Keneth Nollo: Serikali ifute ada Vyuo Vikuu

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Akichangia bungeni mbunge Keneth Nollo, amesema serikali ifikirie kuondoa ada kwa wanafunzi wa chuo nchini sababu umasikini na mkubwa na wengi hawawezi kumudu.

Badala yake wanafunzi wa nje pekee ndio wawe wanalipa ada.

View attachment 2809501
Hakuna serikali, kuna genge walaji, wezi wa kura, wahuni, wahujumu uchumi , wauaji, nk nk
 
Tupia walau kapicha ka mbunge, maana ameongea kero inayosumbua nyakati kama hizi. Hawajui watanzania wengi vipato vyao ni kuunga unga tu, wanapotumia kigezo cha uwepo wa wazazi wamejaribu kujiuliza status zao kuweza kugharimia ada na gharama za mwanafunzi ambazo zinafika hadi milioni nane kwa mwaka.​
 
Nimeweka video tayari
 
Ukiweka siasa kando,
Huo mpango kwa serikali yetu ni almost impossible, hatuna hizo fedha, ili kugharamia hizo ada na vitu ka hivyo serikali itabidi kubuni vyanzo vipya na ndio hivyo sasa zitakuja kodi za kunyanduana bure
 
Watanzania wengi ni kama wamekata tamaa, wanahisi ni jambo lisilo wezekana kabisa

Na hawaji na mpango wa kuishauri serikali ifanye nini ili mpango kama huo uweze kufanikiwa

Comments zao zitasomeka
Mafisadi
Kwa serikali ipi
Haiwezekani
Hakuna pesa hiyo
Zitaibuka kodi kibao
Nk

Ni watu ambao wamejaa lawama kuliko kutafuta njia ya kutatua shida zinazo wahusu Au kuwa sumbua

Kwa namna hii una zani CCM chama changu kitatoka madarakani kama mnavyo waza?

Mtaji wa kiongozi yoyote ni ujinga wa anao waongoza, endeleeni kujipofusha, endeleeni kuwa wajinga...! Maana ndio mtaji wa chama changu
 
Akichangia bungeni mbunge Keneth Nollo, amesema serikali ifikirie kuondoa ada kwa wanafunzi wa chuo nchini sababu umasikini na mkubwa na wengi hawawezi kumudu.

Badala yake wanafunzi wa nje pekee ndio wawe wanalipa ada.

View attachment 2809501
Hii inawezekana kabisa,ni serikali tu kukusudia,kuwa na nia njema kwa watu wake na kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za taifa.
 
Mbunge wa Bahi (CCM) Beneth Nollo ameshauri Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini na badala yake kuwakopesha fedha ya chakula ili watoto wengi wanaotoka katika familia masikini waweze kusoma.

Ombi hilo linakuja wakati Serikali ikiwa imeondoa ada kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita na kupeleka ruzuku ya kila mwaka kwa ajili ya uendeshaji wa shule hizo.

Nollo ameyasema hayo leo Ijumaa Novemba 10, 2023 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2024/25.

Chanzo: Mwananchi

View: https://www.instagram.com/p/CzdyUzktJnz/
 
Sijaona faidi yeyote ya kuondoa ada,infact Ada imeongezeka kwa kuwa michango amounts to 85,000/= not of course forgetting michango ya mitihani na ream.The whole thing ni uhuni tu unayoendelea.
 
Serikali tayari inalipa mishahara ya wahadhiri na gharama nyingine za uendeshaji vyuo vikuu vya umma, kwa nini sasa wanafunzi waliodahiliwa hadi vyuo vikuu vya umma nao washindwe kusoma kisa kukosa pesa ya ada na kujikimu?​
Wafute ada vyuo vya umma na kuondoa mikopo vyuo binafsi
 
Ukiweka siasa kando,
Huo mpango kwa serikali yetu ni almost impossible, hatuna hizo fedha, ili kugharamia hizo ada na vitu ka hivyo serikali itabidi kubuni vyanzo vipya na ndio hivyo sasa zitakuja kodi za kunyanduana bure
Hii kauli ya "hatuna pesa"unaitoa wapi mkuu!?mbona matumizi na pesa zinazopotea kutokana na Mianya ya rushwa ni nyingi sana!?
Kimsingi hili suala linawezekana tena sio TU kusoma Bure Bali pia kupewa meals and accomodations allowances ili kuwafanya wasome kwa ufanisi kumbuka Hawa wote hurudi na kuchangia maendeleo ya nchi baada ya kupata ujuzi mbalimbali so hakuna sababu ya kuwatoza pesa Bali kuwawezesha ili wazalishe kwenye nchi
 
Mkuu, unahisi kwann Marekani hadi leo watu wanasoma kwa pesa sio bure?

China na Ujamaa wake wote watu wanasoma kwa pesa,
Usidhani kusomesha chuo itakuwa ni easy, kwa hio ukiweka chuo free hio mianya ya rushwa itaisha ? Ni bora hizo pesa zitumike kuwekeza kwenye industries na huduma nyingine through PPP ili zizalishe ajira nyingi za wahitimu, ila sio kusomesha watu bure,

Kusomesha bure watu chuo kikuu ni akili za kilofa, boresha mikopo, tengeneza mazingira ya ajira nyingi kisha watu walipe pesa hizo bas, ila sio kuweka bure kabisa mkuu
 
Huwa nakasirika sana nikiona watu wakiichukulia America kama a model country,it is not.America is modelled on Satanic principles:survival for the fittest,hakuna utu America mkuu,everybody fends for himself.

Labda ulikuwa hujui ,America sio Republic as many people are made to believe,it is a corporation or if you like a private company.Sasa a Private Company au Corporation ikulipie ada ya Chuo,hiyo kampuni inapata faida gani.Kama wewe ni a small
mind,naamini hutanielewa,but those are the facts.America is not what you believe it is.
 
Back
Top Bottom