Migogoro ya wakurugenzi na wakuu wilaya (DC) na mikoa (RC) haitaisha kwasababu zifuatazo

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
naomba kutumia mfano wa makinda ya ndege au watoto wa nguruwe!

ukipita kwenye banda ukakuta pako kimya ujue vinanyonya!

kila kimoja kinanyonyo lake mdomoni kinakamua!

Hivi ndivyo ilivyo kwenye vyeo vinavyogongana maslahi kama hivi.
TWENDE PAMOJA KWA SABABU ZIFUATAZO!

Vyeo hivi vya Mkurugenzi na RC vina mgongano mkubwa sana wa kimaslahi, nashauri viandaliwe utaratibu mwingine ikiwezekana cheo kimoja kifutwe ili kuondoa mgongano wa maslahi kwasababu!

Wakurugenzi ni wasimamizi wakuu wa watendaji katika eneo husika! Wakurugenzi ndiyo wenye wataalamu katika eneo husika, wakurugenzi ndiyo mikono ya serikali na vitendea kazi!,wakurugenzi siyo mwanasiasa ingawa wanatoka kwenye chama cha siasa!

Tofauti kubwa iliyopo kwa RC&DC ni hivi!

RC/DC ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika eneo, ni Icon ya serikali hasa kwenye masuala ya Kiitifaki (protocol)! Ni auxiliary leader katika eneo! Mikono yake mikubwa ni Polisi peke yake! Kwasababu wataalam mpaka migambo wote ni wa wakurugenzi!

Yaani RC/DC akitaka kula peke yake ni kwenye madili haramu ya kipolisi!

Nje ya hapo RC na DC hawezi kula bila mikono na baraka ya Mkurugenzi! Maana mambo yote ya dokomenti yako chini ya Mkurugenzi!

Hivyo tukirudi kwenye sakata la Mwanza!
HAKUNA MWEMA PALE lakini SHIDA Ni ule ulaji UMELIWAJE!

Mkurugenzi anaweza kutusua dili peke yake na likaisha bila msaada wa RC/DC
Na hili ndiyo maana wakurugenzi wanaonekana ni wabaya kila siku!

Mkurugenzi siyo mwanasiasa bali ni mtaalam! Hivyo kula yake haihitaji blaah blaah na makamera!

UKIONA ENEO HALINA MGOGORO UJUE MKURUGENZI NA RC/DC WANAKULA SAHANI MOJA!

INJE YA HAPO MKURUGENZI AKIMWAGA MBOGA DC ANAMWAGA UGALI!

Hivi vyeo ni mzigo tunaoumia ni sisi wananchi kulipa kodi!

Bila katiba mpya hawawezi kuvifuta hivi vyeo kwasababu cheo cha ukurugenzi ndicho kinachoiba kura, na cheo cha u-dc/Rc ndicho kinachobeba masanduku ya kura!
 
Mi naona hawafanani hata maofisini watu wanagombana kwa vile watu hawapataki by nature..

Bora wangekuwa wanachagua angalau watu wanaendana na kuwapa uongozi sehemu moja .
 
Back
Top Bottom