Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
Mkuu Masanja chukua tano kwanza.
Ukikaa karibu na wanafunzi wa UDSM ndipo utrakapobaini kuwa wengi wao mawazo yao hayaendi mbali sana. Ukiwasikiliza kwa makini, wanatoa hoja ambazo hazina mashiko. Madai yao yanaweza kuwa ya halali lakini wanashindwa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Wanachoomba ni mikopo na inashangaza sana unakwenda kumkopa mtu, anakuamba hana uwezo wa kukukopesha chote unachotaka kukopa, halafu unamjia juu ukimlazimisha akukopeshe kwa kiwango unachotaka wewe na si kulingana na uwezo wake.
Bodi ya mikopo imetengenezwa kama namna fulani ya revolving fund. Wapo wanafunzi ambao walipaswa kuwa wanalipa madeni yao hivi sasa na fedha hizo zingetumika kuwakopesha wanafunzi wengine, lakini nenda ukaulize kiasi gani cha fedha ambacho kilipaswa kuwa kimerejeshwa lakini hakijarudi, utashaa.
Katika madai yao ya sasa wanataka kubadilishwa kwa sera-hivi sera inabadilishwa ghaflaghalfa tu? Walishaambiwa na Maghembe kuwa hicho si kitu cha kukaa na kuamua tu, inahitaji mashauriano ya madau wote, hawataki kusikia. ndio wanaweza kusema kuwa madai hayo yamekuwa ya muda mrefu ambao ungetosha kulifanyia mabadiliko jambo hilo, lakini kweli lazima imesaidia kutatua matatizo yao?