SoC02 Mikakati madhubuti ya kuboresha Sekta ya Kilimo Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Phenol 41

Member
Jul 20, 2022
17
37

Utangulizi


Kilimo ni kitendo cha kuzalisha mazao shambani. Ni mojawapo ya shughuli za mwanadamu zinazomsaidia kupata mazao kwaajili ya chakula na biashara ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku. Nchini Tanzania kilimo ni miongoni mwa shughuli muhimu na inayofanywa na watu wengi nchini, hii ni kwa sababu ya maeneo mengi yanafaa kwa kilimo pia uwepo wa mvua za uhakika kila mwaka.

Mazao yanayolimwa ni yale ya biashara na chakula, miongoni mwa mazao ya biashara ni kama vile pamba, kahawa, chai, pareto, Korosho, Mkonge na Sukari. Mazao ya chakula ni Pamoja na Mahindi, Mchele, Ngano, Mtama,Mikunde, Ndizi, viazi na mbogamboga.

Taswira ya kilimo nchini

Nchini Tanzania wakulima wengi wanatumia majembe ya mikono na yale yanayokokotwa na Wanyama. Kuna watu wachache na makampuni ya wawekezaji wanamiliki zana bora za kilimo ikiwemo matrekta ya kulimia Pamoja na mashine za kuvunia. Uzalishaji wa mazao unakua kadri siku zinavyoendelea japokua nimdogo sana ukilinganisha na nchi zingine. Pamoja na kulima bado serikali inapoteza kiwango kikubwa cha pesa kila mwaka kuagiza bidhaa hizi kama sukari, ngano na mafuta kama inavyoonekana kwenye jedwali Na:1

Jedwali Na:1 mazao yanayo zalishwa kwa kiwango kidogo nchini 2022 (tani)

ZaoMahitaji Uzalishaji wa ndaniupungufu
Sukari655,000370,00285,000
Ngano1,000,00070,288929,712
Mbegu za mafuta650,000300,000350,000
Chanzo: wizara ya kilimo 2022


Picha zikionesha wakulima wadogo wakiwa shambani

vc.jpg




hy.jpg

Chanzo: IPP Media



Changamoto zilizopo katika sekta ya kilimo



1.Uhaba wa mashine na zana duni zinazotumika katika shughuli za kilimo.

Ni wazi kua wakulima wengi nchini Tanzania wanatumia majembe ya mikono na yanayo kokotwa na Wanyama ambayo kwa hakika haviwezi kumudu kulima eneo kubwa litakalotoa mazao ya kutosha. Mashine zilizoingizwa nchini kwa mwaka 2021/2022 hadi April 2022 ni kama zinavyoonekana kwenye jedwali Na 2

Jedwali Na.2: mashine na zana za kilimo zilizoingizwa nchini
jedwali 2.jpg

Chanzo: wizara ya kilimo 2022

2. Uhaba wa mbolea na zilizopo kuuzwa kwa bei ya juu.
Tanzania bado inao uwezo mdogo wa kuzalisha mbolea, mbolea nyingi anayo tumiwa na wakulima ni ile iliyo agizwa kutoka nje kupelekea upatikanaji kua mgumu na kwa bei ya juu ambapo mkulima wa kawaida anapata kiasi kidogo sana cha mbolea ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji yake. Hii inapelekea serikali kupoteza kiasi kikubwa sana cha pesa kila mwaka ili kuagiza mbolea kutoka nje.
Kwa msimu wa kilimo 2021/2022 mahitaji yalikua ni tani 698,262 lakini hadi kufikia aprili 2022 ni tani 436,579 pekee ndizo zilikua zimepatikana huku tani 274,973 zikiagizwa kutoka nje ya nchi, tani 117,900 ni bakaa ya msimu wa 2020/2021 na tani 43,579 ndizo zilitengenezwa nchini huku kukiwa na upungufu wa tani 262,683 za mbolea kwa msimu wa 2021/2022 kama inavyoonekana kwenye jedwali namba 3
Jedwali Na.3: upatikanaji wa mbolea hadi April 2022

jedwali 3.jpg

Chanzo: wizara ya kilimo 2022

3.Ukosefu wa masoko ya uhakika.
Wakulima wengi wanazalisha mazao kwa wingi lakini uhakika wa soko ni mdogo sana, jambo hili linafanya wakulima wengi kuzalisha mazao kidogo wakihofia kutumia gharama kubwa wasije kuingia hasara kwa kukosa wanunuzi. Pia uwepo wa madalali na vipimo visivyo rasmi umekua mwiba mkubwa kwa wakulima ambao wanashindwa kuona faida za kilimo kwa sababu ya maslahi duni yan.rrayopatikana katika kilimo.

4. Ukosefu wa viuatilifu kwaajili ya wadudu waharibifu.
Viwavijeshi, kweleakwelea na nzi wa matunda ni miongoni mwa wadudu waharibifu wanaopatikana nchini Tanzania na wanaathiri sana mazao yanayolimwa nchini. Viuatilifu kwaajili ya udhibiti wa wadudu hawa vinapatikana kwa shida sana hii ni kwasababu viwanda vya kutengeneza nchini ni vichache mno hivyo kufanya wadudu hawa kupunguza ubora wa mazao yanayopatikana shambani

5.Ukosefu wa elimu kwa wakulima wengi.
Wakulima wengi nchini wanalima kwa mazoea hawana elimu ya kutosha juu ya mbegu bora wanazo paswa kutumia, matumizi sahihi ya mbolea kutokana na aina ya udongo wa eneo husika, muda sahihi wa kuanza kilimo katika msimu husika, eneo analoweza kulihudumia kutoka na zana alizo nazo na matumizi sahihi ya viuatilifu.



Mbinu za kimkakati ili kukuza sekta ya kilimo

1.Serikali kupitia wizara ya fedha itoe mikopo kwa wakulima itakayo wasaidia kupata zana bora za kilimo, mbolea Pamoja na viuatilifu kwaajili ya kuua wadudu.

2. Kuwepo na maabara za kutosha za kupimia sampuli za udongo ili kuwasaidia wakulima uelewa wa aina ya mazao wanayopaswa kulima kwa sehemu husika lakini pia aina ya mbolea na kiwango watakachokitumia kutokana na aina ya udongo ya sehemu husika.

3.kuanzishwe viwanda vya kutosha vya kutengeneza mbolea na viuatilifu vitakavyosaidia upatikanaji wa mbolea na viuatilifu vitakavyo jitosheleza kwa msimu husika pia itapunguza gharama za kuagiza kutoka nje ya nchi

4.Kila halmashauri kijengwe kiwanda walau kimoja kikubwa kwaajili ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo au kutengeneza bidhaa mpya. Mfano Halmashauri ya wilaya ya mlele inajihusisha na kilimo cha karanga basi kijengwe kiwanda cha kukamua mafuta kutokana na karanga zinazo limwa hapo. Hii itasaidia upaikanaji wa soko la mazao pia itaondoa utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

5.Kuanzisha skimu kubwa za umwagiliaji zitakazolimwa mazao ambayo yanauhitaji mkubwa kama vile sukari, ngano na mbegu za mafuta

6. Serikali kupitia wizara ya kilimo watatafute masoko ya uhakika duniani kwa mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini, tusiishie tu kuuza mchele na mahindi kwa wakenya na waganda ila tutengeneze bidhaa zinazopata soko duniani kote. Mfano zao la mahindi ni nchi chache sana zinazo nunua mahindi kutoka Tanzania kama inavyoonekana katika jedwali Na: 4
Jedwali Na: 4. Uuzaji wa mahindi nje ya nchi (tani)
jjedwali 4.jpg

Chanzo: mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)



HITIMISHO

Kilimo kisichukuliwe kwa mazoea, ni sekta ambayo inaweza kua mkombozi kiuchumi kwenye jamii yoyote ile. Uandaliwe mpango mkakati wa kukiinua kilimo ndani ya miaka mitano ambapo wizara ya kilimo itengewe bajeti kubwa Zaidi ili kuweza kujenga viwanda kila halmashauri pia iweze kushirikisha watu binafsi walio tayari kuanzisha viwanda iwawezeshe kiuchumi ili waanzishe viwanda kwenye halmashauri zao, halafu mikopo ya pembejeo kwa wakulima itolewe na wakulima wapewe elimu ya kutosha juu ya mazao wanayolima. Ndani ya miaka mitano serikali itakua imetengeneza msingi imara kwenye sekta ya kilimo utakaowafanya wakulima kukua kiuchumi na kukuza pato la taifa.
Ndimi wako phenol 41
 

Attachments

  • jjedwali 4.jpg
    jjedwali 4.jpg
    15.4 KB · Views: 11
Kuna haja ya kuwepo kwa mjadala mpana namna ya kukuza kilimo chetu kiweze kumkomboa kila mwananchi, kwa kukifanya kiwe uti wa mgongo na sii cha kuvunja uti wa mgongo kwa kuendelea kutumia zana za enzi ya mawe ("stone age"). Ndio maana katika makala yangu "Tunaweza kufanya Mapinduzi ya Kilimo Tanzania kwa kulima wakati wa Kiangazi", nimesisitiza sana kilimo cha kisasa cha umwagiliani kwa kutumia teknologia sahihi na rahisi, ambapo mkulima mdogo atamudu kukifanya.
 
Nimependa jinsi ulivyotumia data,changamoto nyingine ni kutotumia data,lol, data zinatupa picha nini challenges zetu kama taifa kwenye kilimo. Data zingeweza kutujulisha tulime nini,kwa wakati gani,etc pia Data zingeweza kutusaidia kuexplore markets ndani na nje ya nchi, nimependa mapendekezo yako...big up Mkuu....
 
karibuni tujadili suala zima la kilimo pia usisahau kuvote uzi huu kwa kugusa alama ya kijani chini ya uzi huu
Andiko zuri mkuu kura yangu umepata .. naomba na wewe usome andiko langu na kupigia kura kwa kugusa hii link
 
Back
Top Bottom