Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 89

Kupitia mlango wa nyuma, kulikuwa na gari lake, akampakiza na kuondoka naye. Safari ilikuwa ndefu na walipofika sehemu iliyoonekana kuwa na takataka nyingi, akasimamisha gari lake na kumwangalia Fareed aliyekuwa hoi japokuwa nguvu zilianza kumjia.

“Nisamehe tu! Shetani aliniingia. Amekuwa akinitesa sana katika mchezo huu, uliponiambia shida yako, nilizidiwa kabisa, naomba unisamehe,” alisema Padri Luke huku akimwangalia Fareed aliyekuwa akilia tu.

“Nitakuua! Nitakuua padri!” alisema Fareed, akaufungua mlango na kuteremka, hakupiga hatua nyingi, akadondoka na kupoteza fahamu. Padri Luke akaliwasha gari lake na kuondoka mahali hapo huku akimwacha Fareed akiwa hoi. ***

Bado bilionea Keith alikuwa kwenye penzi la dhati na msichana Maria, moyo wake ulichanganyikiwa, ulikufa na kuoza, hakutaka kusikia kitu chochote, kwake, msichana huyo alikuwa kila kitu.

Alitumia kiasi kikubwa cha pesa kwa msichana huyo, hakutaka kabisa kumuona akipata tabu ya aina yoyote ile. Alimpenda, alimpeleka nchini Ufaransa, Italia, Dubai na sehemu nyingine nyingi kwa ajili ya kula naye maisha.

Msichana huyo hakutaka kuleta uvivu kitandani, alifanya kila linalowezekana kumchanganya mzee huyo, alijua kucheza na kiuno chake, alijua kucheza na mdomo wake uliomchanganya mzee huyo na kuona dunia yote ilikuwa yake.

Maria hakurudi nchini Nigeria, aliendelea kubaki nchini MArekani huku akiendelea kutanua na mwanaume huyo. Penzi likamchanganya mno Keith, wakati mwingine hakuwa akifanya kazi zake, alitamani sana kuendelea kuwa na mwanamke huyo kwani kila alipomuacha hata kwa saa tano, alihisi kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akiliiba penzi lake.

“Have you ever seen collossium?” (Umewahi kuliona Collessium?) aliuliza Keith.
“I’ve just seen it but I’ve not touched it!” (nimewahi kuliona lakini sijawahi kuligusa) alijibu msichana huyo.

“Are you serious baby?” (kweli bebi?)
“Yeah!” (ndiyo)
“I want to take you there!” (nataka nikupeleke huko)
“I real want to touch it,” (natamani sana niliguse) alisema msichana huyo.
 
SEHEMU YA 90

Collossium lilikuwa jengo kubwa la kizamani lililokuwa Roma nchini Italia. Jengo hilo ni miongoni mwa majengo makubwa ya zamani ambayo Waroma walikuwa wakiyatumia kwa ajili ya michezo na kuwaua mateka wao kwa kuwataka kupambana na simba.

Lilikuwa jengo la kutisha, lililomwaga damu za watu wengi miaka ya nyuma kipindi cha mtawala Julius Caesar. Kila mtuu katika kipindi hicho alitamani kuliona jengo hilo lililokuwa na historia kubwa na ya kutisha.

Kwa mtu kama Keith, kwa kuwa alimpenda sana Maria akaona kwamba kumpeleka katika jengo hilo na kuliona jinsi lilivyokuwa ingemfanya msichana huyo kufurahia. Hakutaka waendelee kukaa nchini Marekani, siku mbili mbele wakapanda ndege na kuelekea nchini Italia.

Walichukua saa kumi na tano kufika huko ambapo wakachukua chumba katika Hoteli ya Pretorita. Usiku ulikuwa ni wa mahaba tele, walishikana hapa na pale, walifanya michezo yote ambayo wapenzi walitakiwa kufanya wawapo faragha.
Kwa Maria, alifanya kama siku nyingine, alimuongezea mautundu kwa ajili ya kumpagawisha mzee huyo aliyekuwa tayari kufanya kitu chochote lakini si kumuacha msichana huyo mrembo.

Alimchanganya mno kitandani, moyo wa Keith ukazidi kumpenda Maria kiasi kwamba akawa hajiwezi kwa msichana huyo.

Siku iliyofuata wakaelekea katika jengo hilo. Maria hakuamini, alizoea kusoma historia ya jengo hilo kubwa lakini siku hiyo alikuwa akiliona kwa macho yake na kuligusa. Walikaa huko kwa dakika arobaini na tano ndipo wakaondoka kurudi hotelini ambapo kama kawaida mchezo wao ukaanza upya.

Walichoka, walipomaliza, wakaondoka na kwenda chini kabisa kulipokuwa na mgahawa, wakaagiza chakula na kuanza kula. Wakiwa huko, macho ya Keith yakatua kwa mtu ambaye alimfahamu kabisa, alikuwa bilionea mwenzake kutoka nchini Hispania, Jose Mendoza.

Wakasalimiana, kama alivyokuwa yeye, hata huyo Mendoza naye alikuwa hivyohivyo, mtu wa wanawake wadogo ambapo alitumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuuridhisha moyo wake.
“Nakuona umekaa na mtoto mkali,” alisema Mendoza huku akimwangalia Keith.
 
Back
Top Bottom