SEHEMU YA 41
“Haina shida.”
Akakaa na kumsubiria mzee huyo. Alimwambia kwamba angefika nyumbani hapo muda si mrefu. Akajiachia kochini huku moyo wake ukiwa na amani kwamba alifanikiwa kulala na Dk. Fabby, hata kama hakumtaka tena kwake wala hakulijali sana.
Baada ya saa moja, Keith akafika nyumbani hapo. Alipomuona Fareed, akamfuata na kumkumbatia. Alimkumbuka na muda wote alikuwa akimuwaza yeye tu. Walikaa na kuzungumza, Keith hakutaka kumwambia ukweli Fareed jinsi alivyokuwa akijisikia ila alijua kwamba mwanaume tata huyo alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Umefanikiwa?” aliuliza Keith.
“Ndiyo!”
“Safi sana, hebu nione,” alisema mwanaume huyo na kutaka kuonyeshewa.
Hilo halikuwa tatizo kwa Fareed, akavua nguo zake na kisha kumwangalia. Mapigo ya moyo wa Keith yalikuwa yakienda kasi, hakuamini kama alikuwa akimwangalia mwanaume huyo.
Mwili wake ukamsisimka, hakutaka kukubali, akamchukua Fareed na kwenda naye kitandani, hapo, akaanza kumwambia maneno mengi ya mahaba, jinsi alivyokuwa akimpenda, hakuacha kumsifia kwa kila kitu kiasi kwamba Faredd akajiona kuwa mzuri kuliko watu wote duniani.
“Kweli?”
“Ndiyo! Wewe ni malaika wangu, ni mrembo kuliko warembo wote waliowahi kutokea katika hii dunia!” alisema Keith maneno ambayo alikuwa na uhakika kwamba hayakuwa kweli bali alitaka kukamilisha kile alichokitaka.
Fareed akaachia tabasamu pana, akajiangalia, akahisi kwamba kweli alikuwa mrembo kuliko warembo wote waliowahi kutokea katika dunia hii. Akashikwa mkono, akaacha, akashikwa bega, akaacha, kila alipokuwa akishikwa huku na kule, aliacha na mwisho wa siku, baada ya saa moja wote kujikuta wakiwa hoi kitandani.
“Ahsante,” alisema Fareed huku akimwangalia Keith kwa uso uliokuwa na tabasamu pana.
“Umeridhika?”
“Sana mpenzi! Kumbe nilikuwa najichelewesha tu!” alisema Fareed huku akimwangalia mwanaume huyo.
Penzi jipya likaanzishwa, kila mmoja alikuwa bize na mwenzake, japokuwa Keith alikuwa na familia yake jijini New York lakini hakutaka kurudi huko, alitekwa na biashara zake zote alizihamishia huko, mahesabu akawa anapelekewa hukohuko alipokuwa.