Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 133

“Let’s roll with him,” (twende naye huyo) alisema Frankline, mmoja wa FBI waliokuwa wakifuatilia tukio hilo.

Kwa kutumia kamera mbalimbali waliweza kumfuatilia Fareed aliyekuwa akikimbia, alipofika chooni, akaingia na kisha kutoka na kuendelea kukimbia.

Wakahisi kwamba huyo ndiye aliyekuwa amehusika na mlipuko ule, wakaendelea kumfuatilia mpaka nje, kituo kikalipuka, na yeye mwenyewe akarushwa na kujipigiza katika gari moja.

“Take his picture,” (chukua picha yake) alisema Frankline na mwenzake kufanya hivyo, walivyoikuza, wakamgundua, picha ikaprintiwa na mpaka gari la wagonjwa lilipomchukua na kuondoka naye, walikuwa wakifuatilia kila kitu.
“Which hospital?” (hospitali gani?)
“St. Joseph!”

“Let’s go…let’s go,” (twendeni…twendeni) alisema Franckiline, maofisa wanne wa FBI waliokuwa na bunduki wakaanza kwenda kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kumkamata Fareed ambaye walikuwa na uhakika kwamba alihusika kwa asilimia mia moja katika mlipuko huo.

Wakawapa wenzao taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea, hawakuishia kuwataarifu bali wakawatumia na picha za mwanaume huyo na kwamba walikuwa njiani kwenda kumkamata.

Kwa kuwa mahali hapo hakukuwa mbali na hospitali, ndani ya dakika kumi wakafika na moja kwa moja kuingia ndani. Kulikuwa na idadi kubwa ya watu, wengi waliokuwa mahali hapo walifika kwa ajili ya kuwaona ndegu zao waliokuwa hoi.

Wakazungumza na madaktari na kumuonyeshea picha ya Fareed, kwa kuwa daktari huyo alikuwa akiwakumbuka watu aliokuwa amewapokea, hakukuwa na ugumu kugundua kwamba picha ya mtu aliyekuwa ameonyeshewa alikufikishwa ndani ya hospitali hiyo saa moja iliyopita.

“Where is him?” (yupo wapi?)
“Come with me,” (nifuateni) alisema daktari huyo na kuanza kumfuata.
Daktari yule akawapeleka mpaka katika wodi aliyolazwa Fareed ambapo akawakabidhi watu hao kwa nesi aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa waliokuwa katika wodi hiyo.

Alipoonyeshewa picha ya Fareed, alimgundua kwani alikuwa miongoni mwa wagonjwa waliokuwepo humo ndani.
“I know him,” (namfahamu)
“Where is he? (yupo wapi?)
 
SEHEMU YA 134

Nesi yule akawachukua mpaka katika kitanda alicholazwa Fareed, walipofika, mwanaume huyo hakuwepo na alipomuuliza nesi mwenzake akamwambia kwamba Fareed alikuwa amekwenda chooni.

“Where is the toilet?” (choo kipo wapi?)
“Come with me,” (nifuateni) alisema na kuanza kumfuata nesi huyo kwenda huko chooni.

**** Maofisa wale wa FBI na nesi yule wakafika ndani ya choo kile, wakaangalia huku na kule, mtu waliyekuwa wakimtafuta hakuwepo humo.

Nesi alishindwa kuelewa kwamba ilikuwaje Fareed asiwe humo na wakati alimuona akielekea chooni na hakuwa na uhakika kama mwanaume huyo alikuwa ametoka.

FBI hawakutaka kuridhika, walijua kwamba mwanaume huyo alikuwa ndani ya vyoo hivyo, wakaendelea kumtafuta kwenye kila choo lakini hawakuweza kumuona.

Hawakutaka kukata tamaa, waliamini kwamba kama mwanaume huyo hakuwa chooni humo basi atakuwa ametoka, na kama ni kipindi kifupi kilichopita waliamini kwamba hakuwa mbali kutoka mahali hapo.

Wakaelekea sehemu zingine ndani ya hospitali hiyo lakini hawakuweza kumuona Fareed, wakaelekea mpaka nje kabisa lakini kila kona waliyoangalia, mwanaume huyo hakuonekana machoni mwao.
“Where is he?” (yupo wapi?) aliuliza ofisa mmoja.

“I don’t know! He just went to the toilet,” (sijui! Alikwenda chooni) alijibu nesi.

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU 135

Fareed alikuwa chooni, moyo wake haukuwa na amani hata kidogo, aliamini kwamba ilikuwa ni lazima kutafutwa kwani alikumbuka kwamba katika kituo kile cha treni kulikuwa na kamera ndogo za CCTV hivyo kugundulika lilikuwa suala jepesi sana.

Hakutaka kubaki humo, ilikuwa ni lazima kuondoka kuelekea popote pale lakini si kuona akikamatwa kwa kufanya jambo ambalo alilazimishwa kulifanya pasipo kujua kama lilikuwa kosa lolote lile.

Akaondoka na kuelekea nje ya choo kile, hakutaka kuonekana, aliondoka mpaka kufika nje huku akikutana na madaktari wengi ambao hawakumuuliza kitu chochote zaidi ya kumuacha tu.

Alijipekua mfukoni, alikuwa na kadi yake ya benki ambayo ilimuwezesha kuchukua kiasi chochote cha pesa sehemu yoyote ile. Akaelekea mpaka katikakibanda cha ATM na kutoa kiasi cha dola mia tano na kuondoka zake.

Safari yake iliishia katika hoteli ya kawaida ya Windows iliyokuwa hapohapo Pennyslvania, akachukua chumba ambacho alitakiwa kulipa dola mia mbili hamsini, zaidi ya laki tano kwa usiku mmoja tu.

Hilo halikuwa na tatizo, alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha ambacho angeweza kufanya jambo lolote lile, hivyo akaelekea katika chumba hicho. Hakulala, alibaki akifikiria namna alivyonusurika kuuawa kwa kulipukiwa na bomu.

Moyo wake ukawa na ghadhabu, akawa na hasira na Waarabu kwani aliamini kwamba watu hao hawakuangalia utu, hawakujua ni watu wangapi waliwakosea, katika kuua, waliua kila mtu hata kama hawakuwa na hatia kama alivyokuwa.

Hakutaka kuwafikiria sana Waarabu, alichokitaka ni kusonga mbele na kutekeleza kile alichokuwa akikitaka. Aliingia nchini MArekani kwa lengo la kumuua Bilionea Belleck ambaye aliamini kwamba alikuwa nchini humo.

Akaanza kufuatilia, alikuwa na marafiki wachache nchini humo ambao wangekuwa na data zote kuhusu bilionea huyo na kwa jinsi gani angeweza kumpata.

Kwa kuwa bilionea Belleck alikuwa na maadui wengi akiwemo bilionea mwenzake, Peter Williams, alichokifanya ni kumpigia simu.

“Unanikumbuka?” alimuuliza bilionea huyo ambaye aliwahi kutambulishwa na Bilionea Belleck kabla ya wawili hao kutofautiana kwenye mambo ya kibiashara.
 
Back
Top Bottom