Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

Leo jumapili tumalize hii tuanze nyingine itapendeza
 
Katika hadithi ambazo hazinitii uvivu kusoma ni zako shunie kwa sababu huna longolongo. Na unakuwa mkweli kabisa.arosto ni adimu.asante
 
Katika hadithi ambazo hazinitii uvivu kusoma ni zako shunie kwa sababu huna longolongo. Na unakuwa mkweli kabisa.arosto ni adimu.asante
Asante sana mamy ila ipo moja ya shigongo ina arosto siku moja moja lakini toka mwanzo nilitoa taarifa niliwaambia watu mbele itakuwa na arosto sababu bado haijaisha
 
Asante sana mamy ila ipo moja ya shigongo ina arosto siku moja moja lakini toka mwanzo nilitoa taarifa niliwaambia watu mbele itakuwa na arosto sababu bado haijaisha
Nakupendea hapo chochote kile huwa unatujulisha.
 
SEHEMU YA 07

Walihitaji kufahamu ukweli. Taarifa zilisema kwamba mwanaume huyo alikaa hotelini kwa siku nne, na siku zote hizo alikuwa akilala na mwanamke hotelini lakini mpaka muda huo walikuwa wamefanikiwa kuzungumza na wanawake watatu tu, kulikuwa na mmoja alibaki, alikuwa nani? Walihitaji kumfahamu msichana huyo.

Wakaelekea mpaka hotelini na kuwauliza wahudumu. Wengi walikumbuka kwamba siku ya nne mwanaume huyo aliingia na msichana aliyekuwa amevalia nikabu na suruali ya jinsi, alikuwa na shepu bab’ kubwa na nyuma alionekana kujazia hasa, aliingia na bilionea huyo ndani ya chumba kile lakini hawakumuona alipokuwa ametoka, walihisi kwamba huyo ndiye alifanya mauaji.

“Ana muonekano gani?” aliuliza polisi.
“Ni mrefu, kwa muonekano wa macho yake, anaonekana ni mzuri sana, halafu anatembea kwa madaha kama twiga mbali na hayo, mwanamke huyo ana bomba moja kubwa sana kwa nyuma,” alijibu mhudumu mmoja wa kiume.

“Bomba ndiyo nini?”
“Kalio! Kajazia sana.”
“Na alipotoka hamkumuona?”
“Ndiyo! Ila alikuwa naye hotelini!”
Mpaka hapo polisi wakapata uhakika kwamba mtu aliyemuua biliona huyo alikuwa mwanamke ambaye wakati akiingia ndani na bilionea huyo alijitambulisha kwa jina la Victoria. Walitaka kumfahamu msichana huyo, baada ya kuondoka, alielekea mahali gani, na kama hakupitia pale mapokezi, alipitia wapi?

“Na hakuna mtu anayeweza kupitia mlango wa nyuma?” aliuliza polisi.
“Hakuna! Mlango wa nyuma ni kwa ajili ya wafanyakazi tu, tena inabidi uingize namba za siri ambazo zinajulikana kwa wafanyakazi tu,” alijibu msichana mmoja.
Waliwahoji wafanyakazi kadhaa ndani ya hoteli hiyo, kila mmoja alimwambia alichokuwa akikifahamu kuhusu kifo cha bilionea huyo. Wengine wakahisi kwamba alijiua, kwamba aliingia ndani ya chumba kile na kujimaliza mwenyewe kwa kuwa tu alikuwa na mawazo mengi kuhusu mkewe aliyefariki miezi mitatu iliyopita.

Hilo halikuingia akilini mwa polisi, walijua kabisa kulikuwa na mtu aliyemuua bilionea huyo na walihisi kabisa mwanamke huyo wa mwisho aliyeingia naye ndiye aliyefanya mauaji hayo.

SEHEMU YA -06

Walipokwenda mapokezini na kuangalia wateja walioingia, wakaliona jina la mwanaume huyo, aliitwa Belleck Peter, bilionea mkubwa aliyekuwa akimiliki kiwanda cha karatasi na viwanda kadhaa vya kutengeneza mbao vilivyokuwa nchini Marekani.

Kila mtu alishangaa, hawakuamini kama mtu aliyeuawa ndani ya chumba kile alikuwa Belleck. Alijulikana dunia nzima kutoka na utajiri wake mkubwa wa dola za Kimarekani bilioni 7 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 14, aliheshimika na watu wengi walimuita kwa jina la Golden Angel ‘Malaika wa Dhahabu’ kwa jinsi alivyokuwa akiwasaidia watu wengi, hasa vituo vya watoto yatima na masikini waliokuwa wakilala mitaani.

“Is this Belleck I know?” (huyu ni Belleck ninayemfahamu?) aliuliza polisi mmoja huku akionekana kushangaa.
“Yeah! What has happened?” (ndiyo! Hivi ni kitu gani kimetokea?) aliuliza polisi mwingine.

Hakukuwa na aliyejua, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuwatafuta wasichana wote waliokuwa wamelala naye kwani kwa taarifa walizozikuta hotelini hapo ni kwamba tangu Belleck afike katika hoteli hiyo, kazi yake kubwa ilikuwa ni kubadilisha wanawake tu.

Msichana wa kwanza alikuwa Natasha, alichukuliwa kutoka katika mawindo yake ya usiku, wa pili alikuwa Stella na wa tatu alikuwa Neyonce. Wote hao walikuwa wakijiuza mitaani na mtu ambaye walifanya naye biashara yenye malipo makubwa alikuwa mwanaume huyo.

Kila mtu kwa wakati wake wakaingizwa ndani ya chumba cha mahojiano na kuanza kuulizwa kuhusu msichana huyo. Hakukuwa na aliyejua, kitu pekee walichokuwa wakikifahamu ni kwamba walinunuliwa na mwanaume huyo, wakafanya naye mapenzi na kisha kuondoka zao baada ya malipo kufanyika.

“Alors rien n'est arrivé ,” (kwa hiyo hakuna kilichotokea?) aliuliza polisi kwa kutumia Lugha ya Kifaransa.
“Rien ne se passe que le sexe,” (hakuna kilichotokea zaidi ya ngono)

SEHEMU YA 05

Zilisikika kelele za mwanamke kutoka ndani ya chumba kimoja kilichokuwa katika Hoteli ya Melkizedek iliyokuwa ndani ya Jiji la Marseille nchini Ufaransa. Watu wote waliosikia sauti hiyo walishtuka, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, kwa jinsi sauti hiyo ilivyosikika, haikuonekana kuwa ya amani hata kidogo, ilionyesha kabisa kwamba kulikuwa na kitu kikubwa kilitokea.

Wateja wengine waliokuwa katika vyumba vingine wakatoka, walitaka kujua ni kitu gani kilichokuwa kimetokea. Walipotokea ukumbini, macho yao yakatua kwa msichana aliyekuwa mhudumu ndani ya hoteli hiyo akiwa amekaa pembeni kabisa akilia huku akitetemeka kwa hofu kubwa.

Hakukuwa na aliyejua kitu kilichomfanya msichana huyo mrembo kuwa katika hali hiyo. Wakamsogelea kwa lengo la kumuuliza lakini hakujibu kitu, alichokifanya ni kuwaonyeshea chumba kilichokuwa mbele yake ambapo baada ya watu kuufungua mlango wa chumba hicho, macho yao yakatua katika maiti moja iliyokuwa sakafuni.

Kila mmoja alishtuka, hawakujua ni kitu gani kilichokuwa kimetokea. Harakaharaka simu ikapigwa kwenda kwa polisi na kwa meneja wa hoteli hiyo ambapo baada ya meneja kufika, akamuuliza msichana huyo ni kitu gani kilitokea lakini akawaambia hakuwa akijua, alimpelekea mteja kahawa lakini akakutana na maiti hiyo.

Baada ya dakika chache polisi wakafika mahali hapo. Kitu cha kwanza kilikuwa ni kuzungumza na msichana huyo ambaye maelezo yake alisema kwamba alikuwa na utaratibu wa kumpelekea kahawa mteja huyo kila inapofika jioni lakini kitu cha ajabu kabisa, jioni ya siku hiyo akakuta maiti ya mwanaume huyo ndani ya chumba hicho.

Kitu cha kwanza walichokitaka ni kumfahamu mtu ambaye alikuwa ndani ya chumba hicho na mwanaume huyo ambaye hawakujua alikuwa nani kwani alichomwa visu kadhaa shingoni mwake, damu nyingi zilimtoka, nyingine zikauziba uso wake na pale alipoanguka, aliburuzwa na hivyo kufanya michirizi ya damu kuonekana sakafuni.

MICHIRIZI YA DAMU-04

Taarifa hiyo ikawekwa kwenye mitandao ya kijamii na kutangazwa sana katika vituo vya televisheni na radio. Kila mtu aliposikia habari hiyo alishangaa, hawakuamini kama bilionea Keith aliuawa ndani ya piramidi nchini Misri kwani alikuwa mtu mwema ambaye kila mtu alijua kwamba angeishi miaka mingi kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watu masikini.

Serikali ya Marekani haikutaka kukubali, mawasiliano yakafanyika kwenda nchini Misri na kuwaambia kwamba wafanyaje kila linalowezekana mpaka muuaji huyo apatikane, kama walikuwa na uwezo wa kwenda sehemu yoyote ile, ilikuwa ni lazima mwanamke huyo akamatwe.
Lilikuwa ni agizo kubwa na gumu, hawakujua mahali alipokuwa muuaji hivyo polisi kwenda kuulizia katika piramidi hilo na kuambiwa kwamba bilionea huyo alikuwa na mwanamke wa Kinageria aliyeitwa Maria Ogabugu.

“Huyu mwanamke ndiye anayetakiwa kutafutwa na kupatikana haraka iwezekanavyo,” alisema kamanda wa jeshi la polisi jijini Cairo.

“Sawa mkuu!” Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuifunga mipaka yote ya nchi hiyo, uwanja wa ndege kukawekwa ulinzi wa uhakika, sehemu ya kivuko kwa kupitia katika mfereji wa Suez napo kukawekwa ulinzi mkubwa, kila kona, mpaka bandarini kote huko ilikuwa ni kulindwa kwa nguvu zote na kulipokuwa na askari wachache, wakaongezwa wengine kuhakikisha huyo mwanamke anayejulikana kwa jina la Maria Ogabugu hapiti kuondoka nje ya nchi hiyo. Iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumatwa na kufikishwa katika mikono ya sheria.

Je, nini kitaendelea?
Je, mwanamke huyo ni nani na kwa nini ameua?

MICHIRIZI YA DAMU-03

Akaangalia kwenye kompyuta ile kwa lengo la kujiridhisha, kile alichoambiwa ndicho alichokiona kwamba bilionea huyo aliingia na mwanamke aliyejulikana kwa jina hilo ndani ya piramidi hilo.

Hawakujua mwanamke huyo alikuwa wapi kwani walikuwa na uhakika kwamba yeye ndiye aliyemuua Keith na kisha kukimbia.
Wakawasiliana na polisi ambapo baada ya dakika kadhaa wakafika na kuingia ndani ya piramidi lile. Wakaelekea mpaka kule kulipokuwa na maiti ile kisha kuiangalia. Ilionyesha kwamba hakuuawa muda mwingi uliopita, na hata kama muuaji alikimbia, hakuwa amefika Cairo.

Wakaupiga picha mwili ule kisha kuubeba kwa lengo la kuondoka nao ila kabla hawajaondoka, wakaona kipande cha karatasi kikiwa chini, kilikuwa kimezibwa na mwili ule, wakakichukua kikaratasi hicho kilichoandikwa kwa maneno machache kwa Kifaransa yaliyosomeka C'est fait yakiwa na maana ya kukamilika kwa jambo au ‘done’ kwa Lugha ya Kiingereza.

Hilo likaibua maswali mengi, hakukuwa na mtu aliyejua maana ya neno lile lililoandikwa. Mwili ukachukuliwa na kupelekwa hospitali ambapo familia yake ikapigiwa simu na kuambiwa kile kilichokuwa kimetokea.

MICHIRIZI YA DAMU-02

Wakaingia mpaka ndani, wakaanza kumulika huku na kule, wakaelekea kule mwanamke yule alipokwenda huku wakiwa makini kuangalia chini. Kama alivyosema mwanamke yule ndivyo walivyokuta, macho yao yakatua katika mwili wa mwanaume mmoja uliokuwa chini, ulichomwa visu mara tatu kifuani na tumboni, mbali na hivyo, maiti yake iliburuzwa na kuachwa michirizi ya damu pale chini.

Kila mmoja alishtuka, hawakuamini kile kilichotokea, ilikuwaje mwanaume huyo auawe ndani ya piramidi hilo halafu muuaji asionekane? Kitu cha kwanza kabisa, hawakuigusa maiti ile, wakatoka ndani na kuelekea katika kompyuta zao na kuangalia orodha ya watu walioingia ndani ya piramidi lile dakika chache zilizopita kwani hata maiti ile ilivyoonekana, haikuonekana kama iliuawa muda mrefu uliopita.

“Mmeangalia jina lake?”
“Hapana!”
“Hebu kampekueni, mnaweza kuona hata kitambulisho,” alisema mwanaume aliyeshika kompyuta mpakato na hivyo walinzi hao kurudi ndani ya piramidi lile huku watu wengine wakiwa nje na idadi kubwa ya watu ikizidi kuongezeka.

Walipoingia humo, wakampekua mfukoni na kukuta ‘business card’ iliyomtambulisha kwa jina la Benjamin Keith, mwanaume wa Kimarekani aliyekuwa akimiliki kampuni kadhaa ikiwemo kampuni ya mavazi ya Cotton Keith.

“Kumbe ni Keith!” alisema mwanaume mmoja kwa mshangao.
“Ndiye nani?”
“Yule bilionea wa Kimarekani!”
“Unamaanisha yule mwenye utajiri wa dola bilioni kumi na mbili?” aliuliza mlinzi mwingine.

“Ndiyo!”
“Mh! Hebu nione hiyo kadi.” Akakichukua na kuanza kukiangalia, kama alichokiona mwenzake na yeye alikiona hivyohivyo. Kila mmoja alishangaa, hawakuamini kile walichokuwa wakikiona, waliwafahamu sana matajiri, kila kona walipokuwa wakienda, walikwenda na walinzi wao, ilikuwaje Keith aende huko peke yake mpaka kuuawa? Kila walipojiuliza wakakosa majibu.

Wakatoka nje wakiwa na ile kadi na walipomuonyeshea jamaa aliyekuwa na kompyuta, akaangalia jina lile, akagundua kwamba Keith alikuwa ameingia ndani ya piramidi lile na msichana, mrembo aliyeitwa kwa jina la Maria Ogabugu aliyekuwa na asili ya Nigeria.
“Aliingia na mwanamke humu ndani,” alisema jamaa huyo.
“Hebu tuone.”

MICHIRIZI YA DAMU 01- Nyemo Chilongani

GIZA, Misri
Zilisikika kelele kutoka ndani ya piramidi moja lililokuwa katika Mji wa Giza uliokuwa nchini Misri. Watu waliokuwa humo ambao asilimia kubwa walikwenda kutalii wakatoka huku wakikimbia kwani mbali na kelele hizo, piramidi hilo halikuwa la kawaida, lilikuwa linatisha kiasi kwamba hata watalii waliokuwa wakiingia, walishikana mikono kama njia mojawapo ya kutokutana kuuawa na majini yaliyosadikiwa kwamba yalikuwepo ndani ya piramidi hilo.

Mwanamke yule aliyekuwa amepiga kelele akatoka huku akitetemeka, kijasho chembamba kikimtoka, walinzi waliokuwa mahali hapo wakamsogelea kwa lengo la kutaka kufahamu kilichomfanya mpaka kupiga kelele kiasi hicho hadi kuwaogopesha watu wengine.
Walipomuuliza mwanamke huyo wa Kiingereza akawaambia kwamba aliiona maiti ndani ya piramidi hilo kitu kilichomtisha kila mtu.

“What?” (nini?) aliuliza mwanaume mmoja.
“A deadbody!” (maiti)
“Are you sure?” (una uhakika?)
“Yes!” (ndiyo) alijibu mwanamke huyo huku akiendelea kutetemeka kwa hofu.
Watu wote waliotoka ndani ya piramidi hilo wakaanza kumwangalia mwanamke yule, wengine hawakuridhika, wakamsogelea na kumuuliza kilichokuwa kimetokea ndani ya piramidi lile, hakuficha, aliwaambia wazi kwamba aliiona maiti ikiwa chini kitu kilichomfanya kupiga kelele na kukimbia.
“Siyo kwamba umeona mauzauza?” aliuliza jamaa mmoja.

“Kwani mauzauza siyajui? Nimeona maiti!” “Sasa kwa nini ulikuwa peke yako na wakati hairuhusiwi?” aliuliza mwanaume mwingine.
“Niliingia na mume wangu! Yeye alikwenda upande mwingine na mimi kwenda mwingine,” alijibu mwanamke huyo na mumewe kutokea hapo, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumkumbatia mkewe.

Walinzi waliokuwa hapo wakachukua tochi zao na kuingia ndani ya piramidi hilo, walitaka kuona kile alichokiona mwanamke huyo. Kwa miaka mingi, tangu karne ya ishirini ilipoingia hakukuwa na mtu yeyote aliyekufa ndani ya piramidi hilo japokuwa kulikuwa na tetesi za kuwepo kwa majini. Kama hakukuwa na mtu aliyekufa! Iliwezekanaje mwanamke huyo kuona maiti humo?View attachment 726704
 
Back
Top Bottom