Mikutano Miwili Mikubwa ya China: Ina umuhimu gani kwa jamii ya kimataifa?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111370967754.jpg


Mikutano Miwili mikubwa nchini China, ambayo ni Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) na Mkutano wa Bunge la Umma la China (NPC), inatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi Machi hapa Beijing katika Ukumbi wa Mikutano.

Mikutano hii imekuwa ikifuatiliwa sana na jamii ya kimataifa, ambayo inatilia maanani sana maendeleo ya nchi hii kubwa inayoendelea na ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, ikiifuata Marekani.

Mikutano hii miwili inajumuisha mikutano ya kisiasa, na inawawezesha viongozi wa nchi hiyo kufanya tathmini ya kazi za serikali kwa mwaka uliomalizika, na kupanga malengo kwa ajili yam waka unaofuata.

Kawaida, mkutano wa Baraza la Mashauri ya Kisiasa hufunguliwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Bunge la Umma la China. Jukumu kubwa la Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ni kutoa ushauri kwa serikali. Baraza hili linajumuisha watu kutoka ngazi mbalimbali za maisha, wakiwemo wafanyabiashara, wanamichezo, wasanii, na wanasiasa. Wajumbe wa Baraza hili wanachukua nafasi kubwa katika kutoa mapendekezo ya sera na kufanya majadiliano kuhusu masuala mbalimbali.

Mkutano wa Bunge la Umma la China una jukumu la kupitisha sheria na kuridhia bajeti. Bunge hili lina wabunge karibu 3,000 na pia ni bunge kubwa zaidi duniani.

Ni kwa nini basi jamii ya kimataifa inafuatilia sana Mikutano hii? Ni wazi kwamba China imeendelea kuongoza katika sekta ya uzalishaji duniani kwa miaka karibu 12 mfululizo. Kutokana na hilo, mipango ya kiuchumi ya China imekuwa na athari chanya katika uchumi wa dunia.

Kwa upande wa Afrika, China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa bara hilo, na uwekezaji wa China barani Afrika umezidi kuongezeka, ambapo mwaka 2020, China iliwekeza dola za kimarekani bilioni 2.96, ikiwa ongezeko la asilimia 9.5 ikilinganishwa na mwaka 2019. Afrika imefaidika sana na maendeleo ya China, hususan kwenye sekta ya ujenzi wa miundombinu na pia sekta ya afya.

Kutokana na hilo, tunaweza kusema kuwa Mikutano hii miwili mikubwa ya China itakayoanza mwanzoni mwa mwezi Machi, ina umuhimu wa kipekee kwa nchi za Afrika. Hii inatokana na kuwa China imekuwa ikijitahidi kusaidia maendeleo ya nchi za Afrika bila ya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi hizo.
 
Back
Top Bottom