SEHEMU YA 45
Marafiki wa Saed nao hawakutaka kukubali, kwa kuwa Fareed alionekana kuwavutia tena huku kwa nyuma akianza kutuna na kifua kuonekana, hawakutaka kumuacha, walichokifanya ni kuanza kummendea kitu ambacho kilimfurahisha kwani akili yake ilifikiria fedha kuliko mapenzi.
Alipokea meseji nyingi kutoka kwa wanaume mbalimbali, wote walimtaka kimapenzi. Hakuwa mchoyo, alikubali kufanya nao na hivyo kukutana nao sehemu yoyote waliyotaka na kuwaridhisha.
Ndani ya mwezi mmoja akatembea na marafiki kumi wa Saed, hakuwa akijua, alipokuwa naye alikuwa akimsifia kwa marafiki zake kumbe ndiyo haohao waliokuwa wakimbadilikia kila alipowapa kisogo.
Wakati mwezi wa pili ulipokatika, ndipo akaingia kwenye umbo rasmi la kike, alikuwa na muonekano kama wa wanawake wengine, alikuwa na kifua kikubwa, wowowo, mavazi ya kile, alijitahidi kuibadilisha sura yake kwa kuipaka sana poda, akaseti nywele zake, kwa kifupi alikuwa mwanamke kamili isipokuwa sehemu za siri ambapo alishindwa kuibadilisha.
“Hivi huyu mpumbavu Keith anaendelea kunisubiri au? Asahau! Mimi siwezi kuwa na bwana mmoja. Kwanza ukila ugali kila siku utachoka, siku nyingine kula wali, ukiuchoka, kula pilau, nalo ukilichoka, nyonya koni,” alijisemea huku akiirambaramba midomo yake kama mwanamke aliyepewa ahadi ya kukutana na mwanaume kwenye nyumba ya wageni.
Wakati yeye akifikiria hayo yote, upande wa pili Keith alikuwa na hasira kali, hakuamini kama kweli Fareed alikuwa amemtenda kiasi hicho na wakati alikuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha kumgharamia.
Hakukubali, moyo wake ulijaza ghadhabu nzito na alikuwa tayari kufanya lolote lile kumshughulikia mwanaume huyo.
Alimtafuta, aliwaagiza vijana wake kila kona hapo Los Angeles kumtafuta na kumleta kwake. Vijana hao wakafanya kazi usiku na mchana, wakazunguka katika Cassino mbalimbali lakini hawakuweza kumuona.
Hawakuishia hapo, wakazunguka kwenye miji mingine lakini napo hawakuweza kumuona kitu kilichowapa maswali mtu huyo alikuwa wapi.
“Tumemtafuta sana! Hatujamuona!” alisema kijana mmoja.