Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

yeye kutaarifiwa hakuna tatizo lakini mko kwenye msafara mmoja, na Waziri wako anaenda hotelini kutia sahihi mkataba ambao utajenga mgodi wa dola milioni 400, hauambiwi unasema ilikuwa sawa? Hivi ni nani huyo anayewakurupusha kujibu? Sasa leo Rais kakataliwa na wananchi kuingia Buzwagi.. wataeleza na hilo ni sawa? Haya ndiyo naita majibu ya kihuni!

....amen brother! its really irritating.
 
Kwa maoni yangu Wizara ya madini ni moja ya Wizara nyeti za Tanzania. Hasa ukitilia maanani malalamiko makubwa ya wananchi kuhusiana na mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania na pia kiasi kikubwa cha pesa kinachohusika katika mikataba hii.

Muungwana anastahili kupata briefing at least kila wiki kama siyo kila siku ya nini kinachoendelea katika wizara hiyo kama siyo kila siku ili kuwa up to date na matukio muhimu wizarani. Kuna wizara ambazo muungwana hana haja ya kuzifuatilia kwa karibu kiasi hicho lakini si wizara nyeti ikiwamo ya madini.

Ofisi ya Rais imechemsha kwa kudai kwamba Rais haihitaji kuarifiwa kuhusu mikataba. Karamagi wizara imeshamshinda na hana tena credibility hapo wizarani na hata machoni kwa Watanzania. Muungwana inabidi atafute mtu mwingine ili aongoze hii wizara nyeti.
 
"Rais anawaamini watendaji wake na amewapa dhamana ya kuwakilisha nchi katika masuala mbalimbali," alisema Kibanga na kumtetea Karamagi kuwa waziri huyo alifuata taratibu zote kabla ya mkataba huo kutiwa saini.

Alisema alichofanya Karamagi kuweka saini mkataba wa uchimbaji wa madini wa Buzwagi bila kumuarifu Rais ni sahihi kwa vile hatua za majadiliano juu ya mkataba huo zilikuwa zinafahamika ndani ya Serikali na Rais alikuwa anaarifiwa.


I wonder when did this woman know these kind of things. I am not even sure if she really know what she is talking about, labda ndio huo huo ushabiki, nidhamu ya uoga, au kuonesha solidarity tu. Nafahamu kuwa kuna siku hii itadhihirika wazi, na sijui hao wanaosema kuwa yuko sahihi wataficha nyuso zao wapi. Kwanini mkataba usainiwe hotelini London, na sio ubalozi. Karamagi was right, this is ridiculous! Kibanga angekaa kimya tu kujilindia heshima yake.
 
basi tumekwisha mweeee, laiti kama jk hapaswi kujua juu ya mikataba kusainiwa ! nadhani haitokuwa vibaya kama nikifikiria kuna mikataba zaidi ya 20 iliyosainiwa kisanii.
 
...400m$ is a big chunk of deniro kwa nchi kama Tanzania,sasa kusema Kikwete sio lazima ajue sijui wana maana gani...mikataba mikubwa kama hii ni level ya State house & cabinet,National security na bunge pamoja,nafikiri huyo mpuuzi anazungumzia miradi ya kuchimba visima
 
1. Mudhihir ktk kujenga hoja yake alilidanganya Bunge kuwa Zitto alisema Karamagi ni muongo amelidaganya Bunge! Huo ulikuwa uzushi na kama alivyodai kuwa ni ushindani wa mchezo, kapafanya Bunge kuwa mahala pa michezo ktk maslahi ya taifa..
2.Kuna mbunge mwingine mwanamke wa huko Bukoba aliyedai Bungeni kuwa rais anafahamu uwekaji wa Mkataba huu kwa sababu walikuwa pamoja na Karamagi London!

Wabunge hawa wame lidanganya Bunge na sisi wananchi na kama kuna watu wa kusimamishwa basi hawa wawili ndio walioleta habari zote za upigaji kura kumsimamisha Ziito.
Hawa wachombezi wa mambo ya kisiasa ni lazima wasimamishwe na iwe funzo kwa Wabunge vilaza!
 
mwenzenu nafikiri Karamagi alipitiwa tu, sasa kwa vile hatuna utamaduni wa kuomba msamaha na kukubali kukosea ndio imebidi agangamale hivyo hivyo, kwani nani kati yetu hakosei? tuachane na mambo haya na tusonge mbele.

asanteni

Kwanza kabisa heshima yako Bi.Senti 50.

Nakumbuka kunawakati ulimtaka Mkjj aache harakati zake kwani kwa madai yako ni kuwa ange 'lauliwa', leo tena unakuja na hili, kwa kweli kabisa mimi nashindwa kukuelewa... Sasa nikuulize;

--Ditto alipiga risasi mtu... naye tumsamehe na kusonga mbele?!
--Mikataba mibovu viongozi walisaini kuhusiana na IPTL na Richmond... nayo tu samehe na tusonge mbele?!
--Majengo mapya ya BoT yako inflated ujenzi wake na utunzaji...tusamehe na tusonge mbele?!
--Mabarabara yana mahandaki...tusamehe na tusonge mbele?!
--Maji masafi hayapatikani....tusamehe na tusonge mbele?!
--n.k.
--n.k.
--Majambazi yanavamia mabenki/maduka...tuyasamehe na tusonge mbele?!
--Mikopo ya wanafunzi inaibiwa...tuwasamehe wezi na tusonge mbele?!
--Dala dala zinakatisha route... tuzisamehe na tusonge mbele?!
--Lecturer kapokea hongo... tumsamehe na tusonge mbele?!
--Wanamziki/mijibaba wanalaghai watoto wadogo wa shule...tuwasamehe na tusonge mbele?!
--n.k.
--n.k.
--Paka/mbwa wako kajisaidia chumbani mwako...msamehe na usonge mbele?!
--Jirani anatembea na mume/mke wako...msamehe na usonge mbele?!
--WAZIRI ANASADIKIKA KUFANYA MAKOSA YA KUINGIA MIKATABA...TUMFUNGIE ALIYESEMA HIVYO,TUMSAMEHE WAZIRI HUYO NA TUSONGE MBELE?!
--N.K.
--N.K.

Ndugu, hivi mwanzo wa kuwa ajibisha wafanyao makosa,kuwa lazimu kutambua makosa yao, kuwa kosoa, na kuwa lazimisha watubu hadharani makosa hayo na kuweka kikomo kwa makosa haya yanayo jirudia rudia mwaka nenda rudi, ni lini mawazoni kwako?! Huoni kuwa tumechoka na kusamehe na kusonga mbele gizani?! Matokeo yake ni kuambiwa kuwa chukueni hizo 30% za madini yenu tuliyachimbua ardhini kwenu nasi hii 70% ni yetu, tutawaachia hayo mashimo kuyafukia baada ya miaka 25 pale ndege yenu itakuwa inajaza mafuta Kiwalani tayari KUPAA!!

Kwanini viongozi wetu hawa adhibiwi?..Lini chanzo cha hili, wanao ua hawafungwi, wanao iba hawafungwi, hamna anayetubu makosa, kila kukicha tunaambiwa ni makosa yakiutendaji ya viongozi...ni wapi hawa kama hatu wakani hadharani na kuwaadhibu wanao ligharimu Taifa letu mabilioni baada ya kuingia bichwa bichwa kwenye wasiyo yajua na bila kuwa na subira?! Tusubiri mpaka lini kuona kiongozi wa Tanzania amefungwa?!

Je, viongozi wetu wamesahau kuwa kila kitu kina mwisho?! je wamesahau kuwa njia za mawasiliano na kimtandao kupitia radio,simu,television,internet zinabadilika na hawana uwezo wa kuzuia hili?!
Kwa kweli Bi.Senti 50 nakusihi uwaambie viongozi kuwa MWANZO WA MWISHO UMEANZA; KUTIMIZA AHADI NI WAJIBU NA ZA MWIZI NI AROBAINI. Usipofanya hivyo nao wakawa hawajui hili, toba, tutaisha kwa kutegemea kusamehe na kusonga mbele tusikokujua...tuking'ang'ania unachodai,nami hapa nitaondoa heshima yako kwa kubadilisha jina lako na kuwa- Bi.Senti TANO!! 🙂
Ahsante.

SteveD.
 
What $ 400 Mills Rais asiambiwe, duh kweli kazi tunayo.
Mimi najiuliza huyo Karamagi alidandia msafara wa Rais kama mhusika mwenye hakujua kinachompeleka Karamagi UK?
Kwenye huo ujenzi wa mgodi wanafaidika wengi directly na indirectly(THA,TRA,TRC, vibarua) lakini bado washauri wa rais na wa wizara husika hili hawakuona lina umuhimu wa kumtaarifu Rais, hapa kuna walakini si bure watu wanajaribu kufuta nyayo zao.
 
Hivi hivi vichwa vinavyoplan hii demage control operation walikuwa wapi wakati kina Mudhihir wanajifunga (ama wanamfunga JK) goli la kisigino> Kwanza alikuja mama naibu spika, Makinda na kuwa issue ya Zitto bado ina umuhimu lakini alikosea kutumia neno waziri muongo baada ya wengine kukurupuka na vitisho sasa wamekuja kina Primi na hii ya kutokuwa na ulazima wa rais kujua kama waziri ana mkataba.

Ingawa ni vigumu kuingia akilini kwa watanzania walioshaudhiwa na waliojawa ghadhabu ni wazi utetezi wao kidogo unaonyesha dalili ya kukaa na kupanga. I bet hii ni matokeo yaq vikao lukuki vya kuokoa jahazi baada ya mabaharia watundu kutoboa ngalawa kwenye mkondo wa msumbiji...

Tanzanianjema
 
Mkataba wa $400m kutojulishwa raisi wa nchi maskini kama Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa hivi karibuniwananchi hawajaridhishwa na mikataba mingi, najiuliza raisi na ofisi yake kwa nini kuwepo maana mawaziri waweza fanya kila kitu? je mikataba yote isiyofaida kwetu hapo nyuma ilitiwa sahihi na mawaziri bila rais kujulishwa na kwamba mpaka sasa rais hajajua kwamba haikua sahihi kufanya hivyo na kua alitakiwa kufuatilia mikatapa mipya moja kwa moja. Kwa nini raisi ajihusishe moja kwa moja kurekebisha mikataba badala ya kuhakikisha mikataba mizuri na ya uwazi inafanywa kwa kuhusishwa ofisi yake moja kwa moja. Kutojulishwa ni kosa na lazima tuonyeshwe na serikali kwamba hili kosa linatatuliwa vipi ili lisitokee tena na kwamba nani atabeba hilo kosa, ni raisi ama waziri.
 
Naomba nichangie kwa maono tofauti kidogo kuhusu kauli ya Ikulu kwamba "Si lazima Rais ajulishwe kuhusu mikataba na kwamba alijua kuhusu mchakato."

Kwanza kabisa, natanguliza kusema NAWAPONGEZA SANA IKULU kwa Kumuunga ZItto mkono kwa asilimia mia moja, kabla ya kuitetea hoja yangu hapo juu. Hapa sasa ndio wale wanaojipendekeza wataona kwamba JK hayuko pamoja nao.

Siku moja tu baada ya Zitto kuibua hoja hiyo bungeni, kabla hata suala hilo halijapamba moto, gazeti la KULIKONI liliandika habari iliyosema kwamba, Karamagi hakumjulisha Rais aliposaidni mkataba London wakiwa pamoja" kwa mujibu wa habari hiyo, KUlikoni walisema kwamba hata BAraza la Mawaziri, linaloongozwa na JK halikuwa na taarifa. Hakuna msemaji wa Ikulu aliyekanusha habari hiyo kabla ya habari ya jana katika gazeti la serikali ka HabariLEo kusema kwamba " Si lazima Rais ajulishwe". lakin ukiangalia habari hiyo ya HabariLEO, utaona kwamba habari haikua kwamba Si lazima Rais asijulishwe, ila habari ni kwamba, "JK AKIRI KWAMBA KARAMAGI ALIMPIGA CHENGA WALIPOKUA LONDON".

Nini maana ya habari hiyo ya gazeti la Serikali. Habari hiyo imeandikwa kisiasa na imewekwa KIDIPLOMASIA kudhihirisha kuwapo kwa tatizo kubwa ndani ya mfumo mzima wa serikali. Ikulu wameamua kuvunja ukimya ili umma ujue kwamba kuna TATIZO.

Katika mazingira ya kawaida, mikataba, makubaliano, uwekezaji, uuzaji mali za umma, nyaraka zake hujadiliwa katika vikao vya awali kabla ya waziri mwenye dhamana kuwasilisha hoja yake katika kikao cha Baraza la Mawaziri kupata baraka ama kukwamishwa. Sasa Leo Ikulu inakiri, utaratibu umekiukwa lakini kwa HILI LA KARAMAGI hakukua na tatizo kwani SI LAZIMA RAIS AJULISHWE NA KWAMBA ALIKUA AKIFAHAMU MCHAKATO. HAta kama hivyo ndivyo, hivi hata katika mazungumzo ya kawaida ya kirafiki, KAramagi alishindwa kumwambia Jk, "Mshikaji unajua leo kuna dili nakwenda kukamilisha na jamaa zetu wa Barrick" na baadaye amwambie, "Nimekwishasaini ile dili na hii ni nakala ukipata mda upitie"... Badala yake, Zitto ndiye anayekuja kutoa taarifa bungeni na kuwaacha mawaziri midomo wazi. Hivi Karamagi ana tofauti gani na KAtibu Mkuu wa UWT, Halima Mamuya aliyefukuzwa kwa kuingia mkataba wa kuuza Majengo ya UWT pale City Ambasador?

Hivi kwanini Watanzania wasiwaamini viongozi wa kisiasa pale Jangwani waliosema kwamba Rais ana ubia na watu katika URAIS wake pamoja na kutamka mara kadhaa kwamba hana ubia na mtu kwani, haiwezekani hata kidogo kwa Waziri kuingia mkataba ambao Rais hajui, BAraza la MAwaziri halina habari na hata Mwanasheria Mkuu naye hana habari, na hapohapo anakwenda kusaini nje ya nchi, tena akiwa na Rais, anasubiri wakati wa mapumziko (sijui usiku au LUNCH TIME) wakati wamekwishaachana na RAis anakwenda kinyemela na kusaini mkataba wake kimya kimya. HAIWEZEKANI HATA KIDOGO.

Hivi kweli Barrick wanavyopenda publicity kwanini hawakuutangaza kutiwa saini kwa mradi wa Buzwagi na badala yake walitangaza kupata hati ya mazingira, miezi mitatu baada ya Karamagi kuingia nao mkataba.
 
ndugu zangu,
huu mkataba ni wa ajabu kwasababu inasemekana Baraza la Mawaziri[Raisi,Makamu,Raisi waZNZ,PM...] walikuwa hawana taarifa na vilevile ulikuwa unasainiwa nje ya nchi.

katika mazingira hayo, USALAMA WA TAIFA walipaswa kumnongoneza Raisi kwamba: Waziri wako Naziri Karamagi, atasaini mkataba na kampuni W, katika gesti X, iliyoko mtaa Y, majira ya saa Z.

Inawezekana kabisa kwamba Raisi hakufahamishwa kupitia Cabinet. Lakini haingii akilini kwamba "SISTIM" haikulijua suala hilo, na kumpa taarifa Raisi na Amiri Jeshi Mkuu.

Hiyo taarifa ya Ikulu ni spinning tu. Tunachopaswa kujiuliza hapa ni kama Raisi aliridhia mkataba huo. Vilevile ni hatua gani Raisi alichukua --kabla na baada ya mkataba kusainiwa.

Ninasema haiwezekani Raisi asiwe na taarifa za mkataba huo. Swali ni: Je, Raisi alimkemea, alimnunia, au alimdharau[spika vs malima] Mheshimiwa Naziri Karamagi?
 
Mimi naona tatizo kubwa zaidi ni pale ambapo waziri anaamua kuondoka na government sill (namaanisha mhuri wa serikali na kwenda nao nje ya nchi halafu tunadhani kuwa taifa hili bado lina usalama .

Ndugu zangu kwa hili kwa kweli hii ni aibu kubwa kwa taifa hili, jk aamue moja kusuka ama kunyoa ila kwa vile alikuwa yupo na kagramagi huenda ameshiriki naye moja kwa moja .
 
Me kinachonivutia ni style ya WALADAU kutoka katika hili korongo. Mitaani tunasema angalao sasa majibu yanaelekea kuendewa tuition. Tatizo ni kuwa waswahili walishasema "MAJI YAKIMWAGIKA HAYAZOLEKI"


Tanzanianjema
 
Kuna Utaratibu wa Rais kuwa Briefied kila asubuhi mambo yote muhimu yaliyotoke/yatakayotokea siku hiyo.Kufahamishwa huko kunakuwa asubuhi kabla ya kuingia Ofisini,mara nyingi hufanywa na Maafisa Waandamizi wa Ikulu.Najua kuwa Utaratibu huo bado upo!Sasa haingii akilini kuona kuwa siku ile ya kusainiwa Mkataba huu wa Buzwagi Mkuu wa Kaya hakufahamishwa!.Haingii akilini kwamba tukio hilo lilikuwa Dharura,kwa sababu Ndg Mwanyika alitoka Dar kumfuata Waziri huko London.Nina wasiwasi kuwa kuna mambo makubwa zaidi ya tunayoyajua yanafichwa.

Leo tunaambiwa kuna Mkataba wa Gasi ya Mkuranga pia umesainiwa!Je? Rais,Bunge na Baraza la Mawaziri wanalijua hili?Hawa watu tunaowapa madaraka kwa mtindo huu watauza mpaka Ardhi yetu kwa wageni bila Ufahamu wetu!Sidhani kama hawa wawekezaji ndio watakuwa ufumbuzi wa matatizo yetu!,kwa mwendo huu tunajiingiza kwenye matatizo na umaskini zaidi,kwani kile kichache tunachojivunia wanakivuna chote,na soon wanaondoka wakituacha watupu na maskini zaidi!
 
Haingii akilini kwako wewe msomi lakini sio kwa asilimia 80% waliotoa ushindi wa Tsunami na hao ndio walengwa kaka. Wanachofanya ni kutumia simple but effective strategies...with some risks though

Organised politiki at its best in the working

Tanzanianjema
 
Kuna Utaratibu wa Rais kuwa Briefied kila asubuhi mambo yote muhimu yaliyotoke/yatakayotokea siku hiyo.Kufahamishwa huko kunakuwa asubuhi kabla ya kuingia Ofisini,mara nyingi hufanywa na Maafisa Waandamizi wa Ikulu.Najua kuwa Utaratibu huo bado upo!Sasa haingii akilini kuona kuwa siku ile ya kusainiwa Mkataba huu wa Buzwagi Mkuu wa Kaya hakufahamishwa!.Haingii akilini kwamba tukio hilo lilikuwa Dharura,kwa sababu Ndg Mwanyika alitoka Dar kumfuata Waziri huko London.Nina wasiwasi kuwa kuna mambo makubwa zaidi ya tunayoyajua yanafichwa.

Leo tunaambiwa kuna Mkataba wa Gasi ya Mkuranga pia umesainiwa!Je? Rais,Bunge na Baraza la Mawaziri wanalijua hili?Hawa watu tunaowapa madaraka kwa mtindo huu watauza mpaka Ardhi yetu kwa wageni bila Ufahamu wetu!Sidhani kama hawa wawekezaji ndio watakuwa ufumbuzi wa matatizo yetu!,kwa mwendo huu tunajiingiza kwenye matatizo na umaskini zaidi,kwani kile kichache tunachojivunia wanakivuna chote,na soon wanaondoka wakituacha watupu na maskini zaidi!

Kisichoniingia akilini, Karamagi alimwambia nini Kikwete masaa yote waliyokuwa kwenye ndege kuwa anakwenda kufanya nini UK?
 
Kisichoniingia akilini, Karamagi alimwambia nini Kikwete masaa yote waliyokuwa kwenye ndege kuwa anakwenda kufanya nini UK?

..alikuwa hajui!

..hapa kuna fumbo kubwa kuhusu issue yote!

..likifumbuka tutastaajabu na kuacha midomo wazi!
 
Na kwa kuwa aliondoka na mihuri, basi alijua alichokuwa anakwenda kufanya huko Ulaya. Halikua ni jambo la kushtukiza hata kidogo kama anavyotaka tuelewe. Hivi unaposainia mkataba 'gesti' house utapata muda wa kuupitia upya kweli kabla ya kuusaini. Je kama kuna kipengele kilibadilishwa in between itakuwaje hapo? Nchi ya kisanii kweli hii
 
Back
Top Bottom