SEHEMU YA 40
Baada ya dakika arobaini na tano, kila mmoja alikuwa hoi. Dk. Fabby alimwangalia Fareed, moyo wake ukajisikia hukumu nzito na kulaumiwa kwa kile alichokuwa amekifanya. Hakujua ni shetani gani alimuingia mpaka kumpelekesha namna ile na kuamua kufanya ushenzi mkubwa kama ule.
Alijuta moyoni mwake, alishindwa kumwangalia Fareed, akaelekea choooni. Huko, alibaki akilia kwa maumivu mazito, huzuni kubwa ilimuingia na hakuamini kama ingetokea siku ambayo angefana ushenzi mkubwa kama huo.
Alimlaumu shetani, alimpa tamaa mbaya ambayo ilimfanya kuusaliti moyo wake na Mungu wake. Kule chooni hakutoka haraka, alikuwa akilia kwa majuto makubwa.
Fareed alipoona Dk. Fabby anachelewa kutoka, akausogelea mlango na kuugonga. Daktari huyo alishtuka na kukumbuka kwamba kulikuwa na kazi aliyotakiwa kufaya, hivyo harakaharaka akanawa uso na kutoka nje.
Hakutaka kumchangamkia Fareed, alichokifanya ni kumpeleka kitandani, akamlaza na kisha kumchoma sindano iliyokuwa na dawa ya kuyaongeza makalio yake kidogo na kifua chake, awe na muonekano kama mwanamke mbichi.
“Tayari!” alisema Dk. Fabby huku akimwangalia Fareed.
“Nashukuru mpenzi!” alisema Fareed huku akimshika kidevu Dk. Fabby lakini akajikwepesha.
“Eeh! Jamani una nini?” aliuliza Fareed.
“Nenda nyumbani!”
“Sawa. Lakini usikose kunipigia.
Nitakumiss sana,” alisema Fareed, Dk. Fabby hakuzungumza kitu chochote kile, akamuondoa Fareed chumbani humo.
Hilo hakutaka kulijali sana, Fareed ni akaondoka hospitalini hapo. Moyo wake uliridhika kwani hicho ndicho kitu alichokifanya kila siku. Aliuchukia muonekano wake na alipogundua kwamba baada ya siku chache angekuwa na muonekano wa kike, akafurahi zaidi.
Alipofika nyumbani, akaelekea chumbani na kutulia kitandani. Akachukua simu yake na kuanza kumpigia Dk. Fabby lakini mwanaume huyo hakuhitaji mazoea tana.
“Lakini mbona unanikataa?” aliuliza Fareed.
“Naomba uniache!”
“Nikuache upumzike?”
“Yaani uniache moja kwa moja. Usinijuejue,” alisema Dk. Fabby na kukata simu.
Fareed alihuzunika lakini hakuwa na jinsi, hakutaka kuwasiliana na Dk. Fabby kwani hakumpenda kama alivyompenda Keith ambaye alikuwa tayari kumpa kiasi chochote cha fedha japokuwa hakutaka kumwambia ukweli.