Mikutano mikubwa ya kisiasa inaendelea kwenye daladala, mabasi, masokoni, vituo vya bodaboda

Majuzi kwenye daladala moja jijini Mwanza mtu mmoja alianza mjadala kwa kumpa sifa mkulu kwa jinsi anavyoendesha nchi na kwamba maisha yatakuwa mzuri hapo baadaye. Duh! kwa namna alivyoshambuliwa kwa hasira utadhani moto uliomwagiwa petroli. Wengi waliulza kuwa mkulu anawezaje kuharibu kwanza ndipo arekebishe baadaye?
 
Uzuri mwisho wa siku kila mtu anashuka kituo chake maisha yanaendelea..Yale mambo ya mtu asubui anaondoka mtupu jioni anarudi na laki mbili ya bila jasho hakuna tena
 
Kwa hii namba tunayosomeshwa na uyu mwalim olewake mtu akosee! Kwenye mtian wa 2020 tutachapana wanafunzi kwa wanafunzi maana uyu mwalim anafundisha kwa bidii zote ata mwanafunzi kilaza anaelewa
 
Wewe ulitaka wakaongelee wapi? Ile ya hadharani mmepiga marufuku waweke gundi midomoni basi
 
Unadhani hao wakuu watabadilika kwa namna youote hata kama Wa tz woo-o-te wakilaumu kwa kutoa mapovu mdomoni ? Hakuna kitu. Naona hali mbaya sana sana ya uchumi miaka michache tu ujao. Kama mapato ya bandari na utalii yameshuka na kwa upande mwingine misaada toka nje ni midogo sana mapato ya serikali yatapungua na inaweza hata kufika mahali ikashindwa kulipa mishahara. Likitokea hilo hakuna anayejua nini kitafuata
 
Kweli vijana wa bavicha hamna kazi, kila siku kutunga umbeya haya tumekusikia
Kila anayetoa maoni msiyoyapenda ni BAVICHA?
Ungejua kwamba vyama vyote vya siasa ukichanganya wanachama wake wote hawafiki hata 10 milioni, usingeandika takataka
 
inaitwa mikutano ya kijamii
Hiyo mikutano ni hatari kuliko hata ya jangwani , kidongo chekundu au kibanda maiti , maana unaambiwa hata askari wanashiriki na kutoa madukuduku yao , unaambiwa ni noma sana !

Hakika siasa haizuiliki .
 
Katika hali ya kawaida. Kama mtu ni mwelewa ,,,siasa haiwezi kujitenga na Maendeleo ya nchi na watu!!! Never!! Watu ndio wanaofanya siasa na ndio wabaamua ni wap watafanyia siasa hiyo, wataongea nn wanajua wao, sio lazima waende kuomba kibali polisccm
 
Back
Top Bottom