekeleze mila njema za mababu zenu! Kwa hiyo sio mila zote ni mbaya!!!
 
Utamu wa mbuzi ujue na jinsi ya kuila la sivyo gaut inakungoja!
 
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu.

Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo.

Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.
Madhara ya kuzaliwa magorofani halafu unajiita Mchagga
 
Nyingi ya hizi mila zimepitwa na wakati na kwa sababu ya dini na shule wengi wameshaziacha. Na ukiona anayengangania ujue huyo ni mchawi.
Huko ndo wazungu walipotufikisha ,ngoja tuje kufahamu kuwa dini zilikuwa feki tutajuta na kusaga meno
 
Mbona Wamasai hamuwasemi mirazao kutembea na Sime lakini Bayazaidi uwezi kuta Mmasai Kilema kwani hawazariwi virema au mira wana wapopotoa kabla kwani ni Mkosi mirazao
 
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu.

Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo.

Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.
Mila sio zote zenye nafasi, zipo baadhi hazifaikabisa kama kutoa kafara ya kuchinja mbuzi na kunyunyiza damu, kwa mfano umenunua gari mpya, umejenga nyumba unatakiwa ufanye, huu mi nauona ni ushirikina kwa nini msifanye sala tuu kwa jina la Yesu.

Nyingine kwa mfano kufukua kaburila marehemu na kutoa mifupa yote na kuiweka kwenye mgomba.

Nyingine kupelekangozi ya kitovu cha mtoto mchanga kinachokatikaga kwa Babu na Bibi eti ilimtoto asiwe anauguagua ovyo.

Au lazima kwenda kuzika Moshi wakati unakutamarehemu amejijenga na kushi sehemu nyingine miaka yote na kwao hata nyumba hana.
 
Frankly speaking, hizo ni Kafara na zina wa cost sana sana. We angalia nguvu ya hao mizimu inavyowavuta kila mwisho wa mwaka wende kutoa sadaka za damu, na huwa wasipoenda wanakufa wenginewanapata ajali. hii ni chambo ibilisi anawamaliza kistaili kwa sababu shetani anapotaka damu baadaye anatake damu ya mtu. kama wewe ni mchaga fanya mpango ukawakomboe ndugu zako wamwamini Mungu wa Kweli. Seriouly sisi Tulijaribu kwenda kuzivunja hizo mila kwa njia ya maombi tukafanikiwa lakini vita ilikuwa kali mno. Mungu anaweza of course wanahitaji masaada wa haraka kwa kuwa wengi wao wanachanganya Mungu na miungu na matokeo yake Mungu amewaacha. Mf nasikia wanapotoa nywele wakati wa msiba ni mapango wa shetani kuandaa mtu mwingine atakayekufa next. inasikitisha na wanahitaji maombi. Tofauti na mikoa mingine ambao wengi wao hawamjui Mungu ni rahisa kuwahubiria juu ya Mungu wa kweli. Lakini hawa wanachanganya...kanisani mila na kwa waganga. Urgent need for intercession!
Nani kakuambia upumbavu huo ingekuwa kutolewa nywele mwingine anafuatia kufa mimi mke wangu mchaga marayakwanza na mwisho kunyolewa nyweli ni 1999 kwenyemsiba wa dadake hadi leo amna alie danja........ Warimu wakue
 
Huko ndo wazungu walipotufikisha ,ngoja tuje kufahamu kuwa dini zilikuwa feki tutajuta na kusaga meno

Cha msingi tuliipokea imani na kwa kipindi chote imetuletea faraja. Ingekuwa tofauti tungetoka kivingine. Hata kama huko kwao dini wameiacha sas hivi ni kipindi chao kimefika na hata sisi kuna kipindi kitafika tutabadilika hii ndio dunia ambapo vitaumbwa vizazi vipya na vitakuwa na hisia tofauti na sisi!
 
Back
Top Bottom