Tatizo kubwa hapa ni maudhui ya hii thread ya Bishanga kuwa kila mwanaume ni mlevi, kila mwanaume ni mshabiki wa mpira wa miguu hasa ligi ya uingereza, kila mwanaume ni fuska na ana nyumba ndogo au anatembea na house girl, kila mwanaume hana muda na familia yake na amewatelekeza watoto. Hii siyo sahihi hata kidogo na mtu responsible hawezi akaiacha mada kama hii ipite bila kurekebishwa. Nimefuatilia thread za akina mama inaonekana wengi wanakubaliana na huo mtazamo wa Bishanga na wengine wanahamu ujumbe uwafikie waume zao. Wasichotaka kukiri ni kuwa wapo wanaume wengi ambao hawaingii kwenye hii "stereotying" ya Bishanga kuhusu wanaume. Hii thread haiwatendei haki wanaume ambao:
- siyo walevi kwa hiyo hawakai bar muda huo anaosema Bishanga,
- siyo washabiki wa mpira wa miguu kiasi cha kukesha wanaangalia mpira,
- wanahudumia familia zao kwa hali na mali,
- wake zao wanafanya kazi na bado wanawapa huduma zote kama wanawake ndani ya nyumba,
- hawadeki wanapougua kama anavyotaka kutuaminisha,
- hawana muda wa kunyang'anyana remote na watoto - Mfano kwangu watoto hawaruhusiwi kuangalia TV muda wote na vipindi wanavyoangalia vinadhibitiwa: siyo kila kipindi watoto wanaruhusiwa kuangalia; Huo ni utaratibu wa taasisi ya familia yetu ya Tata & family.
- hawaongei habari za wake zao nje - hili hata mila na desturi zetu wengine haziruhusu na sijawahi kukaa chini na rafiki au hata ndugu zangu kujadili matatizo ya familia yangu. Siamini kama hii ni njia sahihi ya kutatua matatizo kama yapo.
- Hawatembei nje na vimada/malaya
Hoja yangu ya msingi ni kuwa siyo sahihi kuchukua tabia mbovu za wanaume wachache ukadhani ndio tabia za kila mwanaume. Sipingi kimsingi kuwa kuna baadhi ya wanaume wana hizo tabia kama ambavyo tumeshapata ushuhuda wa baadhi ya wachangiaji wanawake humu ndani - Japo siamini kuwa wote waliochangia wanakutana na matatizo hayo. Ni muhimu kuwaeleza hata hao kina mama wenye wanaume wasiowajibika "irresponsible" kama hawa wa Bishanga kuwa siyo kila mwanamke aliyeolewa anakutana na matatizo kama hayo.