Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

Hii hadithi inakera sana, mtu una scroll kweli kupata hadithi lakini unakuta ishu zisizo furahisha
 
SEHEMU YA 139

Hawakujua kama lengo la watu hao ni kumpata mwanaume aliyekuwa ndani ya hoteli hiyo. Wakati mwingine walikuwa wakikaa mapokezini, Belleck alipokuwa akiingia ndani ya hoteli ile na machangudoa walikuwa wakimuona hivyo kuwa kazi nyepesi kwao kufanya kile walichokuwa wakikitaka.

“Cha kwanza ni kupata kadi ya kufungua vyumba vyote,” alisema De Leux.
Hilo ndilo lililotakiwa, kwa kutumia uzoefu mkubwa wa kuzungumza waliokuwa nao, wakajenga ukaribu zaidi na mhudumu aliyeitwa kwa jina la Natalie ambaye bila tatizo lolote lile, naye akaukaribisha ukaribu huo na mwisho wa siku De Leux kumtongoza.

“Acha masihara wewe! Mzuri mimi?” aliuliza Natalie huku akitabasamu, japokuwa alipinga kwamba hakuwa mzuri lakini sifa zile zilimfurahisha.

“Wewe ni mzuri sana. Una tabasamu pana, msichana mrembo sana! Umeumbinka kama Mona Liza,” alisema De Leux huku akimwangalia Natalie kwa macho ya nipe nikupe.

Akamsifia usiku mzima, msichana huyo akachanganyikiwa, kila wakati akawa anapandisha juu mpaka katika chumba alichokuwa akilala De Leux na kuingia ndani. Hakutaka kufanya mapenzi na msichana huyo, kitu muhimu kilikuwa ni kuweka ukaribu na mwisho wa siku kuichukua kadi ambayo alikuwa akiitaka mno.

Wakati walipokwenda kuonana na Fareed, walimwambia kabisa kile kilichokuwa kimetokea kwamba kulikuwa na kadi moja muhimu ambayo ingewawezesha wao kuingia ndani ya chumba chochote kile.

Fareed akafurahi kwani urahisi huo ndiyo aliokuwa akiutaka kwa hali na mali. Siku hiyo wakaondoka na kwenda katika hoteli hiyo. Wakachukua chumba kwa ajili ya Fareed ambaye akaingia bila tatizo na uzembe mkubwa ambao waliufanya wahudumu wa hoteli hiyo ni kutokuishikilia passport yake.

Akaingia mpaka chumbani, akajipumzisha na kuambiwa kwamba mtu aliyetakiwa kumuua alikuwa njiani kufika mahali hapo hivyo alitakiwa kusubiri.

De Leux na mwenzake wakarudi mapokezi, wakatulia kochini. Ilipofika saa sita usiku, wakamuona Belleck akirudi hotelini hapo huku akiwa na mwanamke ambaye alivalia hijabu ila kwa nyuma alijazia hasa kiasi kwamba hata wao walipokuwa wakimwangalia walimtamani kupita kawaida.
 
SEHEMU YA 140

“Huyo hapo! Subiri!” alisema De Leux.
Wakati mwanaume huyo akiingia ndani na mwanamke huyo, De Leux akamuita Natalie na kuanza kuongea naye.

Alimwambia wazi kwamba siku hiyo alitaka kukaa naye na kuzungumza naye mambo mengi lakini iwe baada ya kufanya usafi katika vyumba mbalimbali.
“Haina shida mpenzi! Nitakuja,” alisema Natalie huku akionekana kuwa na furaha tele.

De Leux akaondoka na mwenzake mpaka chumbani kwake, wakakaa huko na kuyapanga kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa mtu huyo ambaye alikuwa adui wa bosi wao kwa kipindi kirefu.

Wakamfuata Fareed na kumwambia kilichokuwa kikiendelea kwamba ni yeye tu ndiye aliyekuwa akisubiriwa kufanya mauaji hayo.
“Haina tatizo!”

“Sawa. Ngoja nimuite huyu msichana alete kadi,” alisema De Leux na hapohapo kuchukua simu ya mezani na kupiga mapokezi ambapo alimtaka Natalie aende huko kuchukua shuka kwenda kulifua.

Msichana huyo hakuchelea, baada ya dakika kadhaa, akawa ndani ya chumba hicho. Alijua fika kwamba hakuitwa kwa ajili ya kubadilisha shuka bali aliitwa kwa sababu kulikuwa na kitu kingine.

Alivaa kimitego na hata alipoingia ndani ya chumba hicho, kitu cha kwanza kabisa ni kuipandisha sketi yake kwa juu, upaja wake ukaonekana, kidogo De Leux akatetemeka.

“Mmh! Leo hatoki!” alijisemea huku akimwangalia msichana huyo kwa matamanio makubwa. Ila akili yake haikuhama kutoka kwenye kadi ile.

Ilikuwa ni lazima aipate na kumpelekea Fareed ambaye angefanya kazi hiyo aliyokuwa ameifuata nchini Ufaransa. **** Huo ndiyo ulikuwa muda wa kukamilisha alichokuwa akikitaka.

Alimwangalia Natalie kwa macho yaliyomaanisha kwamba alimtaka sana kitandani hapo. Msichana huyo pasipo kugundua kwamba kila kitu kilichofanyika kilikuwa ni maigizo, akaanza kumfuata mwanaume huyo.

Hatua zake zilikuwa za taratibu, za mahaba zilizoashiria kwamba alimuhitaji sana De Leux, mwanaume huyo akasimama na kumsogelea, alipomfikia, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuuwahi mdomo wake na kuanza kubadilishana mate.
 
SEHEMU YA 141

Zoezi hilo liliambatanisha na kushikana hapa na pale. Wakati yote yakiendelea, akili ya De Leux ilikuwa kwenye kadi aliyokuwa nayo msichana huyo, hakutaka kupoteza lengo lake kwani aliamini kwamba kama asingefanikisha suala hilo muda huo basi kazi waliyokuwa wakiitaka isingeweza kufanyika.

Wakapelekana mpaka kitandani, wakavuana nguo na kuendelea na zoezi lao. Miguno ya kimahaba ilikuwa ikisikika kila kona na baada ya muda fulani, sauti zile ziliongezeka zaidi.

Kulikuwa na mwanga hafifu, Natalie alichanganyikiwa, muda wote wakati mwanaume huyo alipokuwa juu yake, aliyafumba macho yake, hisia za raha zilikwenda mpaka kwenye ubongo wake, zikamchanganya kiasi kwamba akaona hakukuwa na kitu kilichokuwa na raha duniani kama hicho kilichokuwa kikiendelea kitandani hapo.

De Leux akachukua nafasi hiyohiyo kupekua katika mifuko ya msichana huyo, alichokuwa akikitaka ni kadi iliyokuwa na uwezo wa kufungua milango yote, hilo wala halikuwa zoezi gumu kwani ndani ya sekunde chache, tayari alikuwa na kadi hiyo mkononi mwake.

Akaificha kwenye mfuko wa suruali yake, alipomaliza kufanya mapenzi na msichana huyo, wakabaki wamelala huku wakivuta raundi ya pili iendelee.

Muda wote Natalie alikuwa akifikiria ngono, kilipita kipindi kirefu pasipo kufanya mchezo huo na ndiyo maana alipoambiwa aende chumbani kwa mwanaume huyo, hakutaka kujiuliza, haraka sana akaenda tena huku akiwa amejiandaa kikamilifu.

“Una pumzi sana,” alisema natalie huku akiupeleka mkono wake chini ya kiuno cha De Leux.
“Kweli?”

“Yeah! Sijawahi kukutana na mwanaume mwenye pumzi kama wewe. Halafu unajua, kuna wakati nilihisi kama unataka kunivunja kwa jinsi ulivyokuwa ukinikunja,” alisema msichana huyo huku mkono ule ukiwa kulekule.

“Pole sana jamani! Ila nataka tuendelee!”
“Wewe tu! Mimi nipo tayari!” alisema De Leux.

Hata kabla hawajaendelea, De Leux akasimama na kumwambia Natalie kwamba alitaka kwenda kumuona rafiki yake kwamba ikiwezekana asimpigie simu asubuhi sana kwani ilikuwa ni lazima alale na msichana huyo ambaye kwa siku inayofuatia ilikuwa ni ya mapumziko kwake.
 
Hizo sehemu za nanilii ungeweka nyota nyota...

Mwezi siyo rafiki kabisa... wahurumieni watu...

Cc: mahondaw
 
Bora walivyomalizana haraka haraka...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom