robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 740
- 1,214
Tufahamishane kwamba, ni kweli takribani nusu ya wanafunzi wa SUA wameshindwa kuhitimu ktk mahafali ya mwezi Novemba 2023 kama ilivyo kawaida ya miaka yote, na wanatakiwa kurudia mitihani baada ya mwaka mzima wa kusubilia mitihani. Sababu kubwa ni maamuzi mabaya ya viongozi wa chuo. Waliamua kuingiza ubunifu mpya usiyokuwepo chuo chochote duniani.
Viongozi wa SUA wamefuta muda maalumu wa mitihani ya marudio tofauti na taratibu za vyuo vikuu. Sababu kubwa iliyotolewa na uongozi kwa wahadhiri ni kwamba ili wapate muda wa likizo. Uamuzi huu haukupitia majadiliano yoyote, ni maamuzi ya viongozi watatu wa chuo. Hakuna mwanataaluma anayeelewa faida ya mabadiliko hayo, maana miaka yote wanakwenda likizo, kila mtu kwa muda wake.
Hili ni tatizo kwa watu wote wanaotegemea kujiunga na chuo hiki na walipaji wa ada. Ukijiunga na SUA huna uhakika wa kumaliza chuo kwa miaka iliyopangwa.
Sasa, wanafunzi wanadaiwa kulipia ada ya shilingi elfu 30 kwa mitihani ya marudio, ikimaanisha mitihani ya marudio imekuwa ni biashara ndani ya chuo. Yaani chuo Kinajiongezea mapato kwa mitihani ya marudio bila bodi ya mikopo au walipaji wengine kutaarifiwa. Wanafunzi wanatakiwa kulipia wakati ni wanafunzi halali na wana usajili wa masomo kwa mwaka mzima.
Nje ya chuo, viongozi hawasemi ukweli wa uamuzi huu, na kuna tetesi za kuzunguka kwa wabunge wasilisemee mjengoni. Wanajivunia kuwa una lengo la kuinua elimu, sijui kwa njia gani inayojulikana kwao tu? Waacheni wanafunzi wakajitafutie maisha mtaani badala ya kuwalazimisha kulipia gharama za kutengeneza.
Hili ni zigo lako Mh. Waziri, Mkenda na TCU, ambao ndo wadhibiti ubora. Wabunge mbaneni waziri huko Bungeni aseme nini kinaendelea ktk taasisi za wizara yake. Za chinichini zinasema viongozi wanafanya lobbying kwa wabunge ili lisisemwe, lakini kwa mtindo huu tuliosoma tunawatetea wanafunzi. Wote tumesoma vyuo vikuu, hatukukutana na usanii huu.