TANZIA Michael Ngaleku Shirima mmiliki wa Precision Air afariki dunia

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,611
IMG_5098.jpeg


Mmiliki wa Shirika la Ndege Nchini Tanzania la Precision Air, Michael Ngaleku Shirima, ameaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya AgaKhan, Jijini Dar es Salaam

===========

Mfahamu zaidi Michael Ngaleku Shirima

Michael Ngaleku Shirima CEO wa Shirika la Ndege za Precision Air alianza kufahamika zaidi na watu baada ya ndege za shirika kukumbwa na tafrani za hapa na pale zikihusisha ajali iliyotokea jijini Mwanza ambapo ndege ya shirika hilo ilishindwa kutua katika uwanja wa ndege Bukoba na kulazimika kugeuka Mwanza ambapo rubani aliona ni vyema kuishusha ndege hiyo kweye maji ya ziwa Victoria.

Michael Shirima ni moja kati ya wapambanaji ambao wamepambana kutoka chini hadi kufikia mafanikio ya juu kwa kuwa alikuweka ujasiri na kutokata tamaa. Michael alizaliwa mwaka 1943 huko Usseri Rombo Mkoani Kilimanjaro, baada ya kumaliza shule na kila kitu aliamua kuingia katika ulimwengu wa wachakarikaji kukimbiza ndoto zake ambazo alizigeuza kuwa mipango na baadaye utekelezaji.

Michael aliajiriwa kwa muda kidogo na hapa anasema “Nilipokuwa naanzisha Shirika la ndege la Precision Air haikuwa kama lilivyo sasa hivi lilianza kidogo, likakuwa. Nimekulia kwenye Taasisi ya usafiri wa anga. Nilipofikisha miaka 18 ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia kwenye mambo ya ndege (ilikuwa ndege ndogo). Ndipo ilipoingia kwenye damu na ijapokuwa nilibadilisha mawazo mara kwa mara lakini nilirudi kwenye wazo langu. Sikuanzisha Precision Air moja kwa moja lakini nilifanya kazi kwenye Shirika la ndege ya East African Airways kwa miaka 12 Jijini Nairobi. Lilikuwa ni Shirika la Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda”

“Mtaji wa kuanzisha Kampuni ya Precision Air niliutoa kwenye Kahawa. Ni kazi ambayo ilikuwa haifanywi na watu wengi. Na pia nilikuwa dereva wa malori. Nilikuwa napeleka mizigo Mwanza kutoka Moshi. Nilikuwa napeleka mbao kule. Pia nilikuwa nanunua mafuta ya pamba naleta Moshi” Mzee Michael Shirima, Founder wa Precision Air na Mwandishi wa kitabu cha On My Father Wings

“Tuna wafanyakazi 300. Hii kazi ni ngumu Sana, sio watu wengi wanaweza kuifanya. Kuna Mtaalamu aliandika kwamba ukitaka kuwa Milionea (Dola kwa mfano) uwe Bilionea halafu uingie kwenye kazi ya kuendesha Shirika la ndege ndio utakuwa Milionea. Na huingii kwenye kazi hii ili uwe tajiri au utengeneze fedha hapana unaingia kwenye kazi kwa sababu ya kupenda passion. Na Mimi sifanyi kazi kwa maono nafanya kazi iliyopo sasa hivi”
 
Rest well Michael Ngaleku Shirima
Tunamshukuru Mungu kwaajili ya zawadi ya uhai wako. Umetumikia utume wako kwa nguvu na maarifa. Umeumba! Na umeacha alama duniani

Pole kwa familia na wote walioguswa na msiba huu
 
Mtu wa 1943 ni classmate wako na bado una uwezo wa ku type humu? Kweli kuna watumna bahati zenu na maisha !!!
Classmate sio lazima primary au sekondary. Hata kwenye mafunzo maalum ambayo kijana wa kampuni A anaweza kutana na mzee wa kampuni B wote wakiwa wanafunzi kwa muda fulani. Ukumbuke pia Kuna watu wanasoma Phd wakiwa na 30's na wengine 60's.
 
Back
Top Bottom