Kuna shemeji yangu mchaga, yaani mapishi ni zero kabisa , dagaa wa jero mafuta anaweka nusu ndoo... daah
Mikoa ya Geita nimegundua hakuna Nazi ...ila kwa wali wanawazidi aisee wanapika wali vzr sana
Leo Kanda ya pwani tumesifiwa
Ni matatizo ya ulimi wako mkuu usituaminishe kwamba hawa wanajua kupika na hawa hawajui kupika
Tanga siamini kama kuna mtu atajitokeza na kusema Tanga hawajui kupika.... Wale watu kwenye swala la kupika ni namba nyingine....
Acha kupiga chekecha.
Povu atakalo pata kutoka kwa watu wa Arusha na Kilimanjaro hautaamini macho yako
Mchaga akupikie mtori utapenda
Mtori una maana kwenye wali ni boko boko la ligi kuu?
Mkuu unatokea geita?
hahahaha mchanyato wa ndizi na nyama mkuu
Ndio nafahamu lakini umeona eneo moja la mtori ambao wanavuruga ndizi ule uji wanaweka kwenye chupa ya chai ili usipoe halafu nyama wanakata finyango ndogo ndogo wanakuwekea kwenye bakuri, una maana wali wachaga hawafahamu kupika
Aisee mbona sisi ambao tumezaliwa, kukulia na kuoa kwenye hiyo mikoa ya list B tukipikiwa chakula huwa kitamu sana lakini mwisho wa yote kupika inategemea na mtu bila kujali katokea mkoa gani labda uwe na chuki na watu wa hiyo mikoa ndo unaweza usione kwamba wanapika vizuriWakuu.
Nimetembelea mikoa mbalimbali katika harakati za kusaka maisha lakini kama mnavofahamu mikoa mingi kuna tamaduni tofauti za mapishi
Kuna mikoa chakula unaweza kula ukaona ladha ya chakula japo ni kwa mama ntilie lakini chakula kitamu na mikoa mingine imejaa laana bin balaa yaani ukila chakula utahisi hadi kuugua homa ya manjano.
A: Mikoa Wanayojitahidi Kupika vizuri
1. Tanga
2. Pwani
3.Lindi
4. Mtwara
5.Dodoma
6. Morogoro
7. Mwanza
8. Kigoma maeneo ya Ujiji
9. Dar Es Salaam.
10. Tabora.
Ifuatayo ni Mikoa yenye laana bin balaa sijui hua wanaloweka au maana chakula asilimia kubwa hakina ladha kabisa.
B:Mikoa hiyo ni Kama Ifuatavo
1. Mara
2.Arusha
3.Manyara
4.Singida
5.Ruvuma
6. Rukwa
7. Katavi
8. Iringa
9. Mbeya
10.Njombe
11.Geita
12. Simiyu
13.Kagera/Bukoba
14. Kilimanjaro.
Huo ni utafiti mdogo kabisa sijui wanatatizo gani
Mkuu Singida na Manyara pande za Kondoa wale washenzi wanajua kupika bana! Tanga hawaoni ndani..Kwa Tanga sina ubishi,kama ndio umepakuliwa halafu umejifungia chumbani na hakuna mtu anakuona unaweza kujikuta unalamba na sahani...
Wachaga ni wapishi wazuri mno ndio maana mahotel makubwa wapishi wakuu ni wachaga,hata matamasha ta nyama choma wamiliki ni.wachagaUnachotafta toka kwa wachaga utakipata japo umenena ukweli mtupu
Subiri wanakuja