Shuhuda za utajiri utokanao na kilimo Tanzania

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kuna matajiri wakubwa Tanzania ambao utajiri wao waliupatia kwenye kilimo. Kuna ambao ni wakulima matajiri wanaoendelea na kilimo mpaka sasa. Na kuna matajiri walioamua kuingia kwenye kilimo baada ya kugundua kuwa kilimo kinalipa kuliko biashara zao za awali.

Na, kwa mujibu wa huu uzi, kilimo ni pamoja na ufugaji. Anayefuga mifugo na anayelima mazao ya chakula na biashara wote ni wakulima.

Tupe ushuhuda wako.
 
Mzee Tango wa Arusha. Nilishawahi kusoma na watoto wake.

Sijasikia habari zake hivi karibuni. Lakini miaka ya nyuma alikuwa ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa sana mkoani Arusha.

Kuna kipindi alienda kuonana na Waziri Mkuu wa kipindi hicho, Mizengo Pinda, kuishtaki TRA kwa kuyashikilia malori yake 18 na kumsababishia hasara ya bilioni sitini.

Inasemekana utajiri wake aliupatia kwenye kilimo cha vitunguu. Ndiko alikopatia mtaji wa kuanzishia biashara ya usafirishaji mizigo.
 
Anayemiliki milioni mia mbili sitini benki ni tajiri?

Sina tafsiri sahihi ya "tajiri", lakini mwenye kiasi hicho benki si maskini.

Ni taarifa niliyoisikia Juzi za mtumishi wa Serikali mkoa fulani, akiwa ni mtaalam wa kilimo, ni Afisa Kilimo.

Kama inavyofahamika kuwa kila mwaka watumishi wa Serikali wa ngazi fulani wanapaswa kujaza fomu ya Mali wanazozimiliki, huyo naye alifanya hivyo. Alivyohojiwa alivyopata hizo milioni mia mbili sitini, aliwadadavulia kinagaubaga na kuwapeleka mpaka shambani kwake. Anamiliki shamba la mboga na matunda.

Ingawa yupo "mikoani", lakini soko lake ni Dar Es Salaam. Magari huyafuata mazao shambani kwake "mikoani".
 
Mfugaji aliyenunua shamba la milioni mia moja.

Rafiki yangu ana mashamba makubwa mkoa fulani. Mwaka Juzi, aliamua kuuza sehemu ya hayo mashamba.

Mteja aliyeletwa, hakuwa anafania na mtu mwenye uwezo wa kuwa na milioni mia moja. Alikuwa mfugaji. Kumbe anamiliki ng'ombe wa kienyeji zaidi ya mkoa mmoja Tanzania.

Walipokubaliana bei, shilingi milioni mia moja, alitaka kulipa papo hapo shambani. Hela ilikuwa imebebwa kwenye begi.

Kwa kuhofia kutembea na kiasi kikubwa cha pesa, aliwaambia wakakutanikie benki. Ndiko walikoenda kulipana.

Ilikuwa mara yake ya kwanza kumwona mfugaji akiwa na mamilioni mengi ya fedha kiasi hicho. Na huyo mfugaji ambye kabila lake ni Msukuma, alimwomba kuwa akitaka kuliuza eneo jingine, amjulishe ili alinunue.

Tanzania kuna wafugaji ambao japo wanafuga kienyeji, lakini ni matajiri wakubwa sana. Fikiri mtu mwenye ng'ombe zaidi ya elfu moja, huyo si tajiri?
 
Kuna matajiri wakubwa Tanzania ambao utajiri wao waliupatia kwenye kilimo. Na kuna ambao ni wakulima matajiri wanaoendelea na kilimo mpaka sasa. Na kuna matajiri walipoamua kuingia kwenye kilimo baada ya kugundua kuwa kilimo kinalipa kuliko biashara zao za awali.

Na, kwa mujibu wa huu uzi, kilimo ni pamoja na ufugaji. Anyefuga mifugo na anyelima mazao ya chakula na biashara wote ni wakulima.

Tupe ushuhuda wako.
Inategemea mtu na mtu pia eneo pia upepo pia baraka na neema zitokazo kwa aliye juu.
Vinginevyo kilimo ni kamari.
 
Mfugaji aliyenunua shamba la milioni mia moja.

Rafiki yangu ana mashamba makubwa mkoa fulani. Mwaka Juzi, aliamua kuuza sehemu ya hayo mashamba.

Mteja aliyeletwa, hakuwa anafania na mtu mwenye uwezo wa kuwa na milioni mia moja. Alikuwa mfugaji. Kumbe anamiliki ng'ombe wa kienyeji zaidi ya mkoa mmoja Tanzania.

Walipokubaliana bei, shilingi milioni mia moja, alitaka kulipa papo hapo shambani. Hela ilikuwa imebebwa kwenye begi.

Kwa kuhofia kutembea na kiasi kikubwa cha pesa, aliwaambia wakakutanikie benki. Ndiko walikoenda kulipana.

Ilikuwa mara yake ya kwanza kumwona mfugaji akiwa na mamilioni mengi ya fedha kiasi hicho. Na huyo mfugaji ambye kabila lake ni Msukuma, alimwomba kuwa akitaka kuliuza eneo jingine, amjulishe ili alinunue.

Tanzania kuna wafugaji ambao japo wanafuga kienyeji, lakini ni matajiri wakubwa sana. Fikiri mtu mwenye ng'ombe zaidi ya elfu moja, huyo si tajiri?
Yupo msukuma mfugaji....nilimuuzia pikipiki Fekon miaka kadhaa ilopita..
Alitoka nayo Dar anarudi mkoa huku akikagua makundi ya mifugo...kila akituma picha na mifugoye wawezabdhani msanii
 
Mfugaji aliyenunua shamba la milioni mia moja.

Rafiki yangu ana mashamba makubwa mkoa fulani. Mwaka Juzi, aliamua kuuza sehemu ya hayo mashamba.

Mteja aliyeletwa, hakuwa anafania na mtu mwenye uwezo wa kuwa na milioni mia moja. Alikuwa mfugaji. Kumbe anamiliki ng'ombe wa kienyeji zaidi ya mkoa mmoja Tanzania.

Walipokubaliana bei, shilingi milioni mia moja, alitaka kulipa papo hapo shambani. Hela ilikuwa imebebwa kwenye begi.

Kwa kuhofia kutembea na kiasi kikubwa cha pesa, aliwaambia wakakutanikie benki. Ndiko walikoenda kulipana.

Ilikuwa mara yake ya kwanza kumwona mfugaji akiwa na mamilioni mengi ya fedha kiasi hicho. Na huyo mfugaji ambye kabila lake ni Msukuma, alimwomba kuwa akitaka kuliuza eneo jingine, amjulishe ili alinunue.

Tanzania kuna wafugaji ambao japo wanafuga kienyeji, lakini ni matajiri wakubwa sana. Fikiri mtu mwenye ng'ombe zaidi ya elfu moja, huyo si tajiri?
Kama unatambua kuwa ng'ombe mmoja aliyekamilika hauzwi chini ya laki 7 huwezi kuwa na swali kwa mtu ambaye anamiliki ng'ombe elfu 1.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom