Mgomo kesho unafanyika chuoni hapo kutokana na ukandamizaji unaofanywa na menejimenti ya chuo kwa wanafunzi chuoni hapa. Prof mmoja anaitwa Mlacha ndo chanzo cha matatizo yote, hana utu, yeye kwake pesa ndo utu. Wanafunzi wamechoshwa na ukandamizaji wake. Hashauliki huyu bwana. Sasa kazi inaanza kesho na ole wake watoto wa maskini wana hasira sana nae.
Chuo cha JK nako wanagoma, au ndio mzimu wa Mwankupili?
Sasa kwa nini msiibane bodi ya mikopo.
Kumbe Mlacha hapokei pesa, basi mgewagomea hao wahasibu wanaojali sana kupokea
Habari ya vyumba inahusikaje direct na Mlacha? je hakuna mgawanyo wa madaraka hapo Udom kiasi ambacho VC anaingia direct katika sakata la vyumba? Nilidhani mngeenda kushtaki kwake kwa vyumba ni soo! Kwani ni lazima mlipie chumba malipo sawa na malipo ya udsm?
Kuhusu Malipo ya ada, ingekuwa vizuri kama chuo kingekubali malipo ya awamu, lakini na Mlacha anaingiaje kwenye hili hadi mumkomeshe?
Watoto jaribuni kujua sheria na kuzifuata, hii migomo migomo hii itawapeleka pabaya....... sio lazima mgomo ili muonekane na nyie ni wanafunzi wa chuo!!!
Nimessikia wamegoma leo
Namuonea huruma huyu waziri wa hii wizara kwani kuna mgomo mwingine wa TAHLISO unakuja mwezi huu
Si hobby Shy hapana ni kuonyesha ni kiasi gani wajieleze kwa kuwa wakijieleza kwa njia ya kawaida hakuna anayesikiliza kwa kuwa viongozi wetu wamejaa dharau na kupandisha mapega juu kwa majivuno.Siku hizi watanzania wana hobby ya kugoma
Mgomo kesho unafanyika chuoni hapo kutokana na ukandamizaji unaofanywa na menejimenti ya chuo kwa wanafunzi chuoni hapa. Prof mmoja anaitwa Mlacha ndo chanzo cha matatizo yote, hana utu, yeye kwake pesa ndo utu. Wanafunzi wamechoshwa na ukandamizaji wake. Hashauliki huyu bwana. Sasa kazi inaanza kesho na ole wake watoto wa maskini wana hasira sana nae.
Kwani waziri ana shida gani? Tuwaonee huruma watoto wetu wanaokosa elimu na kunyanyasika kutokana na mifumo mibovu. Pamoja na kwamba kamwe siungi mkono mgomo wa aina yoyote, nadhani wakati umefika kwa viongozi katika vyuo vyetu kupewa mafunzo madhubuti kuhusu namna ya kusimamia mifumo ya elimu ya juu, maana hii ndiyo chanzo cha vurugu zote. Kila wakati wanafunzi wanagoma, zinatumika mbinu za "zima moto" kutatua tatizo kwa muda tu, na baadae yaleyele yanarudiwa tena kama si chuo hichohicho, basi chuo kingine!
Wana haki kabisa kugoma.
Kama hawatendewi haki zao za msingi wanazo dai njia sahihi ni kugoma tu.