Mianaume ndo tulivyo......hovyoooo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mianaume ndo tulivyo......hovyoooo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bishanga, Nov 17, 2011.

 1. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Hebu fikiria:

  1.Uko ndani ya ndoa,mwaka wa kumi sasa na hamjapata mtoto,mkeo hospitali zote kamaliza na anaambiwa hana tatizo,kila akikwambia na wewe ukapimwe hutaki unajidai huna tatizo,ndo nini sasa hiyo? Kwa nini usipimwe mkajaribu IVF?

  2.Ukienda Rose Garden we ndo Reginald Mengi kazi kuzungusha raundi huku ukijidai kusema...'uza nyumba utunze heshima bar'....asubuhi mwanao akikwambia 'baba shati la shule limechanika'..unakuwa mkaaaaaali,hovyooooo!

  3.Umetoka zako kwenye mipombe,ni saa saba za usiku ,mama siku nzima mihangaiko kachoka we ukifika kitandani na ny....zako unamrukia tu bila hata maandalizi....ku ku...ku .....aaaaaaaagh....halafu huyo unakoroma,yaani mpaka mkeo anaona ka alikuwa anaota hivi,jamani hiyo sio baiskeli ya gym huyo ni binadamu ati.

  4. Mnawaita beki tatu ma haus geli hao,juu ya nini unajipoza kwa mtumishi wa ndani? huoni unamdhalilisha mwenzio? Hivi ukibambwa utasema nini?

  5.Ulipompenda ulimkuta ana kakazi kake,we na miwivu yako hutaki afanye kazi unamwachisha,hivi una uwezo wa kumpatia mahitaji yake yote yakiwemo matunzo ya wazazi na ndugu zake? Halafu kwa nini utake mwenzio kazi yake iwe kusafisha makochi na kuangalia plasma wakati wewe uko bize unachangamsha mwili na akili? Kufanya kazi au biashara is more than kuingiza kipato ,na ku interract na watu pia is healthy.

  6.Mkeo akikusoea unaanza kumtangaza kwa watu...'mkeo wangu sijui yukoje....mara hivi mara vile.....huoni unajiaibisha mwenyewe?

  7.Na hizo nyumba ndogo hizo,ukienda huko kazi kumsimanga mkeo,matokeo yake siku mkeo akigombana na hawara yako anashangaa matusi anayovurumishiwa...we nae mwanamke wewe...si kikojozi wewe....du toba yarabi!

  8.Ukiumwa kidogo tu full madeko yaani unajitia hata kidole huwezi kukisogeza,mwenzio serious tumbo linamsumbua,hata kusema ngoja nikae ndani nimuuguze mwenzangu ndo kwaaaanza unawahi kaunta Jackies,sana sana unampigia simu dada yako akamwangalie wifi,inahuu kwani yeye ndo kamwoa,akilalamika mkeo unamsimanga eti anadeka.

  9.Nje utembee sasa ndo hata kuzaa uzae kabisa huko? maduka zinakouzwa condoms huyajui? au utasingizia ilikupasukia,na wa pili nayo ilipasuka? acheni hizo!

  10.Huko kwenye mabaa na huo upuuzi unaoongelewa huko ....eh chapati shurti ikaangwe pande zote...sijui nini sijui nini...unarudi nyumbani na mipombe yako unataka ujaribu upuuzi wako kwa mkeo,peleka huko ujinga wako.

  11.Umelala nje asubuhi unajitia kurudi nyumbani umefungwa pingu ili mke aone ulilala kituoni,mambo ya 1947 hayo,kinamama hawadanyiki na hizo siku hizi!

  12.Mpira ..mpira...mpira....hamchoki? wikiendi nzima uko bar unaangalia mpira ,jumamosi man siti vs man yu,jumapili aseno vs chelz, weekdays kazi,hivi lini unakaa na kukagua kazi za watoto za shule? lini unakaa na mke na wanao na ku chat nao? mpira ndo utakaokuzika?

  13. Ubinafsi wako huo,ukikaa sebuleni remote control haiko mbali na wewe unabadilisha tu chanel,si umuulize mkeo au wanao kama nao kuna kitu wanataka kuangalia? kuna mtu aliwahi kusema eti wanaume huona remote control kama ni extension ya mb....zao.

  14.Sijui ndo umepiga wapi kabomu kako cha kwanza unamnunulia hawara yako ka vitz wakati mkeo anapanda daladala,kha!

  15.Mke akilalamika mitabia yako mibovu unaanza..'kwani unataka nini..gari nimekupa..zaabu nakununulia...frigi imejaa chakula...kelele za nini? kwani kwao hakuacha chakula? yeye alikufuata wewe ati na sio plasma yako.

  .......itaendelea....leo wababa wa humu ndani nakula nao sahani moja!
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mhhhhh sitaki kuongeza neno duh balaa hili
  Afu na mengine unafanya wewe hapo
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  dahhh
  Naona leo hii ni zamu ya wanume thread
  ya tatu hii sasa nakumbana nao kuhusu wanaume.dahhh..
   
 4. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  wapashe wapashike aoooo....ila jiangalie watakugechaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  hujambo mamitoo.
  muda kidogo sjakuona..
   
 6. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kama vile unamsema Mume wangu!Kha!Kama we hufayagi hata moja kati ya hayo basi you are the perfect man I have ever met
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ajisafishe kwanza na yeye
  Aseme ni yapi kati ya hayo ambayo hafanyi
  Au amechukulia mfano wake kuja kutupa taarifa hapa
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe umejuisha wanaume wote, ilihali wa kawako tu ndio anakufanyia hayo. Umesahua kuwa binadamu wanatofautiana kutoka mmoja kwenda mwingine. Wengine akili ya kuambiawa anachanganya na yake kuacha ushauri mbaya pale pale. Sio mianaume yote, mingine ina malezi mazuri, inajali.
   
 9. King2

  King2 JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mada ipo Juu ya umri wangu.
   
 10. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahaha ngoja nifurahi kidogo maana na fukuto nililonalo kwenye koo leo naweza meza mtu!
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  kakwambia nani? mimi ndo mme mkamilika, sina doa hata moja! muulize memba flan humu mmu atakwambia.
   
 12. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie namtafuta mmoja ambaye hana kati ya hayo yalioorodheshwa................tunaruhusiwa kuongeza mengine.


   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  umefurahi AD? ongezea basi kero nyingine.
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hivi ni wanaume au wavulana?????
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ubarikiwe na ibarikiwe ndoa yako
   
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hagechwi mtu hapa.
  halafu wewe na jicho lako hilo? haya....
   
 17. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I wish aingie apa leo
   
 18. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  wakuu_mimi napita hapa.
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  we acha tu,i am more than perfect!
  sasa mzee unamzibiti vipi?
   
 20. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  nitarejea
   
Loading...